Kenya yafikiria sera ya mwanamke 1 watoto 2

Kenya yafikiria sera ya mwanamke 1 watoto 2

Phlagiey

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
3,500
Reaction score
1,688
[h=1][/h] Utafiti uliofanywa nchini Kenya umeonesha taifa hilo litashindwa kufikia dira yake ya maendeleo ya mwaka 2030 kutokana na wingi wa watu na sasa linataka kuanzishwa sera ya mwanamke kutozaa zaidi ya watoto wawili.
Mtoto wa Kiafrika.

Ripoti ya utafiti huo iliyopewa jina la "Uchambuzi wa Hali ya Idadi ya Watu nchini Kenya" na kuchapishwa rasmi mwishoni mwa mwezi uliopita na Wizara ya Mipango ya nchi hiyo, inasema haja ya watoto ni kubwa sana nchini humo na kwamba lazima idhibitiwe.
Maeneo kame ya kaskazini mwa nchi hiyo, licha ya kuwa kwake na shida kubwa zaidi ya maisha, yametajwa na ripoti hiyo kuwa yanayoongoza kwa idadi kubwa ya vizazi.
Ingawa ripoti hiyo haisemi moja kwa moja, lakini inaelekea sana kupendekeza sera ya kila mwanamke kuzaa watoto wawili nchini Kenya kuwa jambo la lazima.
Kazi kubwa zaidi yahitajika
Watoto wa Kibera, Nairobi.
Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema kwamba hata kama sera hiyo itaanzishwa, italazimika kutanguliwa na mfumo mzuri sana wa kuisaidia, zikiwemo njia za kuimarisha uzazi salama, afya ya kimama na watoto wanaozaliwa na pia kampeni itakayokwenda hadi vijijini.
Kubwa zaidi ni kuhakikisha kuwa wasichana wengi zaidi kadiri inavyoyumkinika wanapatiwa elimu angalau mpaka ya sekondari, kwani utafiti huo ulionesha kwamba wanawake wenye watoto kidogo zaidi ni wale ambao angalau wamefikia kiwango hicho cha elimu.
Wakosoaji wa pendekezo hili la kuanzishwa kwa sera ya watoto wawili kwa kila mwanamke, wanasema kwamba hakuna uwiano kati ya idadi ndogo ya watu na kufikiwa kwa Dira 2030 inayoielekeza Kenya kuwa taifa lenye uchumi wa kati.
 
Nchi za Afrika karibu zote bado kumudu
zoezi gumu kama hili yaani uweke idadi ?
Nadhani nchi zetu zimeshindwa kuiga
maendeleo yenye tija sasa ni kutapatapa.
 
Hata hivyo kwa ukubwa wa nchi yao nafkiri ni hatua nzuri, sie WaTizedi aridhi ipo tena tele acha tujinafasi, ila mkuu hu uzi wako pia peleka jukwa la magreat thinker kule wale jamaa kule dah! wanakesha library nadhani watakua na usemi juu ya hili
 
Nchi za Afrika karibu zote bado kumudu
zoezi gumu kama hili yaani uweke idadi ?
Nadhani nchi zetu zimeshindwa kuiga
maendeleo yenye tija sasa ni kutapatapa.
Unasababu zipi za kukufanya wewe usiamini kama hili swala linawezekana , mpaka kufikia hatua ya wewe kuliita gumu.
 
Hata hivyo kwa ukubwa wa nchi yao nafkiri ni hatua nzuri, sie WaTizedi aridhi ipo tena tele acha tujinafasi, ila mkuu hu uzi wako pia peleka jukwa la magreat thinker kule wale jamaa kule dah! wanakesha library nadhani watakua na usemi juu ya hili
Kwani hao jamaa wa Great thinker wao wanaishi sayari ipi mpaka wewe ufikie hatua ya kuwaona wao wana uwezo wa kulizungumzia hili kuliko wewe.
Ukiona wenzako wananyorewa wewe tia maji, mpango huu ukifanikiwa kule kenya jua wa tzedi tuta copy na kupaste.
 
Wawaache watu wapumue na idadi ya watoto wanaohitaji.

Mie leo natamani kuwa na vichanga hata 10, God help me!
 
Afadhali hiyo sera ipitishwe na kule Pemba!!!!
Coz kule idadi ya watoto na vipato vya wazee hakuna mahusiano kabisaaaa!
Utakaona katoto kadogooo lakini kana mimba afu kina ndugu wawili na sio mapacha!
Vitoto vinanyonya miezi michache sana!
 
Kwani bara sera hii haifai?
 
Wawaache watu wapumue na idadi ya watoto wanaohitaji.

Mie leo natamani kuwa na vichanga hata 10, God help me!

Hauoni kama utakuwa unachosha viungo vya mwili wako,
Sababu hata tamu hukinai.
==yeroo=
 
Back
Top Bottom