Kenya:Wanaume wagoma kula majumbani mwao!!!!

Pindima

JF-Expert Member
Aug 16, 2011
347
81
Waume nchini Kenya wanapanga
kugomea vyakula vya mabibi zao
kwa siku sita kutoka na
kuongezeka kwa visa vya
wanawake kuwapiga mabwana
zao.
Badala yake wanaume watakuwa
wakila mahotelini na magengeni
Mwenyekiti wa Chama cha
maendeleo ya Kina baba Nderitu
Njoka amesema mgomo huo wa
siku sita una lengo la
kuwashinikiza wanawake kukoma
kuwanyanyasa na kuwapiga
waume zao.
Kiongozi huyo Nderitu Njoka
amesema kuanzia leo jumatatu
ataanza kampeni ya
kuwashawishi akinababa kula
mahotelini badala ya majumbani
mwao.
Mwenyekiti huyo wa maendeleo
ya wauaume alikuwa
akizungumza katika hospitali kuu
ya mjini Nakuru huko Rift valley
ambako alikuwa amekwenda
kumliwaza baba mmoja ambaye
amelezwa humo kutokana na
kipigo alichopewa na mkewe.
Baba huyo akizungumza kwa
uchungu hospitalini alisema
mkewe alimuita nyumbani it
akachukuwe pesa kabla ya
kumfungia chumbani na
kumtandika.
Kwa muujibu wa bwana Nderitu
Njoka, mkoa wa kati nchini
Kenya ndio unaongoza kwa idadi
ya akina baba wanaopigwa na
bibi zao.
Katika mkoa huo wa kati
wanaume karibu nusu milioni
wameripoti kutandikwa.
Chama hicho cha wanaume
kimedai kuwa kuna wanaume
ambao wanalazimishwa kufuo
nguo za wake zao.
Wengine pia wamedai kunyimwa
tendo la ngono na mabibi zao.
Jijini Nairobi wanaume ambao
huona kivumbi kutoka kwa wake
zao ni laki tatu.
Lakini baadhi ya akina mama
kutoka mkoa huo wanasema
akina baba ndio wa kulaumiwa
kwa kushindwa na majukumu yao
ya kifamila.
Wanasema waume wangi
wamekuwa waume suruali tu.
Hata hivyo wengi wanasubiri
kuona kama kweli mgomo huo
utafaulu, na ni wanaume
wangapi walio na pesa za kwenda
kula hotelini badala ya kula
majumbani mwao.
 
hata mie nimeisikia hiyo live BBC!!................ mwanzoni sikuamini, ...................nikafikiri ni comedy.................. jamani, hivi hao wanaume wa kenya ni wanaume sawaswa kweli??............... i doubt!!...................hapo ndipo tunapowahitaji wakurya katika dunia hii!!.........................
 
How does it feel to be on the receiving end kaka zangu?
Mnadhani unyanyasaji ni kitu kidogo? Waelezeni wenzenu ili waache na dunia iwe mahali salama.
BTW - Kwanini hao wanaume hawaachani na wake zao wanyanyasaji?Nini siri ya kung'ang'ana tu kukaa na mke mnyanyasaji?
Wenzenu wanawake hawaondoki kwa vile wamezaa watoto hapo na wanaogopa kuacha watoto zao.Nyie mnasubiria nini wakati hamnyonyeshi?
 
Vituko vya wakenye me siviwezi, midume ina chama cha kutetea maslahi yao!!!!!
 
Dah!! Hii kali, lakini bora hao wameweka wazi kuwa wanapigwa. Huku huenda wapo ambao wanapigwa lakini wapo kimya..
 
  • Thanks
Reactions: FJM
ila hiyo njia ni sahihi?
Maana kuna hatari ya kuchezea kichapo kwa kutokula nyumbani....
 
Wakimaliza mgomo watachezea tena kichapo cha kutokula nyumbani na uloda hawatopewa :lol: kuishi kwingi ni kuona mengi
 
How does it feel to be on the receiving end kaka zangu?
Mnadhani unyanyasaji ni kitu kidogo? Waelezeni wenzenu ili waache na dunia iwe mahali salama.
BTW - Kwanini hao wanaume hawaachani na wake zao wanyanyasaji?Nini siri ya kung'ang'ana tu kukaa na mke mnyanyasaji?
Wenzenu wanawake hawaondoki kwa vile wamezaa watoto hapo na wanaogopa kuacha watoto zao.Nyie mnasubiria nini wakati hamnyonyeshi?
mkuu unawaambije nimekutaliki?mwenyewe na mashaka na huo mgomo wao
 
Back
Top Bottom