Kenya wamepiga marufuku makampuni ya simu kuruhusu usambazaji wa sms za uchochezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenya wamepiga marufuku makampuni ya simu kuruhusu usambazaji wa sms za uchochezi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIBE, Oct 24, 2012.

 1. K

  KIBE JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo kwetu tanzania sms za uchochezi sasa zimekuwa kama jambo la kawaida ..na hakuna hatu zozote zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaosambaza sms za uchochezi zinazohatarisha amani na kuongeza chuki miongoni mwa watanzania. Kuchukuliwa hatua pia makampuni ya cm kuruhusu usambazaji wa sms hizo ... Wenzetu kenya tayari wamechukua hatua ..sisi je.
   
 2. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  Madhara ya serikali legelege
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  wako siriaz

  Sasa hapa watapigaje wakati CCM ndio vinara wa sms za kashfa na uchochezi???

  Yu wapi yule Shamte??
   
 4. p

  promi demana JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa kwetu tunataka wafungie Radio Imaan na gazeti Al-nuur ambalo siku hizi linawaitwa wakristo ni MBWEHA,

  hapo ndo tuhamie kwenye sms.
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Tanzania haiwezi kupiga marufuku makampuni haya kwa vile serikali ya sasa inanufaika na jinai hii. Hata viwango vya kupiga na kupokea simu tunavyotozwa Tanzania ni ujambazi mtupu. Hii yote inasababishwa na baadhi ya watawala wetu mafisi na mafisadi kuwa na hisa katika makampuni haya. Leo kampuni linaloendeshwa na mtoto wa Makamba kwa mfano haliwezi kugushwa. Huwezi kujua waliopo nyuma ya pazia. Angalia mawasiliano yetu yalivyo ya hovyo. Ajabu akina Chenge na wezi wenzake walituibia kwa kununua mikangafu ya rada na upuuzi mwingine na bado tunawavumilia. Hapa inapaswa kujilaumu kama wananchi ambao tunakubali kugeuzwa mbuzi wa kafala na kila **** na jambazi.
   
 6. Dumelang

  Dumelang JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 2,190
  Likes Received: 1,543
  Trophy Points: 280
  Meseji za fitina na uchochezo ziliiweka CCM madarakani.
  nani atazipinga Tanzania

  Kenya walishang'atwa na nyoka wanajua uchungu.

  Serikali legelege, Raisi Dhaifu kiuongozi na hata kiafya
  Taasisi zimekufa...Nchi si tofauti na shimo la panya kwasasa.

  Tunaongozwa na nyang'au wengi kuliko kondoo, nani atasema LABDA meseji hizo ziandikwe na MwanaHalisi zitakuwa jinai...
   
Loading...