KENYA: Mamlaka ya mawasiliano yapiga marufuku matangazo ya moja kwa moja kwa mikutano ya Kisiasa

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,038
3,931
Mamlaka ya mawasiliano ya Kenya, imetangaza kupigwa marufuku kwa upeperushaji wa matangazo ya moja kwa moja wa mikutano ya kisiasa, katika kile ilichokiita “kusaidiA kupunguza hali ya taharuki nchini.”

SIiku ya Jumapili polisi nchini humo walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliokuwa wanaandamana mjini Nairobi kupinga mauaji ya watu wanne yaliyotekelezwa jaJumamosi usiku katika mtaa mmoja wa mabanda mjini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baadhi ya mitaa ya mji huo imekumbwa na hali ya taharuki tangu Ijumaa, wakati takriban watu watano waliuawa kufuatia makanbiliano kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, ambaye alikuwa amerejea kutoka ziarani Marekani.

Polisi hata hivyo wamesema waliouawa ni wahalifu.

Haya yamejiri siku moja tu kabla ya mahakama ya juu ya Kenya kutoa uamuzi wake kufuatia kesi zilizowasilishwa kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 26 mwezi jana.

Jaji mkuu David Maraga ametangaza kwamba uamuzi huo utatolewa saa tano asubuhui siku ya Jumatatu.

CHANZO: VOA-Swahili
 
waache ujinga ujinga wafanye kazi. nchi ina madeni makubwa, ukosefu wa ajira wa hali ya juu, baa la njaa, nk. badala ya kufanya kazi ili kupambana na maadhila hayo, wenyewe wanataka kutwa nzima wawe wanaongelea siasa. muda wa siasa za uchaguzi umekwisha. sasa hapa kazi tu.
Uhuru piga marufuku kabisa hao.
 
Kweli bora awe kama huyu wa Kwetu maana Raila amezidi. Huyu wa kwetu amejifunza kwa Museveni,Nkurunzinza na Kagame na sasa nae akampe Somo Uhuru ili amkomeshe Swaiba wake Raila. Patamu hapo.
 
Utakuwa ni ujinga kuruhusu mambo yanayohatarisha usalama wa nchi kwa kigezo cha Demokrasia.

Wananchi hawawezi kuacha kulalamika lakini Rais amekula kiapo kulinda usalama wa watu na hapaswi kuwa mwoga kutekeleza hilo.
 
Watz mmechanganyikiwa mara sijui Kenya katiba yake ni mbovu mara sijui hakuna demokrasia Kenya. Tuambieni basi hiyo katiba yenu bora mlioandikiwa na mjerumani 1895 inawasidia vipi kwenye kukuza demokrasia ya nchi yenu? Mimi naona mpo mpo tu kama ndugu zenu wa Madagascar.
 
Back
Top Bottom