Kenya kama kwetu, Maandamano halali na haramu sambamba leo

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,854
35,862
Raila Odinga (baba) atakuwapo barabarani leo 0600 kwenye maandamano yaliyoitwa haramu na serikali huko. Kwamba:

1. Wana ujumbe wao kupeleka ikulu
2. Wana ujumbe wao kupeleka hazina
3. Wana ujumbe wao kupeleka tume ya uchaguzi.

Hizo ni ofisi za umma na katiba inawaruhusu kufanya hivyo kwa amani.

"Kwamba gharama za maisha zishuke, shakahola watu walikufa, mishahara jana haikupanda, servers (vyungu) havijafungiliwa nk, ni uvunjifu wa katiba ya Kenya kuyaharamisha maandamano yao."

#Maandamano: Protests will begin at 6am, defiant Raila tells Ruto

Haramu huu wategemee sekeseke na polisi kama kwetu tu awamu ile.

Upande wa pili ni ule wa watawala, yaani Kenya Kwanza. Huu utafanyikia nyumbani kwa rais mataafu wa huko, bwana Uhuru Kenyatta. Kenya Kwanza inamtambua huyu, kuwa ndiyo kinara wa maandamano ya Odinga.
Madai makubwa ya Kenya Kwanza ni Uhuru kutambua kuwa walioko madarakani sasa hivi ni wao, na si yeye. Hivyo awape muda japo wa kupumua basi? Hawa songombingo za polisi kama CCM vile halitawahusu.

CS Kuria: We will hold our own protest outside Uhuru's home

"kumbe wenye kuona ukabila kwenye maandamano ya huko ni sisi tu wa kule Mburahati."
 
Rutto anaingia cha kike soon

Kwamba:

1. Uchaguzi ulikwisha?
2. Wananchi wanataka maendeleleo?
3. Siasa ni mpaka uchaguzi mwingine?
4. Kufanya siasa kafanye kwenye jimbo lako?
5. Mkitaka kuandamana nyie na wake zenu muwe mbere?
6. Nk, nk?

Hayo ni ya kuwaambia ndege wa Nanjilinji huko, watakuelewa.
 
Ruto atayameza maneno yake leo, washauri wake wamemdanganya kakaa pabaya sana kisiasa,

Kashindwa kujifunza:

1. Kenyatta Mzee, Raila kakaa sana jela na bado akatoka.
2. Moi hakumgusa Raila.
3. Kibaki kashikana naye mkono.
4. Uhuru kashikana naye mkono.

Sasa Ruto na zile mbuzi za kwetu. Kazi kweli kweli.
 
Lipi sasa? Maana serikali ya CCM ya huko inasema mwenye lake jambo ni Uhuru. Mburahati wazima huko?
Huku Mbezi Beach hali ni shwari sijui huko kwenu Tandale. Jinga ni limoja tu, lizee la kitendawili linalozungumza kama lina umwa dege dege
 
Huku Mbezi Beach hali ni shwari sijui huko kwenu Tandale. Jinga ni limoja tu, lizee la kitendawili linalozungumza kama lina umwa dege dege
Si Kenya, si Ruto, Gachagua au genge lao wenye kuafikiana na mawazo yako. Kwamba pamoja na hivyo bado hujishangai? Bila shaka utakuwa ni mmoja wa ile mivijana ya hovyo akiiongelea jiwe masikitiko makubwa!
 
Back
Top Bottom