Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Mwaka juzi wa 2019 Mwezi November, JF Member My Son drink water aliwahi kusema kwamba "Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania, nashukuru Mungu tena dakika za mwisho TISS walistukia mchezo vinginevyo VodaCom nayo ilikuwa inakufa na ingekuja kufufukia Kenya"
==========
dfrgtr.jpg
==========
Habari zenu waungwana wa jamiiforums

SEPTEMBER 28, 2018: Vodacom Tanzania said on Friday the government had denied its incoming chief executive officer, a Kenyan, a work permit, and it would have to restart the recruitment process.

In April, Vodacom Tanzania named Sylvia Mulinge, at the time head of business at Kenya's biggest telecoms operator Safaricom to the post. She was meant to take up her position on June 1.
==========
asdedcvfgtrf.jpg
==========

HOJA YANGU: Kwani kama mtu alikuchangia USD 300 katika maandalizi ya harusi yako ni lazima na wewe umpe kiasi hicho hicho cha pesa yeye atakapokuwa anajiandaa kuoa/kuolewa?

Kwani kitendo cha Rais Uhuru Kenyatta kufuta work permits pamoja na Business Visas ni lazima kiwe nipe nikupe (quid pro quo) kwa taifa kubwa la Tanzania? Kuna ulazima wowote wa Tanzania nayo kufuta vibali hivyo kwa raia wa Kenya?
==========
derfdfvghtrfd.jpg
==========
Baada ya Rais Kenyatta kufuta documents kwa wafanyakazi wa Tanzania ndio ninakumbuka maneno yaliyopo humu humu JF ya member mmoja anayetumia jina la My Son drink water kwamba;

"65% ya viwanda vilivyokufa Tanzania vilikuja kufufukia Kenya, tafsiri yake ni kwamba, Usalama wa Taifa wa Kenya, KNIA walifanya yao huku TISS yetu ikiwa imelala, na Kiwanda cha mwisho kuhamia Kenya ni cha General Tyres, yaani ajira zinakufa Tanzania kisha zinawafufukia Wakenya. Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania, nashukuru Mungu tena dakika za mwisho TISS walistukia mchezo vinginevyo VodaCom nayo ilikuwa inakufa na ingekuja kufufukia Kenya"
==========
gfhtgbnhfdssw.jpg

==========
SWALI: Tutegemee "Sylvia Mulinge" wa Safaricom kurudi kuwa CEO wa Vodacom endapo Tanzania itafuta work permits pamoja na Business Visas kwa raia wa Kenya?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
..nadhani tunakosea sana kuwakweza TISS na kukabidhi maisha yetu mikononi mwao.

..suala la viwanda kufa au kustawi linategemeana na mazingira ya kibiashara yaliyoko Tz.
Swadakta kabisa mkuu, kinachoigharimu Tz yetu ni mifumo ya hovyo na ujanja² wa kiswahili. Mtoa mada + MATAGA wanahangaika sana kulinda legacy ya Jiwe, hawataki kusema ukweli kwamba uchumi wa Tz kudorora ni matokeo ya;
  • Sheria kandamizi
  • siasa chafu
  • ulimbukeni wa viongozi
  • visasi
  • wivu wa kitoto kwa wenzetu n.k n.k
Hamna cha ujasusi wala nini.
 
..wenzetu wamewekeza kwenye UBUNIFU, sisi tumeng'ang'ania siasa na uzalendo uchwara.

..kwa mfano vijana wanahamasishwa wasijifunze KIINGEREZA na wenyewe wanaamini hivyo, halafu wakikosa kuajiriwa, na kupigwa bao na Wakenya, ktk sekta ya UTALII wanashangaa na kulalamika.
 
Kwani baada ya kumkataa Sylivia Mulinge kuna mtanzania anayeendesha VodaCom kama CEO au shida ni Mkenya ??

Ziara ya Rais Samia ni kubwa na imechukuliwa kwa ukubwa sana na wakenya ila kwetu sisi,

Muda wote ni wanyonge kazi yetu ni kujishuku shuku muda wote, kujiona wanyonge tutapigwa, hatujiwezi. Aisee

Huu ni ulemavu hakika.

Ningekuwa Rais nchi hii, ningegawa passport kwa kila mtu akazurule huko nje labda unyoronyoro ungetoka.

Mbongo muda wote ni kulalamika na kuhisihisi kujiona anaonewa muda wote.

This is too much.
 
Asee ni vile mko mbali na systeam...hivo amuwez jua lolote...

Hakuna watu wanaopambana usiku na mchana kama Tz Intell!genc!!!!!(Tiss"""Mi"")
Hawa hawa walioshindwa kudhibiti siri nzito za serikali kuvuja kwa Kigogo kwa miaka mitano mizima au wengine? Ulishaona wapi taasisi makini ya intelijensia inakuwa na mole miaka na miaka bila kumgundua?

Hopulesi !!!
 
Kwenye work permit mama asijaribu,huku tayari wakenya wengi sana kwenye mahoteri ya kitalii kuliko watz na sisi hawawezi kutupa ajira huko.
Ni lugha za kisiasa tu.
1-umesoma?
2-umeomba kazi ukanyimwa?
3-una connection hata ya jamaa zako KE?
4-una hela ya ziada ya kujisaidia ukiwa ugenini?
5-unaweza kujituma bila kulalamika?
6-mwisho, what's your future plans wakati unataka kufanya kazi inje?

NB:Ukijijibu hayo, bila shaka hutaona wa kukubwaga maishani kwa lolote utakalotaka kufanya, pahali popote pale duniani!
 
..nadhani tunakosea sana kuwakweza TISS na kukabidhi maisha yetu mikononi mwao.

..suala la viwanda kufa au kustawi linategemeana na mazingira ya kibiashara yaliyoko Tz.
Suala la viwanda kufa Tanzania ni kutokana na mtazamo wa uchumi wa kidola tulionao pamoja na siasa.

Kuna mashirika mazuri nchi hii, lakini wakurugenzi badala ya kuwekwa wenye weledi mtu anakabidhiwa shirika kwasababu alimsaidia fulani kwenye kampeni za uchaguzi.

Au yuko karibu na mwenye madaraka au kutoka chama fulani.

Tafsiri yake mtu anapewa shirika ili atafune wakati wake, shirika likifa utamlaumu nani
 
Swadakta kabisa mkuu, kinachoigharimu Tz yetu ni mifumo ya hovyo na ujanja² wa kiswahili. Mtoa mada + MATAGA wanahangaika sana kulinda legacy ya Jiwe, hawataki kusema ukweli kwamba uchumi wa Tz kudorora ni matokeo ya;
  • Sheria kandamizi
  • siasa chafu
  • ulimbukeni wa viongozi
  • visasi
  • wivu wa kitoto kwa wenzetu n.k n.k
Hamna cha ujasusi wala nini.
Absolutely
 
1-umesoma?
2-umeomba kazi ukanyimwa?
3-una connection hata ya jamaa zako KE?
4-una hela ya ziada ya kujisaidia ukiwa ugenini?
5-unaweza kujituma bila kulalamika?
6-mwisho, what's your future plans wakati unataka kufanya kazi inje?

NB:Ukijijibu hayo, bila shaka hutaona wa kukubwaga maishani kwa lolote utakalotaka kufanya, pahali popote pale duniani!
Kijana 254 nakuona unatetea nchi yako
 
Back
Top Bottom