Kenya declares war on Al Shabaab!

Hakuna kitu hapo, Kenya wanachotafuta ni umaarufu na kujaribu kuonyesha wanajeshi makini. Wa America wanatoa fedha nyingi sana kuzishawishi baadhio ya nchi za Afrika ya Mashariki ikiwemo Kenya, Ruwanda na Uganda kuisaidia katika kupambana na Ugaidi baridi ambao unafanyika ndani ya nchi hizi na hasa baada ya matukio ya kulipuliwa kwa Balozi zao Tanzania na Kenya mwaka 1998.

Marekani wapo makini katika kutuchonganisha waafrika tutwangane wenyewe kwa wenyewe. Hii hainiingii akilini kwa nchi hiuru kama Kenya kutangaza vita na wanamgambo wa al Shabaab ambao kismsingi ni kundi la kigaidi ambalo halipingani ncghini Kenya. Hapo Kenya wanafikiria kuivamia Somalia ambapo hao wanamgambo wapo??? Au hiyo vita itapiganiwa wapi?? Tulidhani wanahimarisha usalama wa mipaka yao na sio kutangaza vita na magaidi ambao wanaingia na kutoka nchini mwao!! (hiyo vita itapiganiwa wapi??)
 
ngoja tusubiri tuone...kupigana vita si lelemama hasa unapopigana na adui ambaye yuko so elusive
 
mauaji mengine haya.....
Alshababu si wa kutangazia vita, kwani wao ni silent soldiers. Kwani wana magwanda kama wakenya?
Kwa nini kenya wasingefanya silent movement/operation kuwamalia alshababu?
 
Mi nawakubali wamarekani kwa sababu moja, huwa wana-take advantage of the situation.

Nani asiyejua njaa ya Somalia inasababishwa na Al-shabab ? Nani asiyejua kuwa maharamia wa kisomali wameweka ukanda mzima wa A. Mashariki katika hali ya hatari kiusalama na kiuchumi?

Matukio ya kuuawa na kutekwa kwa watalii huko kenya ni jambo linalo haribu sekta ya utalii ya Kenya hivyo kama ikibidi kuwahakikishia usalama watalii, basi inabidi wafanye hivyo, hapo ndipo hata US wanaweza wakatake advantage ya Regional forces involvement, wenyewe watatoa support tu ya kitaalamu na fedha.
 
leo kwa Kenya, kesho kwetu. Sie tulijitolea kuwafundisha askari wa Somalia na hilo limewaudhi al shabaab. Hivyo, nadhani tujiandae
 
mauaji mengine haya. familia za askari wanaingia katika majonzi makubwa.

AL SHABAB hawana jeshi, hivyo hawana sare zinazowatambulisha. Wanaweza kuingia mahali popote pale kama watu hawakuwa makini.

kwa mawazo yangu, KENYA hakusitahili kutangaza vita, bali wangetangaza oparation na wasingevaa mgwanda kama hayo. huwezi kuvaa magwanda, ukapigana na mtu ambaye hana magwanda, atakumaliza.
 
Tanzania kaa chonjo mwenzio ameshanyolewa?

Halafu Ikulu yetu ipo karibu tu na njia yao wanayoipenda. Nilishaandika humu wakati fulani Wasomali wanaingia zaidi ya 1000 kila siku Tanzania. Ukitoka Himo kuanzia saa 2 usiku utaona mafuso yanavyowabeba na kuwashusha Msata, Chalinze na hata Vigwaza. Nimeshihudia haya.

TAHADARI SERIKALI CHUKUA HATUA.
 
matokeo ya census iliyoendeshwa mwaka 2009 yalizua utata mkubwa kenya kutokana na idadi kubwa ya wasomali
 
mukulu uliye hapo magogoni una taarifa ya hayo mafuso yanayomwaga wanamgambo kwenye nchi yetu tukufu?
 
Kenyan troops off to war

Kenya-armyTankers.jpg




transport_clip_image004.jpg


The Kenya military has been ordered into action to stop al Shabaab militia from further threatening the country's security and economy.

At a press briefing on Saturday, the country's top security chiefs declared war on the terrorist organisation operating from Somalia and said Kenyan security forces will henceforth pursue the aggressors across the border.

Yaani Kenya wanaenda kupigana na Al shabaab na vifaa kama hivi vya kivita? Wanacheza ngoma wasiyoijua! Tom and Jerry catoon.Hii ni Tathmini nzuri
mauaji mengine haya. familia za askari wanaingia katika majonzi makubwa.

AL SHABAB hawana jeshi, hivyo hawana sare zinazowatambulisha. Wanaweza kuingia mahali popote pale kama watu hawakuwa makini.
kwa mawazo yangu, KENYA hakusitahili kutangaza vita, bali wangetangaza oparation na wasingevaa mgwanda kama hayo. huwezi kuvaa magwanda, ukapigana na mtu ambaye hana magwanda, atakumaliza.

Hata US na NATO wanalijua hilo kutokana na vita yao huko Afghanistan dhidi ya Al qaeda na Taliban ambao ni marafiki zao.​
 
Nawafagilia Kenya kuwateketeza hawa Al Shabab, piga risasi kila mmoja wao na waishe na ikiwezekana Kenya waikalie Somalia iwe part of Kenya permanently.

kweli, inafaa kenya waikalie somalia iwe yao na wawashikishe adabu hao al-shabab. ivi AU na UN wameshindwa kujua mfazili wa al-shabab?
 
I have misgivings about fighting an invisible enemy using conventional forces. Just wondering if an undercover seek and destroy mission would have been more effective rooting out the Al Shaabab menace.
 
Back
Top Bottom