KENYA; Amuua mamake Mzazi kisa kaishi muda mrefu

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
27,576
29,988
MAHAKAMA ya Nanyuki Jumanne ilishuhudia kisa cha mwanamume kushtakiwa kumuua mamake mzazi akiwa na umri wa miaka 89 ambapo mshtakiwa alidai kuwa aliafikia ukatili huo kwa msingi kuwa mamake huyo alikuwa ameishi "kupita kiasi".

Satar ole Sanangi, 40 ambaye ni baba wa watoto wanne alifikishwa mbele ya hakimu Jesse Nyagah akidaiwa kumuua mamake, Kuyano Lesanangi mnamo
Julai 14.

Kiongozi wa mashtaka, Osman Mohammed alielezea mahakama vile mshtakiwa alifika nyumbani akiwa mlevi chakari na kisa akamvamia mamake mzazi akiwa katika boma lake.

“Mshtakiwa alifululiza hadi ndani ya nyumba ya mamake na akaanza kumzomea kuwa alikuwa hafai kuwa hai,” akasema kiongozi huyo wa mashtaka.

Ilibidi hakimu kwa wakati mmoja kuonya waliokuwa kortini dhidi ya kupiga usiahi dhidi ya mshtakiwa kwa sauti ya juu.

Aliongeza kuwa mshtakiwa alianza kuorodhesha majina ya waliokuwa rika la mamake lakini walikuwa tayari wameenda zao kuzimu.

“Mshtakiwa alimwelezea mamake kuwa hata yeye alikuwa anafaa kuondoka ulimwenguni ili aende waliokuwa wakongwe wa rika lake,” Mohammed
akaongeza.

Ndipo, korti ikafahamishwa, mshtakiwa alichukua fimbo na kumtandika mamake ili kumuua.

Mahakama ilifahamishwa kuwa kisa hicho kilitendeka katika kijiji cha Olesirikon Wilayani Laikipia Magharibi, hali ambayo ilimwacha mwathiriwa katika hali mbaya.

“Mwathiriwa alipelekwa hospitalini ambapo alitangazwa kuwa marehemu kutokana na majeraha aliyokuwa amepata katika kipigo hicho kutoka kwa mwanawe,”
akasema kiongozi wa mashtaka.

Baada ya kukataa mashtaka ya mauaji na kuwa mlevi na kusabaratisha amani ya umma, Hakimu Nyagah alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh200,000 na mdhamini wa kiasi kama hicho.

Kesi yake itaanza kusikizwa rasmi Agosti 2, 2017.
 
Back
Top Bottom