Kenya: Kibaka ahukumiwa miaka 210 jela

baharia 1

JF-Expert Member
Sep 13, 2019
1,255
1,268
Kibaka wa mtaani jela miaka 210,

ila walamba asali wanatamba *****
===

Kenya. Mwanamume mwenye umri wa miaka 55 aliyeshtakiwa kwa makosa manne ya wizi wa kimabavu na shtaka jingine la ubakaji nchini Kenya, Humphrey Shilisia amehukumiwa kifungo cha miaka 210 jela.

Mahakama ya Eldoret imemuhukumu mwanaume huyo kwenda jela miaka 210 baada ya kupatikana hatika katika makossa matano. Hakimu Mkuu wa Eldoret, Naomi Wairimu amesema upande wa mashtaka umethibitisha kesi yake bila shaka yoyote.

Shilisia alifikishwa mahakamani kwa wizi wa kimabavu pamoja na mkewe Amina Melesi na mtuhumiwa wa tatu, David Gazemba.

Hakimu Wairimu aliwaachia Melesi na Gazemba kwa msingi kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani kutokana na mashtaka yaliyokuwa yanawakabili.

Katika kila mojawapo ya makosa manne ya uhalifu huo, Wairimu alimhukumu Shilisia miaka 50 jela.

Mshtakiwa huyo pia alipatikana na hatia ya ubakaji na alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa hilo, huku hukumu zote mbili zikitakiwa kwenda sambamba.

Kulingana na maelezo ya mwendesha mashtaka, Shilisia alishtakiwa kwa kuiba Sh6,000 za Kenya (sawa na Sh107,169 za Kitanzania) kwa akiwa amejihami kwa silaha butu katika eneo la Wales Estate, Kapseret Juni 20, 2020.

Shilisia alikabiliwa na shtaka la pili ambapo alishtakiwa kwa kumwibia Yulita Mitei, KSh 19,300 (sawa na Sh 344,727 za Tanzania). Walikabiliwa na shtaka la tatu na la nne la kuwaibia Moses Rotich na Gilbert Murei KSh 76,800 (sawa na Sh137,1764 za Kitanzania) ( na KSh 4,800 (sawa na Sh8,5735 za Kitanzania).

Shahidi muhimu katika shtaka la kwanza, alieleza siku ambayo mshtakiwa alivamia nyumba yao akiwa amebeba tochi ya kuwamulika machoni kisha kumnyang'anya simu na kujitumia KSh 6,000 (107,169) kwenye simu yake.

“Kisha alihamisha fedha kutoka kwenye simu ya mume wangu na kumwamuru aingie chini ya kitanda na kuniburuta nje ya nyumba akiwa ameniwekea panga shingoni ambapo alinibaka,” shahidi huyo aliieleza mahakama.

Taarifa za kitabibu zilizowasilishwa mahakamani hapo zilionyesha kuwa Shilisia alimwingilia kinguvu mwathiriwa.

Shilisia katika utetezi wake aliwashutumu maofisa wa polisi akisema wamembambikia makosa akidai walimkamata wakati alipokuwa anakwenda kazini.

Screenshot_20230618-231205.jpg
 
Si bora uyo kuna mmoja marekan alihukumiwa kifungo cha maisha halafu akapgwa tena miaka 200+ sasa mtu kama uyo s balaa
 
Si bora uyo kuna mmoja marekan alihukumiwa kifungo cha maisha halafu akapgwa tena miaka 200+ sasa mtu kama uyo s balaa
sema sheria ina complications nyingi na kwa nchi kama USA kila State in sheria zake tofauti tofauti japo kuna Federal Law. Ningeeleza kwa kina ila ni somo pana la muda mrefu. nikipata muda nitaandika siku nyingine tafsiri ya hiyo uliyoandika na nyingine.

NB: Mimi sio mwanaseria, bali napenda tu kufuatilia na kujua mambo.
 
Usisahau kama sku ukiandika hyo mada untagg nkajiuliza inakuaje mtu afungwe maisha halafu apew na miaka mingne zaidi
 
Usisahau kama sku ukiandika hyo mada untagg nkajiuliza inakuaje mtu afungwe maisha halafu apew na miaka mingne zaidi
Hiyo ndio sheria mkuu, msingi ni kujua unapokutwa na makosa zaidi ya moja, kila kosa lina HUKUMU yake. Kwa case ya huyo jamaa, kesi ya kwanza hukumu yake ndio hivyo JERA MAISHA na hukumu ya kesi ya pili hukumu yake JERA MIAKA 200. Na mara nyingi hukumu hizi huenda sambamba. Pia inaweza ikatokea baada ya muda fulani akapata msamaha wa hukumu mojawapo na akaendelea kuitumikia hukumu nyingine jera.
 
Aaaah maana yke alikua na makosa zaid ya moja ko kila moja na hukumu yake
 
Back
Top Bottom