Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ally Keissy
Keissy amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge.
"Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale" - alisema Keissy.
Aidha, Mbunge huyo aliendelea kwa kusema kuwa "Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika ni dhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye vijiwe sisi wabunge wa bara hatutaki mchezo mchezo namna hii ya kutukana. Spika kwanza anawazidi umri pamoja na cheo" aliongezea Keissy.
Chanzo: EATV