KCMC yakiri kuathirika na mgomo wa madaktari

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
mwenyekiti wa bodi ya usamamizi wa hospitali ya rufaa KCMC Dr alex malasusa amekiri hospitali hiyo kuathiriwa na mgomo wa madaktari.
Huduma kwa wagonjwa hasa wale wa nje imeathirika zaidi na hili limesababishwa na ukosefu wa madaktari interns ambao serikali imewafutia usajili.hizi ndio athari za liwalo na liwe!
KCMC ina madaktari bingwa 45 ambao wamekiri kushindwa mzigo mkubwa wa wagonjwa.
 
Mgogoro uliopo kati ya serikali na watoa huduma za afya nchini umeiweka rehani maisha ya wavuja jasho kila pembe hapa nchini! Hakuna mtawala hata mmoja aliyetoa tamko ya athari zinazoendelea kuitafuna sekta hii muhimu! Wahindi nao wametushika pabaya na hatuna mbadala kwa kuwa wanaotuongoza kumbe na wao wagonjwa!
 
mwenyekiti wa bodi ya usamamizi wa hospitali ya rufaa KCMC Dr alex malasusa amekiri hospitali hiyo kuathiriwa na mgomo wa madaktari.
Huduma kwa wagonjwa hasa wale wa nje imeathirika zaidi na hili limesababishwa na ukosefu wa madaktari interns ambao serikali imewafutia usajili.hizi ndio athari za liwalo na liwe!
KCMC ina madaktari bingwa 45 ambao wamekiri kushindwa mzigo mkubwa wa wagonjwa.

Tusisahau hakuna kiongozi anayetibiwa Tanzania. Wote wanatibiwa India. Huko India madaktari hawajagoma kwani wanalipa mchuzi mnono toka Tanzania. Tunaoteseka na kufa ni sisi walalahoi na walipa kodi. Jamani tuamke usingizini tutetee haki za taifa hili. Ni vyema tu tukailipua hii serikali DHAIFU. Hawa wazee wanaokufa kila kona kwa kukosa matibabu walilitumikia hili taifa kwa uaminifu maisha yao yote. Leo hii hata kidonge cha kutuliza maumivu hawapewi licha hata ya kumwona daktari. Maisha yao na mafao yao yanatunza wahindi huko India. Hivi kweli huyu Kikwete yupo? Ni vipi tunamwacha anatamba mitaani na mikanzu huku akitudhulumu hivi na serikali yake DHAIFU?
 
mgomo haujaisha ila serikali imeuhamisha kutoka kwenye vyombo vya habari na kuupeleka hospitali. Kwa taarifa yako sasa hivi wagonjwa wengi wanakufa kuliko hata kipindi cha mgomo wenyewe....huwezi kuwarudisha madokta kazini bila moyo na ukajidai kuwa umesolve tatizo!!!watafanyaje kazi bila moyo? wataweza kuimprovise? maana hakuna vifaa tiba, siku zote walikuwa wakiimprovise kuwasaidia wagonjwa sasa hata moyo wa kuimprovise raisi amewanyanganya na kuufungia ikulu ya magogoni
 
Back
Top Bottom