Wewe ndo umesoma muhimbili mkuu.. Mimi napaona tu kwa mbali! Vizuri kama unafatilia mastory yangu endelea kula madini chief sio ujaze tu case huko kichwani ndo maana unapaniki vitu vidogoKama ulisoma Muhimbili, itakuwa ulipita Idara ya Mapenzi. Naona sumu yako huko kwenye jukwaa hilo...
Rudia tena nilichosema kuhusu KCMC utaona ni tofauti.
Pale wanapokezana mgonjwa wanafunzi kwa wanafunzi, na wanafunzi zaidi ya 10 wanaweza kumpitia mgonjwa mmoja kabla hajaonwa na daktari kamili. Wanabonyeza wanachokonoa wanatomasa wanahoji jambo moja mara kumi kumi, ukiongea na mmoja ukadhani umemaliza wanakuja wenzake wanauliza yaleyale, wanatonesha kulekule, mara utaona wanaoneshana hiki mara kile kwenye mwilii wa mgonjwa na kujadili mbele ya mgonjwa, mara wabishane wafungue kitabu waanze upya, likitoka kundi hili linakuja lingine mgonjwa anasoteshwa tu! Ndiyo torture ninayozungumzia. Mtu anafika kutibiwa anaishia kuumizwa zaidi.
Ingekuwa ni mwanafunzi mmoja anachukua historia halafu anaijadili na mwalimu wake mbona isingekuwa taabu, ingeonekana ni consultation kama zinazofanyika kwenye taaluma nyingine ambako mteja anakutana na trainee kwenye initial encounter, halafu trainee akishafanya role yake anamjulisha mteja kuwa atadiscuss na trainer wake halafu waendelee na huduma.
Pale KCMC wanafunzi wanapasiana mgonjwa wao kwa wao kama mpira wa chandimu! Hawajali maumivu ya mgonjwa, wanachojali ni kumtumia kama experimental animal, ambayo hata kwenye haki za wanyama tu inakatazwa kabisa!
Wewe ndo umesoma muhimbili mkuu.. Mimi napaona tu kwa mbali! Vizuri kama unafatilia mastory yangu endelea kula madini chief sio ujaze tu case huko kichwani ndo maana unapaniki vitu vidogo
Nilipeleka mgonjwa KCMC tukakutana na wanafunzi wenye umri sawa na wajukuu wake. Alianza mmoja akaongea naye kirefu sana na kumpimapima mara mbilimbili kijana akaandika notes kurasa zaidi ya tano! Mimi nilidhani hizo ni sehemu ya matibabu kumbe ni notes zake za kujisomea! Akaja kijana mwingine makamo yaleyale akarudia yaleyale ya mwenzie naye akajaza notes zake! Baadaye wakaja kikundi cha vijana kama 8 hivi na notebooks, yaani wote makoti meupe kama yangeyange, wanaanza kubishana kuhusu mgonjwa, mmoja akisoma kitu kwenye notes zake wanaanza kupeana upya zamu za kumtomasa tena mzee! Bahati yao mbaya walikuwa wanajadiliana kwa kiingereza kwahiyo niliwaelewa kila kitu kwamba wanabishania mambo ya kwenye kitabu, mara wanataja kuwa profesa fulani hapendi hivi anapenda vile, mgonjwa anadoda tu! Mapokezi tumekaa masaa matatu, na alipokuja daktari halisi ambaye nilimtambua kwa kitambulisho chake aliongea na mgonjwa kwa muda ambao haukuzidi dakika 10, akaandika notes kwenye headed paper ambazo hazikuzidi one page, na hakujadili chochote na wale wanafunzi! Yaliyofuata ambayo nayo ni kero tupu naona niache kwanza nitayasema baadaye. Lakini mtu asinidanganye kwamba kulikuwa na wanafunzi wanaofundishwa chochote pale, wale walimchezea mgonjwa, wakamtonesha, wakamwongezea maumivu, wakaondoka zao na notes zao!Hapo cjui tatizo ni kuchagua upinzani madaktari hapo hasa wa mishipa hakuna kazi za huko anafanya Dr nyangasa wa muhimbili sasa amezidiwa huku mpaka unamwonea huruma huyu umi mwalimu haoni hili tatizo au anafikiri vituo vya afya vilivyojengwa wakati wake ndo anakuja navyo kwenye kampeni ajiandae hii kcmc atakoma tunamsubiri uzuri magufuli anatembea na mawaziri SMS sent
Wanapaita hospitali ya rufaa lakini vifo nje nje! Ukifika pale kwanza kasheshe ni jinsi ya kuingia ndani, mizinguo inaanza getini. Ukipenya geti ukafika ndani unakutana na foleni ya balaa, foleni kila mahali na haitembei! Na kila hatua kuna wanafunzi lukuki, ukidhani sasa ndio unatibiwa unakuta ni mwanafunzi anakupotezea muda weeeee halafu anakupasia kwa mwanafunzi mwingine unapapaswa unachokonolewa weeeee halafu unafaulishwa kwa mwanafunzi mwingine hivyohivyo hadi watosheke, hawajali maumivu yako. Wagonjwa wengi sana wamefia mikononi mwa wanafunzi.
Ukitoboa hapo kwa wanafunzi (hapo utakuwa umeshasota foleni masaa!) kama ni wa kulazwa ni kilio upyaaaa! Tatizo linaanzia kwenye ile machela ya kukupeleka wodini, utaisubiri masaa! Ikipatikana anatafutwa wa kukupeleka, masaa!
Akipatikana anakukokota kama mzigo hadi wodini, hapo utawekwa kwenye korido masaa! Kisha wanaingia kundi lingine la wanafunzi wanakuanza upyaaaa! Usife kwanini?
Watu wakachunguze ile hospitali ni balaa! Mtu anaweza kulazwa asubuhi akaanza kutibiwa usiku au hata kesho yake! Kama mtu umekodi gari ikuwahishe hospitali ya rufaa unajiuliza mara mbili ulikuwa unaharakisha nini? Hii ni jipu kabisa inatakiwa itumbuliwe harakaaaa!
Wewe kwa mtazamo wako hiyo ni halali? Mgonjwa hana haki ya kulindwa usalama wake?Nakushauri siku nyingine uende kwenye vituo vya afya. Huko hautaonana na mwanafunzi. Ukienda hospitali inayofundisha wanafunzi wa udaktari, basi jiandae na yakubali matokeo. Tena wakikuta ugonjwa wako ni wa nadra (rare disease), wafanyakazi wote wa hospitali, isipokuwa wafagiaji, watakuja kwako kujifunza.
Hii si kweli na wala siyo msingi wa mjadala huu. Hospitali hizi zilikuwa za wakristo tangu mwanzo. Tunacholilia hapa ni kwamba KCMC ijirekebishe iondoe uozo na uzembe unaogharimu maisha ya watu.walizipataje wakristo kumiliki hizo hospital kcmc na bugando zamani zilikuwa za serikali . kazi ya nyerere hiyo
I can't imagine wanavyowachokonoa kama mambo yale niliyoyaona wakimtendea babu anayepumua kwa shida vile, kama hayohayo wanayarudia kwa wamama hilo litakuwa baya baya baya baya! Pengine ndivyo wanavyofanya, kwani mkipeleka wake zenu si mnaambiwa mubaki nje? Huko ndani wanafunzi wanapeana zamu za kutomasa na kuchokonoa!i wish niende kcmc niwe mwanafunzi kuchek wakina mama wenye matatizo ya uzazi
On a second note, this is very arrogant, very uncharacteristic of a medical doctor which I doubt if you truly are!Nakushauri siku nyingine uende kwenye vituo vya afya. Huko hautaonana na mwanafunzi. Ukienda hospitali inayofundisha wanafunzi wa udaktari, basi jiandae na yakubali matokeo. Tena wakikuta ugonjwa wako ni wa nadra (rare disease), wafanyakazi wote wa hospitali, isipokuwa wafagiaji, watakuja kwako kujifunza.
You are right. Mikoani hospital ni stress. Kuna siku nimeenda st joseph moshi na mtoto kidogo nilie masaa mawili nipo reception. Sister kaenda huku karudi huku mpaka kuja kupata file ushasota. Kusumbuliwa kote huko nakuta pediatrician yupo likizo nilitamani niwang'ate ng'ateYaani kiufupi ndio maana napenda ishi Dar maana kila kitu kipo.
Hospital ni mimi kuchagua niende wapi
Agakhan
Masana
Rabininsia
Bochi
Msasani
Ccbrt
Muhimbili
Mloganzila
Tmj
Regency
Nyingine nimezisahau
Muhimbili imesomesha madakatari hadi mabingwa wa mabingwa tangu tupate uhuru, mbona haina kasoro hizo?
Huo ni uzembe tu wa KCMC. Yaani unataka kutuambia kuwa ni sawa tu wagonjwa wafie mikononi mwa wanafunzi bila kutibiwa na wataalamu eti kisa nini? Kuna faida gani kuua mtu ili mwingine asome, huo ndio utaratibu?
KCMC imekuwa hospitali mbaya sana, ningeshauri hata ile "C" inayomaanisha "Christian" kwenye jina lake waiondoe waweke kitu kingine hata "Criminal" au "Cruel". Yesu Kristo asingekubali uzembe ule angewafurumusha hata kwa mangumi kama alivyofukuza wacheza kamari hekaluni. Hospitali imekuwa pango la kifo!
Sijafika Mloganzila kwa hiyo sina ushuhuda wa kusema juu yake, lakini Muhimbili ile yenye Kibasila, Sewahaji, Mwaisela na Moi nimefika na nimeona utaratibu wao wa kubalance mafunzo na huduma ni mzuri. Kuna changamoto nyinginezo lakini sio za wanafunzi, tena mara ya mwisho nilipopeleka mama mkwe pale niliona kama wale wanafunzi walimsaidia sana mama yetu.Kwani mloganzila sio Muhimbili?? Mchezo wao Ndio huohuo wa kuwa tumia wanafunzi na Vifo njenje
Sijafika Mloganzila kwa hiyo sina ushuhuda wa kusema juu yake, lakini Muhimbili ile yenye Kibasila, Sewahaji, Mwaisela na Moi nimefika na nimeona utaratibu wao wa kubalance mafunzo na huduma ni mzuri. Kuna changamoto nyinginezo lakini sio za wanafunzi, tena mara ya mwisho nilipopeleka mama mkwe pale niliona kama wale wanafunzi walimsaidia sana mama yetu.
DuhNilipeleka mgonjwa KCMC tukakutana na wanafunzi wenye umri sawa na wajukuu wake. Alianza mmoja akaongea naye kirefu sana na kumpimapima mara mbilimbili kijana akaandika notes kurasa zaidi ya tano! Mimi nilidhani hizo ni sehemu ya matibabu kumbe ni notes zake za kujisomea! Akaja kijana mwingine makamo yaleyale akarudia yaleyale ya mwenzie naye akajaza notes zake! Baadaye wakaja kikundi cha vijana kama 8 hivi na notebooks, yaani wote makoti meupe kama yangeyange, wanaanza kubishana kuhusu mgonjwa, mmoja akisoma kitu kwenye notes zake wanaanza kupeana upya zamu za kumtomasa tena mzee! Bahati yao mbaya walikuwa wanajadiliana kwa kiingereza kwahiyo niliwaelewa kila kitu kwamba wanabishania mambo ya kwenye kitabu, mara wanataja kuwa profesa fulani hapendi hivi anapenda vile, mgonjwa anadoda tu! Mapokezi tumekaa masaa matatu, na alipokuja daktari halisi ambaye nilimtambua kwa kitambulisho chake aliongea na mgonjwa kwa muda ambao haukuzidi dakika 10, akaandika notes kwenye headed paper ambazo hazikuzidi one page, na hakujadili chochote na wale wanafunzi! Yaliyofuata ambayo nayo ni kero tupu naona niache kwanza nitayasema baadaye. Lakini mtu asinidanganye kwamba kulikuwa na wanafunzi wanaofundishwa chochote pale, wale walimchezea mgonjwa, wakamtonesha, wakamwongezea maumivu, wakaondoka zao na notes zao!
On a second note, this is very arrogant, very uncharacteristic of a medical doctor which I doubt if you truly are!
Huko Muhimbili unakosema ulisoma, ulisomea kozi gani? Uwezo wako wa analysis ni duni to embarrassing levels.Ndio ukweli huo. Call it anything... Madaktari wanafunzi wataendelea kujifunza toka kwa wagonjwa...