DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 32,386
- 83,429
Sure Bishoo, ujue tatizo ni kwamba hawa wasomi wengi wanaamini kuajiriwa katika taasisi kubwa kubwa ndio njia pekee ya kufanikiwa. Yani hata awe anaingiza m2.5 huku chaka bado anajiona hajafanikiwa.hili jibu zuri sana
Nimdogo baada yakuchungulia mishahara yawenzio, acha umbeaShida mshahara ni mdogo
Swala la mshahara ni swala la kimkataba (makubaliano)Habarini wanajamii,niende moja kwa moja kwenye changamoto yangu.Nimeajiriwa kwenye taasisi moja hapa jijini dar,sasa katika ajira yangu kitengo nilichopo tulikuwa wawili mimi na huyo niliyemkuta yeye mwenzangu alikuwa kanitangulia kama miaka miwili pale kazini japo tulikuwa level moja ila kiwango cha mshahara alikuwa ananizidi kwa gap kama 800k kabla ya makato.
Baada kama ya mwaka mmoja jamaa aliondoka baada ya kupata kazi nyingine so pale nikabaki mwenyewe na baada kama ya miezi miwili akaletwa mtumishi mwingine,changamoto inakuja yeye analipwa salary kubwa kuliko mimi na ni gap kama la 950k hivi ila mara nyingi kazi mimi Ndio namwelekeza na mara nyingi pia huwa naulizwa. Mimi moyo yea kufanya kazi haupo kabisa naona kazi ngumu Halafu mwenzangu analipwa vizuri.
Hebu wakuu mnisaidie katika hali hiyo nifanye nn?
Umeongea vzr.Usijali mkuu, ukiona uko sehemu hawaithamini value yako wala hata usiwasanue. We anza kutafuta chaka jingine kimyakimya.
Mimi iliwahi nitokea kipindi flani nikifanya kazi sehemu. Offcourse nilibargain mshahara kizembe na sababu kubwa ilikuwa ni njaa kali iliyokuwa ikinikabili kitaa. Baada ya miaka minne kazini ikatokea mdau mmoja karesign kwenye position ambayo ni ya juu kidogo. Nakumbuka kiongozi wangu aliulizwa na director whether wanipromote au waajiri mtu mwingine akasema waajiri mtu kwa sababu mimi bado sitoshi kwenye hiyo nafasi meanwhile mimi ndie niliyekuwa natekeleza majukumu yote yake na ya kumtumia report ambazo alikuwa anaenda kupatia ujiko kwenye management. Huyo mwamba alivyoresign ni mimi pia nilipewa majukumu yake na nilikuwa nafanya kazi kama punda vile.
Basi bwana ikafanyika interview jamaa akamkingia kifua nadhani manzi yake kipindi akiwa chuoni akapata hiyo nafasi. Kiroho safi kafika nkaambiwa nimfundishe kazi. Haloo manzi alikuwa mweupe kupita maelezo kiasi kwamba kiongozi wangu akawa ananipa majukumu yake. Yaani akawa kama bosheni tu ofisini.
Mungu sio Athumani nikapataga chaka moja nafasi kama ya kiongozi wangu tena kwa mshahara wa zaidi ya mara 3 ya mshahara wa kiongozi wangu. Nikaandika barua ya kuresign mwezi mmoja kabla. Saa ngapi nisiitwe na director ati kiongozi kamwambia aniite tuje tudiscuss kuboreshewa maslahi yangu ili nisiende kwenye ajira mpya. Asee niliwagomea katakata, yaani sikutaka kusikia la mtu.
Ni miaka mitatu imepita sasa, yule manzi alishatimuliwa kwa kuunderperform na kiongozi wangu kashaletewa bosi wake maana utendaji ulilegalega kwenye nafasi yake.
Kupitia kisa changu nakushauri usikate tamaa na ongeza juhudi kwenye kazi yako, ila usiache kutafuta chaka jipya. Na ukilipata usiende kinyonge kabisa kwenye kubargain maslahi. Mungu ni mwema utatoboa maana uwezo huwa hauongopi. Kila lakheri mkuu.
Angalizo:
Usijihusishe na kitendo chochote cha fitna kutokana na uchungu ulionao hivyo hufanya wivu usio na faida.
Mkuu hautafika mbali katika career yako kwanza hizo 950k ni hela ndogo Sana sema upo mind broken lakini ukitaka kuwa na Mafanikio kuwa postive endelea kumuomba Mungu huyo Jamaa yako aongezewe mshahara mara dufu na muombee Amani Sana .
Na wewe ukifika wakati wako utaishi vizuri Sana .na utaogelea hela
Unapangwa ili uache kazi kwa hasira. Inaonekana kukufukuza wanaona aibu au hakuna sababu yenye mashiko kukufukuza. Kwani mshahara wako ulipo-bargain ulikuwa na mfanyakazi mwenzako au mwenyewe?Mimi sina roho mbaya ila kazi na mshahara wa chini yangu gap ni kubwa
Akaombe ushauri kwa Djuma Shabaani na Yanick Litombo Bangala watamwambia kama kiberiti huwa kinatingishwa?Mtoa Mada nimekuelewa.
Pole sana, achana na hawa wanafki.
Cha kufanya kama ni Kazi ya Mkataba kuwa mvumilivu na ujitahidi sana kupiga kazi kwa nguvu zote.
Ikifika wakat wa kufanya Renewal of Contract ndio uweke mapendekezo ya kuongezewa mshahara tena kwa maandishi na kuelezea umefanya ACHIEVEMENT zipi hasa.
Hiyo ndio professional way.
Wanafki wengi humu.
Omba kuongezewa mshahara wakikukatalia tafuta kazi kwa Siri maeneo mengine ukipata.Habarini wanajamii,niende moja kwa moja kwenye changamoto yangu.Nimeajiriwa kwenye taasisi moja hapa jijini dar,sasa katika ajira yangu kitengo nilichopo tulikuwa wawili mimi na huyo niliyemkuta yeye mwenzangu alikuwa kanitangulia kama miaka miwili pale kazini japo tulikuwa level moja ila kiwango cha mshahara alikuwa ananizidi kwa gap kama 800k kabla ya makato.
Baada kama ya mwaka mmoja jamaa aliondoka baada ya kupata kazi nyingine so pale nikabaki mwenyewe na baada kama ya miezi miwili akaletwa mtumishi mwingine,changamoto inakuja yeye analipwa salary kubwa kuliko mimi na ni gap kama la 950k hivi ila mara nyingi kazi mimi Ndio namwelekeza na mara nyingi pia huwa naulizwa. Mimi moyo yea kufanya kazi haupo kabisa naona kazi ngumu Halafu mwenzangu analipwa vizuri.
Hebu wakuu mnisaidie katika hali hiyo nifanye nn?