Kazini imekuwa ngumu kwangu msaada

Kazini imekuwa ngumu kwangu msaada

Unafatilia sana maisha ya watu broo.
Kwa style hii kutoboa itakuachukua miaka mingi, Una uhakika gani kama analipwa hiyo we ndo unaidhinisha malipo??
 
Alete kwanza CV yake na CV ya huyo anayemlalamikia.

Kuna wajinga bado hawajui mtu anaweza kukuzidi madaraka na wewe ukamzidi mshahara.

Mwalimu mkuu wa shule anaweza kuzidiwa mshahara na Mwalimu wa kuwaida ambaye hana Madaraka.

Siwez weka cv yangu hapa ila experience na huyo ni Sawa kabisa
 
Shida mshahara ni mdogo
Mshahara haujawahi kutosha hata siku moja,acha kuangalia au kufuatilia mishahara ya wenzako,

Chapa kazi kama vile unafanya kazi bure ili upate experience usepe,au hata hapo wakiona utendaji wako ni mzuri watakuongeza,

Ongeza nidhamu na bidii ya kazi bila kuangalia mshahara,mambo yatabadilika tu au utapata wheel power na kuajiriwa kwingine.
 
analipwa salary kubwa kuliko mimi na ni gap kama la 950k hivi ila mara nyingi kazi mimi Ndio namwelekeza na mara nyingi pia huwa naulizwa. Mimi moyo yea kufanya kazi haupo kabisa naona kazi ngumu Halafu mwenzangu analipwa vizuri.
Usipoacha hiyo tabia utafutwa kazi soon.
Njia rahisi ya kupata mshahara zaidi ni kutafuta kazi kwingine, lakini uwe smart kwenye salary bargaining.
Mwajiri mpya anaweza kutaka reference kutoka hapo ulipo kwa sasa, hivyo chapa kazi vizuri. Mambo ya kusema moyo wa kufanya kazi huna kabisa yatakuponza!
 
Habarini wanajamii,niende moja kwa moja kwenye changamoto yangu.Nimeajiriwa kwenye taasisi moja hapa jijini dar,sasa katika ajira yangu kitengo nilichopo tulikuwa wawili mimi na huyo niliyemkuta yeye mwenzangu alikuwa kanitangulia kama miaka miwili pale kazini japo tulikuwa level moja ila kiwango cha mshahara alikuwa ananizidi kwa gap kama 800k kabla ya makato.
Baada kama ya mwaka mmoja jamaa aliondoka baada ya kupata kazi nyingine so pale nikabaki mwenyewe na baada kama ya miezi miwili akaletwa mtumishi mwingine,changamoto inakuja yeye analipwa salary kubwa kuliko mimi na ni gap kama la 950k hivi ila mara nyingi kazi mimi Ndio namwelekeza na mara nyingi pia huwa naulizwa. Mimi moyo yea kufanya kazi haupo kabisa naona kazi ngumu Halafu mwenzangu analipwa vizuri.
Hebu wakuu mnisaidie katika hali hiyo nifanye nn?
Acha wivu wa kijinga nenda kasome
 
Mtoa mada ulijuaje kama jamaa analipwa 950k zaidi Yako? Au alikwambia?
Lkn binafsi nimekuelewa sana mkuu kiukweli lzm ikukate maini. Kivyovyote lzm Kuna kitu hapo we endelea kuchunguza kama sio ensure ya udini hapo basi Kuna kiukabila.
 
Back
Top Bottom