#KaziNaBata Maana yake nini? REPOST

#KaziNaBata Maana yake nini? REPOST

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,890
Kazi na Bata — Maana yake nini hasa?

Zitto Kabwe

KATIKA mitandao ya kijamii na vyombo rasmi vya habari mwezi huu, kauli mbiu ya #KaziNaBata imepata msukumo mkubwa na nimekuwa nikipata maswali mengi kuhusu msemo huu unaojipatia umaarufu kila uchao.

Nimeona kwamba ni muhimu kwangu kutoa ufafanuzi wa msemo huu ili kwamba usipotoshwe au kupewa maana nyingine na watu ambao kwa namna moja au nyingine #KaziNaBata inawakera.

Siku zote, katika mapambano ya wanyonge kujikwamua kutoka katika makucha ya mfumo wowote, kumekuwa pia na ndoto ya kutaka kufaidi matunda ya jasho, machozi na damu yanayotokea wakati huo wa mapambano.

Kwenye kujikwamua kutoka katika makucha ya mfumo kandamizi, kunaweza kumaanisha hali bora za kiuchumi, heshima, haki na mambo mengine yanayoendana na hayo. Lakini mwisho wa yote, wanadamu watabaki kuwa wanadamu na watataka kufaidi matunda ya jitihada zao hizo.

Ni dhana ndiyo hasa ilikuwa msingi mkuu wa kauli mbiu maarufu ya wapigania haki za wafanyakazi mashuhuri wa karne ya 19 waliokuwa wakipigania mambo makubwa matatu tu kila uchao; “Saa nane za kufanya kazi, saa nane za kulala na saa nane za kufanya tunachotaka.

Mwaka 1912, kundi la wanawake waliokuwa wakifanya kazi katika mji wa Lawrence Massachusetts, uliokuwa kitovu cha viwanda vya kutengeneza nguo waligoma kufanya kazi kwa kudai malipo bora zaidi.

Ujumbe mkubwa uliokuwa umetamalaki katika mabango yao waliyoyabeba wakati wakiandamana ulikuwa ukisomeka “ Mikate na Mauaridi”. Kwa watafsiri wa misemo, ujumbe huo ulimaanisha kwamba watu wanataka kipato cha kuwatosheleza kula vizuri lakini pia kufanya mambo waliyokuwa wakiyapenda; jambo lililowakilishwa ipasavyo na alama hiyo ya uaridi.

Katika tafakari yake mujarabu kuhusu mapambano ya kudai Uhuru barani Afrika katikati ya k=arne ya 20, mwanamapinduzi kutoka Martinique, Ufaransa, Franz Fannon, alisema kwamba: “Kwa watu wanaotawaliwa, jambo lao la kwanza muhimu kwao ni ardhi yao. Ardhi ni muhimu kwa sababu ndiyo itakayowapa chakula na kulinda utu wao.”

Kwa kiasi fulani, tafakuri hiyo jadidi ya Fannon iliungwa mkono na mwanamapinduzi mwenzake wa Guinea-Bissau, Amilcar Cabral, aliyeshajiisha kwamba: “ Watu hupambana ili kuboresha maisha yao. Kuishi vema na kwa amani. Kuona wanaishi kwa muda mrefu na kwa maisha yenye kutia matumaini kuliko waliyokuwa wanaishi chini ya wakandamizaji.

Hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, naye kuna nyakati alionyesha wazi hisi zake katika mtazamo huu kwa kauli mbiu zake maarufu kama Uhuru na Maendeleo ambazo zilikuwa zikitekelezwa kwa vitendo kama ilivyokuwa kwenye vijiji vya Ujamaa –mfano mzuri zaidi ukiwa vilivyokuwa chini ya Ruvuma Development Association.

Kwa bahati mbaya, matamanio haya ya chakula, mauaridi na utu huwa hayapatikani. Hata katika utaratibu ule wa vijiji vya Ujamaa vilivyoanzishwa na serikali, utaratibu wa awali wa watu kukaa na kujipangia maendeleo yao ulivurugwa kwa mtindo mpya wa kupokea maagizo kutoka ngazi za juu.

Tangu aingie madarakani mwaka 2015, Rais John Magufuli ameibuka na kauli mbiu yake ya HapaKaziTu. Dhana hii ilijengwa katika msingi wa kupambana na rushwa ambayo ni tatizo kubwa hapa nchini na kauli mbiu ilitaka kutengeneza vuguvugu la kusafisha tatizo hilo na kuboresha utendaji wa serikali.

Kampeni hii ya Magufuli ilipokewa kwa moyo mkunjufu na walio wengi katika siku za awali za utawala wake ingawa sasa hali imebadilika na msisimko ule uliokuwepo sasa umegeuka kuwa fadhaa.

Badala ya vuguvugu hilo lenye kuleta matumaini ambalo aliahidi wakati wa kampeni za 2015 na katika siku zake za awali za urais, sasa hali imekuwa ya hofu.

Shughuli za kisiasa zimepigwa marufuku, wanasiasa wa Kitanzania sasa wanapigwa risasi na wengine wanatiwa nguvuni pasipo sababu za maana –huku waandishi wa habari na wanaharakati wakitoweka kusikojulikana, wanafunzi wenye mimba wakikataliwa kuendelea na masomo pasipo kusahau kadhia ya wavuvi, wafugaji na wakulima wanaotwezwa kupitia operesheni mbalimbali za kiusalama zinazoendeshwa na serikali hii.

Kwa upande mwingine, uchumi wa Tanzania unaelekea kwenye mserero wa kuporomoka na wananchi hawa wanyonge alioahidi kuwatetea ndiyo sasa wamegeuka kuwa wahanga wa kwanza wa siasa za Rais Magufuli.

Wamegeuka wahanga kwa sababu ahadi zinazotolewa na serikali kuhusu kuboresha sekta ya afya na elimu imebaki midomoni na kwenye makaratasi tu kwa sababu fedha zinazotangazwa kuwa zimepelekwa huko hazifanyiwi hivyo kibajeti. Kwa maana nyingine, ndugu zangu Waswahili wangesema zilongwa mbali, zitendwa mbali.

Utawala wa Rais Magufuli umeleta hali ngumu kiuchumi kiasi kwamba sasa kuna msemo mpya umeingia katika msamiati wa Kiswahili wenye kujaribu kuelezea kinachoendelea; Vyuma Vimekaza.

Kwa sababu ya ugumu unaoonekana katika maisha ya kila siku ya Watanzania, ile dhana ya HapaKaziTu aliyokuja nayo Magufuli sasa inachukuliwa kama ni neno la amri la kutaka mtu atekeleze jambo hata kama hataki kufanya hivyo.

Badala ya kuamsha amri ya uzalendo na kufanya kitu kwa matamanio makubwa ya yajayo mbeleni, HapaKaziTu imegeuka kuwa shuruti.

Mwanadahamu haishi kwa ajili ya kufanya kazi tu. Kwamba afanye kazi pasipo kuwa huru au kuona maisha yake yakibadilika hata kwa mambo ya kuonekana tu.

Kwa bahati nzuri, lugha ya Kiswahili, lugha adhimu ya taifa letu, tayari ina msamiti unaoleza kuhusu matamanio ya watu wake –Watanzania. Msemo wenyewe unasema “Kazi na Dawa”, ikimaanisha kwamba mtu yeyote anayefanya kazi, anatakiwa pia kuwa na jambo la kumpunguzia machungu na kumzawadia kwa jambo kubwa alilolifanya. Jambo la kujipongeza katika namna inayokubalika kisheria.

Jambo hilo sasa ndilo vijana wa kisasa wanaliita bata. Wahenga wetu waliliona hili miaka mingi kabla sisi wengine hatujaiona nchi yetu na vijana wetu wa sasa wanaliona hilohilo lakini katika lugha yao, muktadha wao.

Ukweli ambao haupingiki ni mmoja tu na umebaki hivyo kwa miaka yote; kwamba watu wanahitaji kufanya kazi lakini wanahitaji pia chakula mezani, wanahitaji kupendwa, wanataka uhuru wao, kutimiza haja zao, kuwa na maisha mazuri na kuwa na uhakika wa maisha yao ya sasa na baadaye.

Huu ndiyo ubinadamu. Huo ndiyo Utanzania. Kazi na Dawa, Kazi na Bata.

Watu wanahitaji kufanya kazi. Watu wanahitaji kufurahia maisha.
 
Lazma nifanye kazi na nifaidi jasho langu. Mm sio mashine ya kufanya kazi masaa 24. Hata mashine ina muda ambao ina pumzika na kufanyiwa repair. Hayo ya kazi tu muda wote mm hayanihusu. Nikitoka kazini naenda kuzurula, naenda kula mishkaki, naenda kutafuta mademu, naenda kuruka majoka, bafae narusi kupiga usingizi kesho yake naamkia kazini.
Wao wanafanya kazi muda wote?? Mbona tunamuona kigwangala ktka mitoko ya kila siku,,mara beach, mara zoo, anaogelea. Mm ni nani mpaka nigeuke punda?
 
We zitto unatusahau wanakigoma unakuja kupiga umbea mitandaoni... Unafikir lile ni koloni lako,tutaona 2020...labda urudi kwenu Burundi ukaloge..
Dah mkuu,hii inahusiana vipi na mada aliyoleta Zitto? Kama unahisi una jambo lako kuhusu huyu mtu kafungue uzi wako uanzishe mjadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulimzushia Raisi wetu kifo, internet haisahau, hakuna mtu aliwahi kwenda mbali kiasi hicho, wewe ni evil being, hata mtu akikuangalia usoni anaona evil ndani yako, what goes around comes around, internet haisahau kumbuka hilo kama hata una uwezo wa kukumbuka chochote.
 
Nchi za dunia nzima zimeshapata "UHURU" muda mrefu sana umepita. Ila Tanzania bado hatujapata "UHURU", bado tupo kwenye "UKOLONI".

Tanzania ndio nchi pekee duniani ambayo "SERIKALI" inaingilia na kujihusisha na "STAREHE" za raia wake.

CCM wanaendesha nchi kama kampuni vile toka chama kimeanzishwa, "BOARD OF DIRECTORS" wanakaa na kuamua kurithishana madaraka hata kwa wasiokua na weledi. Wanaendesha nchi kwa mazoea.

CCM ni masikini wa fikra. Uwezo wao wa kufikiria umefika mwisho (Kama ni tenki la mafuta lipo kwenye mshale wa E, na taa ya mafuta inawaka).

Inasikitisha watu na NGO's kila tukio baya (watu kutekwa, watu kuuliwa, watu kupotea, watu kubambikizwa kesi n.k) likitokea, wana "JISEMESHA NA KUTOA WITO" kwa mawaziri husika au serikali kuchukua hatua na kuzuia hayo matukio yasitokee. Mara ngapi matukio haya yametokea na hatua hakuna zilizochukuliwa??? Mara ngapi watu wameyapigia kelele na hatua yoyote haijachukuliwa???. Ni dalili tosha kwamba CCM uwezo wao umefikia mwisho kufikiri.

CHA KUSIKITISHA ZAIDI: Rais (Kama kiongozi wa nchi), ambae anaitwa kiongozi wa wanyonge, hajawahi hata kutoa "POLE, RAI, HOTUBA, KUSIKITISHWA" kwa utekwaji, uuwaji, ubambikizwaji kesi na ukandamizwaji kwa raia. Ina maana halioni hili???

Wanalazimisha na kuaminishwa "RAIA" ili kuunga juhudi kwa mambo ya msingi ambayo raia waliwapa uongozi kwaajili hio. Mtu analazimishwa kusifia ujenzi wa barabara, ujenzi wa hospitali, ujenzi wa madaraja, kuwajibisha mafisadi na viongozi wa umma, kuondoa wafanyakazi hewa. Kwa lipi??? Raia aunge juhudi kwa mambo ya msingi ambayo ni haki yake??? Mnapopewa madaraka (CCM) hio ni kazi yenu, hamjapewa madaraka ili muonekane kwenye T.V na jezi zenu za kijani.

Mtu anaweza kutoa sifa kwa "ZIADA INAYOFANYIKA" ya mambo unayofanya, kama vile kuondoa njaa, kuongeza ajira, kupiga vita umasikini, utandawazi na muongezeko wa biashara, uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari.

NB ukitaka kujua CCM ni masikini wa fikra.

CCM wameamua kumtumia "DIAMOND" aje kushindana na "ZITTO" kigoma na "RELI" ndio inatumika kama kishawishi kwa raia, hili limefanyika ili "JIWE" aoneshwe kwamba diamond ana ushawishi mkubwa kigoma. Kama walivoamua "TULIA" kushindana na "SUGU" mbeya, walivoona hana ushawishi wakaanza kuratibu kampeni za "MISAADA, TULIA TRUST" mpaka ya "KUKEJELI MSALABA" kwa kuweka kwenye jeneza la Chadema. Na "HARMONIZE" kugombea Tandahimba.
 
We zitto unatusahau wanakigoma unakuja kupiga umbea mitandaoni... Unafikir lile ni koloni lako,tutaona 2020...labda urudi kwenu Burundi ukaloge..

Magufuli amepanga nani atangazwe mshindi huko?
 
Back
Top Bottom