kitemaster
JF-Expert Member
- Jun 20, 2024
- 208
- 203
Mwalimu ukituliza kichwa unatoboa coz Una fursa ya kukopaWalimu hawausiki sio je sisi watendaji wa kijiji veo na meo
Mwalimu ukituliza kichwa unatoboa coz Una fursa ya kukopaWalimu hawausiki sio je sisi watendaji wa kijiji veo na meo
KumbeeVeo /Meo kima cha chini kimeongezwa.. Seminar na Vikao vya back to back vinawabeba..
Walimu Mikopo inawabeba
Sawa sawaMwalimu ukituliza kichwa unatoboa coz Una fursa ya kukopa
duh mkuu umeandika kwa uchungu sana. anyway, kazi ndiyo hutupa heshima. tufanye kazi kwa ujenzi wa taifa.Najua mmechoshwa na ' Uhimilivu wa deni la Mama ' sasa twende moja kwa moja kwenye Mada tajwa hapo juu, Zifuatazo ni kazi ambazo kutoboa kwake kupo mbalii sana..
Wafanyakazi wa Sheli za Mafuta.
Licha ya kufanya kazi kwa bidii na kujituma ila watu wa sheli wanapitia kipindi kigumu sana hasa kwa Loss na Mshahara kiduchu..
Walinzi wa Kampuni local
Licha ya kukesha usiku kucha lakini bado walinzi wanatumika km mtego hasa pale Lindo linapoingia dosari ya wizi. Walinzi wengi huangukia Gerezani hata kwa visa wasivyohusika navyo..
Wafanyakazi wa Super Market
Licha ya kuwa nadhifu muda wote lakini Hawa binadamu wanaishi maisha magumu sana, amini ninachowaambia..
Bodaboda
Ukiachilia mbali Maradhi ya kutisha Yale unayoyajua, basi barabara inatajwa kama sehemu Hatari zaidi kwa maisha ya binadamu.. Boda kutoboa ni ngumu saana
Waiter..
Hii kazi nayo kutoboa utapaskia tu kweny radio
Konda
Licha ya kuamka mapema na kufanya kazi ya kutupeleka miangaikoni lakini asilimia kubwa ya abiria bado Hawaoni thamani ya Konda.. Kwa siku moja pekee Konda anazozana na abiria wasiopungua 50, sasa Kuna kutoboa hapo kweli..?
Wenyeviti wa serikali za Mtaa
Hawa nao kutoboa huwa ni ngumu sana, hawana tofauti na mtu anayefanya Intern kwenye taasisi fulani.. fikiria unaamshwa saa kumi usiku kwa kazi ambayo mwisho mwa mwezi haupati kitu
Wauza Maduka ya Tabata na Sinza.. Hawa nao kutoboa kwao kupo mbaliii.. Unakuta duka limepambwa kama Sebureni sasa nani aingie kununua humo
Labor wa viwandani
Hawa nao kutoboa ni mtihani.. Pale Tabata Azam kwenye kiwanda cha Nida labor wanalipwa elfu5 kwa siku, wanakata chakula buku inabaki elfu4 na watu wanajaa kuomba kazi hadi wengine wanarudishwa nyumbani.. Halafu Kuna tahira huko linasifia CCM inaumiza sana..
Tuendelee kujituma na Kumwamini Mungu.. Yote yanawezekana..
View attachment 3366120
Hakika East or West.. home is the best 🙌Brake zime Ng'a Ng'ania home..Usitoke mpaka upate Mgao wako pakiuzwa
Kwann wafanyakazi wa Halmashauri ?Mawinga
Walimu
Wakulima
Wafanyakazi viwandani
Wafanyakazi wa halmashauri
Kwa wale wanaotoka maeneo yenye viwanda,madini uwa wanachukua mgao wao wa kimtindo achilia mbali 10% ya mauziano ya ardhi pamoja na magumashi yao ya ku backdate ardhi za watu kisha kuuza kwa wengine.Nina Shemeji yangu alikua bachela anaishi kwao anazuga mtaani tu, tukajipinda na dada yake tukamnunulia bodaboda mpyaaa akaanza kupiga kazi
Leo hii ameoa yupo na familia yake anakaa kwenye nyumba yake Tandika japo ni ndogo,
Anazo boda boda zingine 4 kawapa wenzake wanamletea hesabu na yeye bado anaendesha
Leo hii nikikwama nimpigie nimwambie niazime 500k ntarudisha siku fulani yaani ni fasta anakupa
Yote hii ni kwa kazi ya BODABODA tu
Wenyeviti wa serikali za mtaa siku hizi wana hela asikudanganye mtu, hawa huwa wana cover eneo kubwa sana kiutawala, kwa siku hakosi si chini ya watu 10 wanaokuja kufuata barua za utambulisho na ni lazima “kuchangia” 5,000 hela ya kalamu na karatasi. Na bado kuna issue kibao zinazotaka involvement ya mwenyekiti mitaani ambayo ni mwendo wa maokoto tu
Wenyeviti wa mtaaKwa wale wanaotoka maeneo yenye viwanda,madini uwa wanachukua mgao wao wa kimtindo achilia mbali 10% ya mauziano ya ardhi pamoja na magumashi yao ya ku backdate ardhi za watu kisha kuuza kwa wengine.
Kingine ni kwamba watu wanafanya kazi sio kuwa matajiri bali ni ili waweze kusurvive na kuweza kulipa kodi, kula na kuvaa na kama wana familia ili watoto wale, wavae nguo na wapate nauli za mwenda shule za serikali. Pia waweze kumudu matibabu ya kawaida.Sema uzuri ni kuwa hizo kazi hakuna anayefanya permanently
Leo atakua konda. .... then after 3 month anakuwa dereva
......Leo atakua mwenyekiti....kesho mbunge +waziri
Leo kibarua .......kumbe anasubiri ajira za TRA
Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
anakaa kwenye nyumba yake Tandika japo ni ndogo
Bado kuna vijiji ujafika uangalie wafanyabiashara vijijini walivyo na maisha kuliko hao uliowatajaKwa LEVEL za maisha ya vijijini mtumishi mwenye maisha bora anaanza Mwenyekiti wa kijiji halafu wanafuatia walimu na bwana shamba/mifugo wa kijiji 😂😂😂😂
Ni kweli barua ni bure lakini kuna kesi na faini za kindezi ndezi kweli huko hizo mwenyekiti anaokota balaa