Kazi zenye changamoto ya kutoboa

Kazi zenye changamoto ya kutoboa

Najua mmechoshwa na ' Uhimilivu wa deni la Mama ' sasa twende moja kwa moja kwenye Mada tajwa hapo juu, Zifuatazo ni kazi ambazo kutoboa kwake kupo mbalii sana..

Wafanyakazi wa Sheli za Mafuta.
Licha ya kufanya kazi kwa bidii na kujituma ila watu wa sheli wanapitia kipindi kigumu sana hasa kwa Loss na Mshahara kiduchu..

Walinzi wa Kampuni local
Licha ya kukesha usiku kucha lakini bado walinzi wanatumika km mtego hasa pale Lindo linapoingia dosari ya wizi. Walinzi wengi huangukia Gerezani hata kwa visa wasivyohusika navyo..

Wafanyakazi wa Super Market
Licha ya kuwa nadhifu muda wote lakini Hawa binadamu wanaishi maisha magumu sana, amini ninachowaambia..

Bodaboda
Ukiachilia mbali Maradhi ya kutisha Yale unayoyajua, basi barabara inatajwa kama sehemu Hatari zaidi kwa maisha ya binadamu.. Boda kutoboa ni ngumu saana

Waiter..
Hii kazi nayo kutoboa utapaskia tu kweny radio

Konda
Licha ya kuamka mapema na kufanya kazi ya kutupeleka miangaikoni lakini asilimia kubwa ya abiria bado Hawaoni thamani ya Konda.. Kwa siku moja pekee Konda anazozana na abiria wasiopungua 50, sasa Kuna kutoboa hapo kweli..?

Wenyeviti wa serikali za Mtaa

Hawa nao kutoboa huwa ni ngumu sana, hawana tofauti na mtu anayefanya Intern kwenye taasisi fulani.. fikiria unaamshwa saa kumi usiku kwa kazi ambayo mwisho mwa mwezi haupati kitu😂😂

Wauza Maduka ya Tabata na Sinza.. Hawa nao kutoboa kwao kupo mbaliii.. Unakuta duka limepambwa kama Sebureni sasa nani aingie kununua humo😂

Labor wa viwandani
Hawa nao kutoboa ni mtihani.. Pale Tabata Azam kwenye kiwanda cha Nida labor wanalipwa elfu5 kwa siku, wanakata chakula buku inabaki elfu4 na watu wanajaa kuomba kazi hadi wengine wanarudishwa nyumbani.. Halafu Kuna tahira huko linasifia CCM inaumiza sana..

Tuendelee kujituma na Kumwamini Mungu.. Yote yanawezekana..

View attachment 3366120
Nakubaliana na maandiko hayo
 
Leo atakuwa mlinzi kesho atakuwa ....hahaha kazi izo ni kufanya kwa muda na mshahara wake usitumie uhifadhi kufanya jambo jingine
Sema uzuri ni kuwa hizo kazi hakuna anayefanya permanently

Leo atakua konda. .... then after 3 month anakuwa dereva

......Leo atakua mwenyekiti....kesho mbunge +waziri

Leo kibarua .......kumbe anasubiri ajira za TRA

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Sawa ila ni uswahilini sana bora angetafuta kiwanja Kibaha

Kuishi uswazi ni ujinga kama ujinga mwinginr
Uzuri wa JF kila mtu ni TAJIRI anaishi USHUANI na sio mswahili 😂😂😂😂

Mkuu Tandika kuna watu wanamajumba yao ya kuishi baadhi ya nyumba Masaki na Obey wanasubiri

USIKARIRI MAISHA MKUU
 
Uzuri wa JF kila mtu ni TAJIRI anaishi USHUANI na sio mswahili 😂😂😂😂

Mkuu Tandika kuna watu wanamajumba yao ya kuishi baadhi ya nyumba Masaki na Obey wanasubiri

USIKARIRI MAISHA MKUU
Ukweli utabaki palepale kwa mtu anayejielewa hawezi kujenga Tandika
 
Back
Top Bottom