kazi za mabox ndio kazi gani?

Pretty

JF-Expert Member
Mar 19, 2009
2,575
552
Jamani naombeni mnifahamishe maana mie nasikia kuwa huko ughaibuni yaani USA na Ulaya watu wengi wanafanya kazi za kubeba box na zinapondwa sana bongo. Sasa huwa najiuliza ndio kazi gani hizo? anayefahamu please nifahamisheni mwenzenu.
 
kupanga mabox ya sabuni au soda shaw's au stop and shop, au new york hakuna shaw's?
bongo majungu mengi.
 
Ni manual labour, wanaziita maboxi kwa sababu kuna kazi nyingi sana za kubeba maboxi ya bidhaa. Kwa mfano niliwahi kufanya kazi ya "Pack Out Crew" duka la vifaa vya nyumbani/ujenzi Home Depot, bidhaa zinakuja kwenye malori mnayafungua maboxi mnapanga vitu vinapotakiwa kwenda.

Nilikua mwanafunzi lakini kuna watu wanaendesha familia kwa kazi kama hiyo na maisha ya sio mabaya, benefits kibao, so sidhani kama ni kazi ya kudharauliwa. Sio kila mtu anahitaji kuwa baller!
 
Kupiga Box ilianzia kama kazi za kubeba mabox supper markets na madukani ughaibuni. Sasa ni kazi zozote manual zinazofanywa kwa ajili ya kuendesha maisha yao na kusaidia nyumbani Bongo.

Sio kweli kuwa kazi hizo zinadharauliwa, ili sisi baadhi ya wabongo wanatabia ya kujisikia bora zaidi kwa sababu fanafanya decent jobs (kazi za maana) na kuwadharau wenzao wabeba box.

Ukweli ni kuwa issue sio kazi gani mtu anafanya, muhimu ni kupata/kujenga maisha bora. Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua. Kuna watu wapiga box huku wanaendesha maisha mazuri na kusaidia sana nyumbani wakati huo huo kuna hao wenye kazi za maana huku maisha yanawapiga na wengi wao wanajengea 'chini'.

Kitu muhimu kuhusu hizi kazi za box, zifanywe huku ukialia mbele na kukumbuka nyumbani, maana ukizifanya kwa miaka mingi bila malengo, unafikia wakata akili inagota, umri unapanda mpaka unafika mahali box haibebeki tena na kujikuta huna jingine uliwezalo.

Mimi mwenyewe sio box tuu nimebeba bali mpaka zege huko ughaibuni. Kuna wenzetu wengi wamewin na sasa maisha ni mazuri, kila mwaka likizo ni Bongo na maendeleo kwa kwenda mbele. Pia kuna wenzetu wamerost, Bongo ni kituo cha polisi, hata ikitokea shida home, nauli ni issue.

'Kazi ni kazi bora mkono uende kinywani'

.
 
kupanga mabox ya sabuni au soda shaw's au stop and shop, au new york hakuna shaw's?
bongo majungu mengi.

Sasa hapo majungu yako wapi wakati umekubali kuwa kazi za kubeba maboksi zipo? nadhani kama ni zipo bora kuzijua tu na wala tukizirtaja hatuzidharau, mimi mwenyewe natarajia kuja huko kusoma hope nitapa maelekezo ya kupata hizo kazi za kubeba mabox humu humu JF
 
Kitu muhimu kuhusu hizi kazi za box, zifanywe huku ukialia mbele na kukumbuka nyumbani, maana ukizifanya kwa miaka mingi bila malengo, unafikia wakata akili inagota, umri unapanda mpaka unafika mahali box haibebeki tena na kujikuta huna jingine uliwezalo.

Mimi mwenyewe sio box tuu nimebeba bali mpaka zege huko ughaibuni. Kuna wenzetu wengi wamewin na sasa maisha ni mazuri, kila mwaka likizo ni Bongo na maendeleo kwa kwenda mbele. Pia kuna wenzetu wamerost, Bongo ni kituo cha polisi, hata ikitokea shida home, nauli ni issue.

'Kazi ni kazi bora mkono uende kinywani'

.

Ha ha haaaaaa, hilo kubwa, nimuhimu wabongo wajue ugaibuni hakuna dili m=kama huna speciall skills wasidanganyike wakaja kupigika na mabox huku. Wacha wanaokuja shule wabebe box kwani wapo shule lakini nao wasilowee hiyo point bolded ni mhimu waijue.
 
Kazi zimegawanyika katika mafungu matatu
1. Skilled - ni kazi ambayo uwezi kufanya mpaka uwe mjuzi, au unatumia uwezo wako wa shule ie doctor, engineer......
2. Semi skilled - hii mara nyingi inatokana na mfanyakazi kufanya kazi mda mrefu katika sehemu na kujua kazi ambazo skilled wanafanya na kuaminika na kuwa anafanya hizo kazi, pia kuna kazi zinahitaji ujuzi lakini sio wahali ya juu.
3. Unskilled (maboxi) - kazi zote ambazo mtu anaweza kufundishwa leo kesho akaanza kufanya mwenyewe haziitaji shule. Cashier dukani benki popote pale, kazi za viwandani lakini sio maengineer, kazi za kwenye maghala, udereva, kuongea na simu.
Kuna kazi kama receptionist, kuongea na simu, cashier watu wanapenda kuziita semi skilled ili kujipandisha chati lakini ni unskilled job.

Kwa mfano tz kazi za mabox - dahaco, bandarini, breweries, receptionist, dereva.

Watu wanaweza kuanza na kazi za maboxi na wakatajiria. Muuza duka anaweza kuanza kuuza duka mpaka na yeye akawa na duka lake. Dereva wa pizza anaweza baadae akawa na duka lake.

Mimi wakati nasoma nilikua nafanya kazi part-time pizzahut na mwenye pizza hut yetu alianza kuwa dereva na sasa hivi ana franchise tano za pizzahut.

Na mimi hiyo kazi ya maboxi imenisomesha, kuna watu wamejenga wengi tu kwa hiyo inategemea na wewe unatumiaje hiyo hela yako.

Mfano madereva wa magari ya mafuta tanker wanapata £40,000 hii ni zaidi ya skilled job nyingi tu.
 
mbeba box anapata mshahara kima cha chini kama vile bongo nako kuna kima cha chini,tofauti inakuja kwenye hali ya maisha,whereas huyu wa bongo ana struggle kupata a square meal huyu mbeba mabox anasahau hata kula,kipato chake kinafanya msosi kama bure.wabeba mabox wengi kwa standard za bongo ni sawa au zaidi ya watu wenye white collar jobs
 
Kubeba Mabox,
Hii kazi mie wala siiogopi wala kunitisha maana Ngosha nazizimia sana kazi za mtulinga. Ila kuna moja tu ambalo huwa naliogopa, nalo ni siku ukifa na hapo Ndugu na marehemu kama unao wanakufanyia mazishi na kujenga kaburi zuri na maneno juu yake :-
"HAPA AMELALA MBEBA MABOX ............ RIP"
 
kumbe ndio kazi za box ehe! manake naona watu wanaponda sana hizi kazi. Nashukuru kwa kunifahamisha.
 
Kazi zimegawanyika katika mafungu matatu
1. Skilled - ni kazi ambayo uwezi kufanya mpaka uwe mjuzi, au unatumia uwezo wako wa shule ie doctor, engineer......
2. Semi skilled - hii mara nyingi inatokana na mfanyakazi kufanya kazi mda mrefu katika sehemu na kujua kazi ambazo skilled wanafanya na kuaminika na kuwa anafanya hizo kazi, pia kuna kazi zinahitaji ujuzi lakini sio wahali ya juu.
3. Unskilled (maboxi) - kazi zote ambazo mtu anaweza kufundishwa leo kesho akaanza kufanya mwenyewe haziitaji shule. Cashier dukani benki popote pale, kazi za viwandani lakini sio maengineer, kazi za kwenye maghala, udereva, kuongea na simu.
Kuna kazi kama receptionist, kuongea na simu, cashier watu wanapenda kuziita semi skilled ili kujipandisha chati lakini ni unskilled job.

Kwa mfano tz kazi za mabox - dahaco, bandarini, breweries, receptionist, dereva.

Watu wanaweza kuanza na kazi za maboxi na wakatajiria. Muuza duka anaweza kuanza kuuza duka mpaka na yeye akawa na duka lake. Dereva wa pizza anaweza baadae akawa na duka lake.

Mimi wakati nasoma nilikua nafanya kazi part-time pizzahut na mwenye pizza hut yetu alianza kuwa dereva na sasa hivi ana franchise tano za pizzahut.

Na mimi hiyo kazi ya maboxi imenisomesha, kuna watu wamejenga wengi tu kwa hiyo inategemea na wewe unatumiaje hiyo hela yako.

Mfano madereva wa magari ya mafuta tanker wanapata £40,000 hii ni zaidi ya skilled job nyingi tu.

Mkuu, nakupa tano!

Mimi nilipotia mguu ughaibuni, nikaamua kuchanganya maboski na shule. Nikawa naingia box usiku na shule inakuwa mchana pamoja na kwenda maktaba.

Mwanzoni ilikuwa ni taabu kidogo lakini nikazoea na kuweza kubukua na kuambulia ka-bsc kangu. Hii nazungumzia miaka ya mwishoni mwa 90 na mwanzoni mwa 2000.

Lakini kwa sasa maboski ni kazi ngumu na hailipi sana kwa sababu ya ushindani katika "labor market".Ila bado inaweza kutoa salio zuri tu la kuweza kuwekeza kule mtu anakotoka kulingana na mipango imara.
 
Jamani naombeni mnifahamishe maana mie nasikia kuwa huko ughaibuni yaani USA na Ulaya watu wengi wanafanya kazi za kubeba box na zinapondwa sana bongo. Sasa huwa najiuliza ndio kazi gani hizo? anayefahamu please nifahamisheni mwenzenu.

Shosti nafikiri kaka Lemutuz William Malecela atatokea sasa hivi akupe ufafanuzi maana yeye ni nguli wa mambo hayo
 
Back
Top Bottom