Kazi yake mola - Madee

Kazi yake mola - Madee

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
36
Reaction score
55
KAZI YAKE MOLA - MADEE

Madee Seneda amefunguka na kudai siri ya wimbo wa kazi yake mola kufanya vizuri mpaka sasa ni kutokana na kutuliza kichwa wakati anaandika mashairi yake tofauti na vijana wa sasa ambao wanaingia studio wakiwa hawajui wanataka kuimba nini.

Madee amesema kuwa pamoja na kuwa zimeimbwa nyimbo nyingi zenye mahadhi ya maombolezo lakini 'Kazi yake Mola' bado imeendelea kuwa wimbo bora kutoka na mashahiri kupangiliwa kwa ubunifu wa hali juu ikiwa ni pamoja na 'beat' ya P. Funk Majani.

"Kazi yake Mola P. Funk aliitengenezea beat ambalo mpaka sasa limeweza kudumu, lakini pia mashairi niliyaandika kwa umakini mkubwa kwani ndo nilikuwa nimepatiwa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu. Japo wimbo haukuwa wa kutoka officially lakini nilijitahidi kuandika mashairi yenye maudhui, ndio maana mpaka sasa wimbo unaonekana hit. Vijana wa sasa wameshindwa kutoa nyimbo itakayoizidi 'kazi yake mola' kwani wengine mpaka wanaingia studio hawana hata mashairi wanataka wasikie mdundo ndio wapate kitu cha kusema"- Madee

#funguka.

Je? KWA mtazamo wako ni wimbo upi Bora kwako wenye maudhui ya msiba...

MADEE - KAZI YAKE MOLA.

Chorus

"kazi yake mola, haina makosa/
kazi yake mola, haina makosa/
anafanya atakalo, anafanya awezalo/

kwani dunia ni yake na hakuna hashindwalo/
kazi yake mola, haina makosa/
kazi yake mola, haina makosa/
anafanya atakalo, anafanya awezalo/
kwani dunia ni yake na hakuna hashindwalo/

Verse 1.

umekuta dunia imeandaliwa/
na we bila hiyana si ukazaliwa/
umekuta wasafiri
waliotutoka kwaheri/
kimwili hauko nasi
kiroho tupo nawe/
upo kwenye kina kati juu mawe/
mchana na usiku tunaomba tuwe nawe
haiwezi kuwa sawa/
ugonjwa unatibika, mauti hayana dawa/
kwa heri mwanahawa, kizima huaribika
kufa na kupotea/
mchana na usiku dua tunakuombea/
ulale mahali pema huku unatungojea/
njia yetu ni moja ipo siku utatupokea/
salamu wasalimie wote utao wakuta/
wambie babu tale/ machozi keshafuta
na keshalala matanga
tangu enzi zile/ alipoondoka kichanga/

Chorus..

Kazi yake mola, haina makosa/
kazi yake mola, haina makosa/
anafanya atakalo, anafanya awezalo/

kwani dunia ni yake na hakuna hashindwalo/
kazi yake mola, haina makosa/
kazi yake mola, haina makosa/
anafanya atakalo, anafanya awezalo/
kwani dunia ni yake na hakuna hashindwalo/

Verse 2.

"hii ni siri kubwa aloipanga manani/
ata abdu bonge siku yako haijulikani/
ata ukiwa na body kama producer majani/
lazima uta kwenda vyovyote inalazimu/
haina pakujificha siku yako inapotimu/
tumuombee mwanahawa yupo kwenye mustahikimu/
awe na ufahari mwili ukiwa kuzimu/
umemwacha mpweke ibra model anakuwaza/
kwani kila kukicha ye maswali anauliza/
mjomba iddi eti mama yuko wapi?
inanibidi niongope huku sitaki/
naangaza pale mbele mama chale -n-lia/
pembeni namuona kwembe tall na ramia/
mbele yao ukungu futa machozi mama dulah
yote kazi ya mungu/
jikaze kama mwanzo alivoondoka
ally zungu.

Chorus

Kazi yake mola, haina makosa/
kazi yake mola, haina makosa/
anafanya atakalo, anafanya awezalo/

kwani dunia ni yake na hakuna hashindwalo/
kazi yake mola, haina makosa/
kazi yake mola, haina makosa/
anafanya atakalo, anafanya awezalo/
kwani dunia ni yake na hakuna hashindwalo

End..

.😭😭😭😭😭. Rest in mandojo..

Moyo wangu una maumivu makali; Nitakukumbuka sana kaka na rafiki yangu. Pumzika kwa amani Mandojo. Hakika maisha ya mwanadamu ni mafupi sana hapa duniani. Pole kwa ndugu, jamaa, na marafiki, na pole sana kaka yangu @domokayatz. Kazi ya Mungu haina makosa,

Kifo cha Mandojo kilitokea siku chache kabla ya siku yake ya kuzaliwa Agosti 22.

Yeeebaba......

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
1771961346753.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom