Kazi ya Uafande inahitaji moyo. Wewe unayeolewa au kuoa Afande hongera sana!

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Nakumbuka miaka ya 1990's nikiwa nasoma kidato cha Nne mkoani Singida!
Enzi hizo shule yangu niliyokuwa nasoma ilikuwa na umbali wa Kilomita kama 15 hivi hadi mjini ambapo ndipo kuna Guest House (nyumba za kulala wageni) na huduma zingine ambazo ni faafu hasa kwa wageni ambao wangeweza kupata ziara ya kuja shuleni kwetu.

Kiufupi shuleni kwetu palikuwa polini kiasi kwamba nilisoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha Nne nikiwa sijui hata umeme unakuwakaje...

Lakini nimshukuru mungu kwa kuwa shule yangu ambayo ilikuwa bushi ilinisaidia na kunifanya nisome kwa bidii hadi Leo Mwanangu ninamsimulia tu maisha ya shule niliyosoma anabaki akicheka na kufurahia kama hadhithi za Juma na Uledi,

Basi bwana nisiende nje ya mada...nimejaribu kutolea ufafanuzi mazingira ya shule yangu ukiwa kama njia ya kutetea Maafande wenzangu kwa kile nilichokiona wakifanya kipindi hicho!

Nakumbuka katika kipindi cha mitihani waliletwa Afande wasimamizi katika kituo cha shule yangu.
Walikuwa Afande wawili wa jinsia tofauti yaani wa kike na wakiume

Lakini wageni hawakuwa peke yao bali na walimu wengine wasimamizi walikuwepo japo wao walipata nafasi ya kuwa wanalala kwa Mkuu wa shule ila wale Afande wao walipewa kigodoro kidogo na shuka moja na wakawa wanalala ofsini kwa Mkuu wa shule.....!

Kama kuna Afande ambae mazingira ya kikazi yalishawahi kumfanyia haya asogee hapa atuambie ukweli kipi kiliendelea kati yao na ni mda wa takriban wiki 2!
 
Mkuu umezaliwa 1992 na miaka ya 1990's ulikuwa kidato cha nne
Screenshot_20180909-161652.jpg
 
Waacheni wafu wazikane, hata wakulima tunakulana mashambani, kila mbuz hula kadil ya urefu wa kamba yake
 
Ha ha ha,anayekaa muda mwingi na mkeo/mumeo iwe kazini au sehemu yoyote ile ni hatari zaidi,ibilisi lazima awapitie.
 
Back
Top Bottom