Kazi ya mikono yetu

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kazi ya Mungu ni ya kiwango cha juu zaidi ya Kazi ya mikono ya binadamu. Ushahidi wa hili uko dhahiri machoni petu. Hata zile Kazi tunazoita zetu sio zetu. Kwasababu Mungu ndiye aliyetuumba na akatupa akili,macho, miguu na mikono ya kufanya kazi.
Kazi yeyote njema na nzuri hutoka kwa Mungu. Huwezi kulinganisha kazi ya mikono ya mwanadamu na ile ya Mungu katika ubora na ufanisi.

Kuna falme mbili zinazopingana ufalme wa nuru na ufalme wa Giza. Na falme zote hizo hujengwa na matendo yetu pamoja na mawazo yetu.

Pale binadamu wanapoenda kinyume na njia iliyosahihi na njema wanajenga ufalme Wa Giza na Nuru hutoweka miongoni mwao.

Matendo mema humuita Mungu na kujenga ufalme wake lakini Matendo maovu humuita shetani kujenga himaya yake.

Ni muhimu kwetu kutafakari njia ipi bora kwetu na kwa familia zetu. Je tumfuate Mungu ama shetani? Matendo yetu ndio Yatatuweka katika sehemu hizo mbili.

Kwa kutenda Matendo mema tunakuwa wema na kutenda Matendo maovu tunakuwa waovu na kuwa mbali na Mungu aliyetuumba. Hakuna njia yeyote kwetu kupata amani kama tutatenda maovu.

Mungu atapata faida gani kwetu sisi kutenda mema au maovu? Mema yetu au maovu yetu ni kwa faida au hasara yetu. Uovu wetu hamgusi Mungu Bali sisi wenyewe wenye nyama na damu. Lakini ukweli ni kwamba anatupenda na hataki tuangamie au tupotee. Anataka tuwe na amani na furaha. Bali Matendo yetu ndiyo yaliyofanya dunia tuliyonayo sasa ni zao la Matendo na mawazo yetu.

Kwahiyo Kazi ya mikono yetu ndio itakayo tengeneza baadae yetu kuwa njema au mbaya. Kwa mawazo yetu na fikra zetu tunazaa Matendo yetu. Na tumetengeneza dunia tuliyonayo kwa mazao ya fikra na Matendo yetu. LAKINI tuna kizazi kinachokuja na kizazi kinachokuja mwelekeo wake kitategemea sana fikra tulizonazo. Fikra hizi ndizo muongozo katika malezi.

Matumaini yetu yanategemea sana aina ya Matendo na mawazo yetu. Dunia tuliyonayo ni Kazi ya mikono yetu. Na tutavuna tulichopanda.
 
Back
Top Bottom