Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,217
- 1,705
Zek 8:15 SUV
[15] vivyo hivyo nimeazimia katika siku hizi kuutendea Yerusalemu mema, na nyumba ya Yuda pia; msiogope.
Kila mmoja anahitaji kufanyiwa jambo jema na Mungu, jambo la kuonekana kwenye maisha yake, awe na jambo la kujivunia ukuu wa Mungu.
Ikiwa Yerusalemu uliazimiwa na Mungu kutendewa mambo mema, inatupa kuelewa kuwa Mungu anatuwazia mema wanadamu au watoto wake.
Mungu anaweza kuazimia kutenda jambo jema kwetu, ila lipo sharti la kutenda hilo jema, tunatendewa bure ila lazima tufuate vile Mungu anataka tuishi.
Mungu anatutaka tuwe watu wa kweli, watu wa haki, watu wasiowaza mabaya juu ya watu wengine, watu waaminifu mbele zake, ndipo tutaweza kuona matendo makubwa ya ki-Mungu kwetu.
Zek 8:16-17 SUV
[16] Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme kweli na jirani yake; hukumuni kweli na hukumu ya amani malangoni mwenu; [17] wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA.
Ukitenda yaliyo machukizo mbele za Mungu, alafu ukataka Mungu atende mambo mema kwako, unaweza kupishana na hizo baraka.
Mungu ataka atubariki tukiwa ndani yake, tukiishi maisha anayoyataka tuishi au aliyotuamuru tuyaishi, ametupa mwongozo mzuri kupitia neno lake.
Kuna baraka tutazipata tukiwa ndani ya Yesu, zingine tutazipata tukiishi maisha yanayompendeza Mungu, na kujiweka mbali na yaliyo machukizo mbele zake.
Ahadi za Mungu ni za kweli, sio hivyo tu, Mungu yupo wazi, ukitaka kumwona akihusika moja kwa moja kwako unahitaji kukaa katika njia yake. Ili kesho ukifanikiwa usiseme nguvu zako, akili zako, na uwezo wako wa kifedha umekusaidia.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana