jitwangabalogi
JF-Expert Member
- Aug 8, 2018
- 480
- 638
Matumaini yetu ni wazima wa afya wakuu!
Katika Sayari hii ya tano tokea Pluto hakuna kiumbe chochote kisichokosea, sio Wachungaji, Mitume, Manabii, Madokta Wazamivu, Masikini, Matajiri n.k. Je, si ukweli ya kwamba wakuu na hata great thinker nao hukosea? Hakuna aliyekamili tangu hapo mwanzo wa neno, sisi wote ni wakosaji na tutaendelea kukosa ingali kama tunaendelea kuishi.
Ndugu zangu wapendwa wangu, yatupasa kusamehana sisi kwa sisi katika yote yale tunayokoseana, kwa nini unahukumu mapungufu ya jirani yako bila kujitazama mapungufu yako kwanza? Sioni kosa kubwa ambalo kalifanya Magufuli ambalo haliwezekani kusameheka. Je, ni ukweli ya kwamba awamu nne zilizotangulia hazijakosea? Kuna haja gani ya kubeba chuki mioyoni mwetu dhidi yake?Yyatupasa kushirikiana naye na kumuunga mkono katika atendayo kwa maslahi yetu sasa na hata vizazi vijavyo. Je, si ukweli sisi wote ni watoto wa mama mmoja/ Tanzania?.
Tupendane, tupendane, tupendane ndugu zangu, kwa njia hii ya upendo itatufanya tuishi kwa amani na ushirikiano baina yetu na hata aliye Baba aliye juu atatubaliki na kutuzidishia katika tufanyayo.
Tuache kuishi kwa visasi, uongo, roho mbaya, chuki, tamaa, tuepuke ufitinishi, tujizuie kujitukuza na yale yote ambayo sisi wenyewe hupendi kufanyiwa"
#amani ya bwana wetu iwe pamoja nasi
Amen: