Kazi sawa ila mshahara tofauti idara ya wanyamapori

Ivindo

Senior Member
Feb 11, 2016
168
239
Hivi inakuaje mtu mnafanya kazi moja ,mnalinda mnyama mmoja, wote mnatumia silaha moja, mnadeal na majangili wanaofanana alafu mtu anaeajiriwa TANAPA (askari) tena form 4 mwenye div 4 anaanza kwa kulipwa 1,200,000 na Ngorongoro anaanza na 1,450,000 na serikalini (serikali kuu na TAMISEMI anaanza kwa 345,000). Why? kwa nini Mr President Magufuli? hapo kuishi kama shetani ni kupi?

Mdogo wangu ameomba nafasi TANAPA ndipo nimegundua kuwa kuna hizi descrepancy. Hii naona sio kabisa, au mdau unaonaje? Naomba tu hawa watu muwape mshiko sawa ili wanyama wetu wasijeteketeza wanyama wetu. Kweli mlinzi analinda tembo mwenye meno 2 ambayo akiuza anaweza acha hata kazi na unamlipa 345,000 kwa siku 30? kabisa yani risk zote za kuumwa na nyoka, kukutana na wajangali adha ambazo hata anaelipwa 1,450,000 anakutana nazo.

Hii ikanifanya nifanye research kdg kujua hawa wenzetu wanautawala gani katika haya mambo. Kumbe TANAPA ni kitu tofauti, Ngorongoro ni tifauti yani hadi uniform zao, na serikali kuu ni tofauti. Wenzetu Kenya wanyamapori wote wako chini ya KWS, Uganda UWA, Zambia ZAWA etc. Sasa nyie Watanzania nani aliwambia muwe na wanyamapori wengi wengi hivyo mpk salary zinakua kama urefu wa vidole?

President Magufuli, Maghembe Mh (Mb) fanyeni hii maneno ikae vizuri, juhudi za kupunguza ujangili zianze hapaaa

Nawasilisha
 
Duh hizi ni scale kwa wanaoanza au??
Ni kufuru, hapo ndo utaona maisha ya Tanzania hakuna haki kabisa. Mtu unakazana kupiga msuli darasani kwa kukesha hadi chuo kikuu unachukua kozi ambazo serikali imezifanya kuwa za njaa(ualimu) alafu mwingine anakuwa hana habari kabisa na kusoma lakini kupitia ujanja ujanja anaingia TANAPA anatusua maisha.
 
Kwa kweli inauma sana sipatii picha wanafanya kazi huko wanapojizua hizi tofauti juu ya mishahara yao huwa wanajisikiaje
 
Back
Top Bottom