Kazi hiyo

Rubi

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Messages
1,623
Likes
49
Points
145

Rubi

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2009
1,623 49 145
Kijana mmoja aliyekuwa anatafuta kazi alifanikiwa kupata kazi katika zoo


ya wanyama. Kijana huyo ilimbidi afanye hiyo kazi japo ni ngumu lakini


alikuwa hana jinsi. Kazi hiyo ilimtaka kijana huyo kuvaa ngozi ya sokwe
na kurukaruka kwenye banda la sokwe ambae alifariki ghafla, kwa kuwa
watalii wengi walimpenda huyo sokwe, ilibidi mmiliki wa zoo amfundishe
huyo kijana staili zote ambazo Yule sokwe alikuwa akiruka.

Kijana alifanikiwa mbinu hizo na kuanza kazi mara moja huku watalii
wakimiminika kuona sokwe wao karudi.

Siku moja kijana huyo katika kurukaruka kwake kwa sifa alijikuta
amedondoka kwenye banda la simba. Simba huyo alimkimbilia huyo kijana na
kumuinamia huku watalii wakishangaa kuona nini kitatokea.

Kijana alianua mdomo kwa kutaka kupiga kelele mana alishaona maisha
yake yako hatarini
lakini cha ajabu alisikia simba akimnong'oneza ''Acha kelele tutafukuzwa
kazi''
 

Forum statistics

Threads 1,191,696
Members 451,730
Posts 27,717,962