KAWAMBWA na MULUGO nani Afadhali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KAWAMBWA na MULUGO nani Afadhali?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by blessings, Oct 25, 2012.

 1. b

  blessings JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 5,073
  Likes Received: 2,860
  Trophy Points: 280
  Wanajamvi hivi katika ya hawa waziri na naibu waziri wa Elimu nani ana afadhali katika utendaji wizarani, kujibu hoja bungeni, na kweli walistahili kupewa wizara hii nyeti(pre-primary, primary, secondary &college&universities zipo chini ya wizara hii ya Elimu, japo kuna baadhi ya majukumu ya Primary &secondary yamepelekwa TAMISEMI au wangepelekwa MIFUGO na UVUVI? au OMR-MAZINGIRA wakapambane na wauza mkaa? (siuliziii kiwango cha Elimu kwao) maana inafahamika wazi.
   
 2. N

  Njaa Mbaya JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 667
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wote wachovu sana nadhani kazi inayowafaa labda kuuza nyanya wanaweza lakini kazi nyeti kama waliyonayo hapana uwezo wao ni mdogo sana na ni aibu mno kuwa na watu kama hawa kwenye taasisi nyeti kama hii ya kukuza uelewa wa watanzania. Kama ningekuwa rais ningemfukuza kilaza Mlugo mara moja kwa upuuzi aliofanya na kuliletea taifa aibu kubwa duniani
   
 3. M

  Mea2 Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tatizo la mulugo nikutumia lugha ambayo ujahizoea vizuri kama mlimwelewa vizuri alikua anajaribu kutaja 1964 kama tunavyosema kiswahili mwaka elfu moja mia tisa sitini na nne,sasa yeye akajikuta kaanza na moja na kurudia elfu moja akapoteza kabisa mwelekeo,kwanini tusiwaige wenzetu wanao tumia lugha za mataifa yao hata kama yupo ugenini si TUNAIGAIGA TU SIKU HIZI UKIONEKANA UNAONGEA KIZUNGU BASI WEWE NDIYO MWELEWA HUU NI ULIMBUKENI
   
 4. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mh Kawambwa ni "Kiraka" wa serikali maana amezunguka (soma "zungushwa") wizara zaidi ya nne au tano katika kipindi cha miaka saba ya Uwaiziri wake. Nisichojua ni kwamba anabadilishwa wizara mbali mbali kwa sababu ya efficiency au kinyume chake? Na kama ni anahamishwa baada ya kuharibu kwa nini asipumzishwe? Au akarudi COET kufundisha wahandisi wetu?

  Kuhusu Mulugo sina mengi ya kusema sana ila nafikiri anatumia nguvu nyingi katika utendaji kazi wake badala ya weledi. In fact anaonekana kama anataka kum-impress bwana mkubwa ili aweze kuendelea kuwa waziri mdogo au hata waziri kamili hapo baadae.

  Nakumbuka kuna kipindi alipiga mkwara kuwa yeye hatakuwa tayari "kufukuzwa kazi" kwa sababu ya watu wengine. Hii inaonyesha kwamba focus yake ni kuendelea kuwa waziri na si nchi itafaidi vipi uwaziri wake. Mtu kama huyu hata akikosea kujiuzuru ni ndoto.
   
 5. M

  MICHAELML New Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naombeni Kuuliza Maana Hii Ishu Ya Mulugo Naisikia Ckia 2 Na Wa2 Bado Hawaamin. Naomben Mnihakishie,kwan Mulugo Amefanyeje?
   
 6. Makbel

  Makbel JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 774
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kaka upo Sayari ipi?
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Nenda youtube andika Mulugo utaona alichofanya!hutaamini
   
Loading...