Kauli za WanaCCM "Hatutaki Vilaza Vyuo Vikuu" zawatokea puani leo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Watoto wa maskini walipofukuzwa chuo kikuu japo wamefaulu vijana wa CCM walianzisha hashtag wakisema ‪#‎HatutakiVilazaVyuoVikuu‬. Leo vijana walewale wamegeuka na kuanza kumtetea "kilaza" aliyeachwa UDOM kisa tu kilaza huyo ni mtoto wa mkubwa. Unafiki, unafiki, unafiki usioelezeka. Hakuna dhambi kubwa kama kumnyanyasa mnyonge kwa sababu tu hana mtetezi.

Mtu anasimama kwa ujasiri eti Jesca alisoma certificate kisha Diploma, kabla ya kujiunga chuo kikuu. Huu ni uongo mkubwa na ni unafiki wa kiwango PhD kwa sababu zifuatazo;

‪#‎Mosi‬, Muongozo wa NACTE (NACTE Standard Operating Procedures, 2005) hauruhusiwi vyuo vilivyosajiliwa na NACTE kudahili wanafunzi wenye ufaulu chini ya division four points 28. Maana yake ni kuwa ili usome certificate itakayokuwezesha kusoma Diploma na hatimaye Degree ni lazima uwe na four isiyozidi ya points 28.

Ukiwa na four ya points 29 au zaidi huwezi kupata nafasi chuo kilichosajiliwa na NACTE. Utapata nafasi vyuo vya mtaani visivyotambulika, na elimu yako haitatambukika. Sasa jiulize Jesca ana four ya points 30 amesomaje Certificate kisha akaenda Diploma? Ina maana alikiuka utaratibu wa NACTE??

‪#‎Pili‬; hata kama Jesca alisoma Certificate (nje ya utaratibu) ilipaswa aanze certificate yake mwaka 2012 kisha amalize 2013 (mwaka mmoja). Then ajoin Diploma mwaka 2013 na kumaliza mwaka 2015 au 2016 (miaka miwili au mitatu kutegemeana na aina ya Diploma). NOTE: Hakuna Diploma ya mwaka mmoja inayotambulika na NACTE au TCU. Kwa hiyo tulitegemea Jesca aanze first year mwaka 2015 au mwaka huu mwezi wa 9.

Lakini cha ajabu mwaka huu mwezi wa 9 anaingia third year. Kasoma kwa utaratibu gani? Hili ndio swali la msingi ambalo wengi hawataki kulijibu. Hakuna anayeweza kujibu kwa usahihi zaidi ya kuweka siasa na kukwepa hoja. Jamani muogopeni MUNGU. Kwanini tunakua wanafiki hivi? Inaumiza sana mtu anapoamua kujitoa ufahamu kisa kosa limefanywa na mkubwa. Kwanini tunafanya double standars hivi?

Kwanini tunaogopa kusema ukweli kwamba kuna makosa yamefanyika kwa kuogopa kuwachukiza wakubwa? Mojawapo ya sifa ya msomi mzuri ni kuhoji. Sasa kwanini tunaogopa kuhoji utaratibu alioutumia Jesca kufika chuo kikuu?

Nani anaweza kuja hapa akaeleza utaratibu huo kwa ukweli na uwazi? Kwanini mkiambiwa mueleze taratibu hizo mnakimbilia kutukana na kutoa lugha za kuudhi?

Narudia tena kusema yupo MUNGU achunguzaye mioyo na nia zetu. Ipo siku atawalipa sawasawa na matendo yenu. Haiwezekani kijana aliyepata div.1 hadi 3 akarudishwa nyumbani eti atatafutiwa chuo kingine cha kwenda kusoma (sio UDOM) wakati kuna wenye div.4 wapo UDOM na wanasoma degree.!

Hawa watoto wa maskini waliokua wakisoma Diploma wameambia wasubiri kwanza maamuzi ya serikali. Lakini watoto wa vigogo wenye di ision four wanaendelea na masomo kama kawaida. Halafu kwa unafiki tunasimama na kuwatetea. Dhambi ni dhambi tu. Ifanywe na mkubwa au mdogo ni dhambi tu. Tujifunze kujadili mambo kwa kuweka utu mbele na si madaraka wa vyeo.

Kama kizazi chetu kitakua cha kuunga mkono yote yanayofanywa na viongozi kwa sababu tunaogopa kuwakosoa hata kama wamekosea, tutakua tumedhulumu pumzi ya mwenyezi Mungu tuliyopewa.

Kwanini hatusimami upande wa hawa vijana 7,802 waliofukuzwa kama mbwa UDOM. Tukavaa viatu vyao, tukashare maumivu yao japo kidogo. Tikawafariji na kuwatia moyo kwamba lipo tumaini?? Tuko busy kuwadhihaki watoto hawa wa maskini, huku tukiwatetea watoto wa vigogo wasio na sifa. Amin amin nawaambia JPM hataondoka madarakani kabla Mungu hajawalipa sawa na matendo yenu.

Namfahamu mtoto mmoja yatima aliyepata div.1 ya point 17 akaenda UDOM kusoma hiyo course maakumu ili amalize haraka apate kazi asaidie wadogo zake. Mpango wake ulikua awe daktari lakini maisha yakamfanya achague kwenda huko kwenye ualimu. Hana baba, hana mama. Aamelelewa na bibi yake ambaye sasa hivi ni kikongwe yeye na wadogo zake.

Pesa kidogo za "boom" alizokua anapata alituma kwa bibi ili wadogo zake nao waishi. Juzi kafukuzwa kama mbwa. Kwa kuwa tunafahamiana alinipigia simu nikamtumia fedha kidogo ya kumuwezesha kuishi pamoja na nauli. Kesho yake akaniambia Mchungaji wa kanisa akilokua akisali (TAG) akimtumia fedha nyingine kidogo za kumsaidia.

Hatimaye akafanikiwa kurudi kwa Arusha. Awakuta bibi na wadogo zake hajui hata cha kuwaambia. Maana yeye ndiye aliyekua tegemeo la familia. Yupo tu abasubiri hatma yake. Lakini jana akapata brief kdg kwamba JPM amesema wao ni "vilaza". Inauma,inauma, inauma. Nani asimame kutetea wanyonge hawa?? Nani aseme kwa niaba yao kama wote tupo busy kumtetea Jesca?? Mungu baba simama ukawatetee watu wako maana sisi tumepigwa na upofu wa kutetea wenye mamlaka tu hata wanapokosea.

Japo Rais kasema wenye sifa watatafutiwa vyuo vua kwenda lakini bado inaumiza. Inaumiza jinsi walivyofukuzwa chuoni kama mbwa. Inaumiza walivyotelekezwa mjini Dodoma bila hata nauli za kurudi kwao. Inaumiza kwa sababu hawajui watarudi lini hata kama wanazo sifa. Inaumiza kwa sababu wanazidi kupotezewa muda nyumbani wakati lengo lao lilikua kumaliza mapema wasaidie familia zao.

Lakini Rais pia kasema wenyevsifa HAWATARUDI UDOM badala yake watatafutiwa vyuo vingine vya kwenda ni hoja isiyoeleweka vzr. Kwanini wasirudi UDOM.? Je hoja ni kqa sababu ni form four? Yani hata kama mtu ana division 1 haruhusiwi kurudi UDOM kumalizia diploma yake? Mbona akina Jesca wa a division four na wapo hapohapo UDOM wanasoma degree? Bado suoni logic.!

Nimalizie tu kwa kusema hakuna dhambi mbaya kama unafiki. Kuogopa kukemea dhambi kwa sabanu dhambi hiyo imefanywa na mkubwa ni unafiki.Tujifunze kukemea hata kama aliyekosea ni kigogo. Mimi huwa siogopi kukemea kwa sababu najua Hakuna kigogo zaidi ya Mwenyezi Mungu.
Ikiwa nitskemea maovu na mtu/watu wakaamua kuniua au kunidhuru kwa sababu tu nimesema ukweli siogopi maana thawabu yangu ni kubwa mbinguni. Ili mradi sijamtukana mtu, wala sijatumia lugha ya kuudhi.

Nitaendelea kuhoji na kukemea dhsmbi wakati wote nitakapoona kuna haja ya kufanya hivyo. Nitahoji bila kuangalia cheo, wadhifa, umri, chama, dini, rangi wala kabila la ninayemhoji.
Albert Einstern aliwahi kusema "duniani pamekua mahali hatari zaidi pa kuishi, si kwa sababu ya kuwepo kwa watu waovu, bali kwa sababu ya kuwepo kwa watu wema lakini hawachukui hatua zozote dhidi ya uovu. Asomaye na afahamu.!

Malisa G.J
 
Matokeo ya kidato cha nne yametoka mwaka 2012 kwa waliofanya mwaka 2011.

Cheti kwa vigezo vya nacte ni mwaka mmoja,.
2012/2013 ilikua cheti.

Diploma kwa vigezo vya nacte ni miaka 2, 2013/2014 na 2014/2015..

2015 septemba au oktoba mwaka wa kwanza chuo kikuu, hapo nyuma tukichukulia kua hakurudia darasa au kuanguka kwenye masomo yake ya kuanzia cheti hadi diploma.

Kwa hiyo 2015/2016 mwaka wa kwanza. Yeye 2015/2016 yuko mwaka wa pili alisomaje?

Hii inakua kama ya siti mtemvu, wakati mwingine huwezi kubishana na ukweli labda uwe na dogmatic personality.
 
Nimeumia sana kwa ujumbe huu. Kauli za mkuu na halo halisi ya Jesca vitamtesa sana binti huyo na huenda akamlaani baba yake kwa kumuibulia fedheha mbele ya jamii. Mungu aepushe mbali lakini haya mambo yanaweza kumfanya binti akaamua kujidhuru kwa aibu na chuki za wenzake ambao yeye hajawakosea
 
Watoto wa maskini walipofukuzwa chuo kikuu japo wamefaulu vijana wa CCM walianzisha hashtag wakisema ‪#‎HatutakiVilazaVyuoVikuu‬. Leo vijana walewale wamegeuka na kuanza kumtetea "kilaza" aliyeachwa UDOM kisa tu kilaza huyo ni mtoto wa mkubwa. Unafiki, unafiki, unafiki usioelezeka. Hakuna dhambi kubwa kama kumnyanyasa mnyonge kwa sababu tu hana mtetezi.

Mtu anasimama kwa ujasiri eti Jesca alisoma certificate kisha Diploma, kabla ya kujiunga chuo kikuu. Huu ni uongo mkubwa na ni unafiki wa kiwango PhD kwa sababu zifuatazo;

‪#‎Mosi‬, Muongozo wa NACTE (NACTE Standard Operating Procedures, 2005) hauruhusiwi vyuo vilivyosajiliwa na NACTE kudahili wanafunzi wenye ufaulu chini ya division four points 28. Maana yake ni kuwa ili usome certificate itakayokuwezesha kusoma Diploma na hatimaye Degree ni lazima uwe na four isiyozidi ya points 28.

Ukiwa na four ya points 29 au zaidi huwezi kupata nafasi chuo kilichosajiliwa na NACTE. Utapata nafasi vyuo vya mtaani visivyotambulika, na elimu yako haitatambukika. Sasa jiulize Jesca ana four ya points 30 amesomaje Certificate kisha akaenda Diploma? Ina maana alikiuka utaratibu wa NACTE??

‪#‎Pili‬; hata kama Jesca alisoma Certificate (nje ya utaratibu) ilipaswa aanze certificate yake mwaka 2012 kisha amalize 2013 (mwaka mmoja). Then ajoin Diploma mwaka 2013 na kumaliza mwaka 2015 au 2016 (miaka miwili au mitatu kutegemeana na aina ya Diploma). NOTE: Hakuna Diploma ya mwaka mmoja inayotambulika na NACTE au TCU. Kwa hiyo tulitegemea Jesca aanze first year mwaka 2015 au mwaka huu mwezi wa 9.

Lakini cha ajabu mwaka huu mwezi wa 9 anaingia third year. Kasoma kwa utaratibu gani? Hili ndio swali la msingi ambalo wengi hawataki kulijibu. Hakuna anayeweza kujibu kwa usahihi zaidi ya kuweka siasa na kukwepa hoja. Jamani muogopeni MUNGU. Kwanini tunakua wanafiki hivi? Inaumiza sana mtu anapoamua kujitoa ufahamu kisa kosa limefanywa na mkubwa. Kwanini tunafanya double standars hivi?

Kwanini tunaogopa kusema ukweli kwamba kuna makosa yamefanyika kwa kuogopa kuwachukiza wakubwa? Mojawapo ya sifa ya msomi mzuri ni kuhoji. Sasa kwanini tunaogopa kuhoji utaratibu alioutumia Jesca kufika chuo kikuu?

Nani anaweza kuja hapa akaeleza utaratibu huo kwa ukweli na uwazi? Kwanini mkiambiwa mueleze taratibu hizo mnakimbilia kutukana na kutoa lugha za kuudhi?

Narudia tena kusema yupo MUNGU achunguzaye mioyo na nia zetu. Ipo siku atawalipa sawasawa na matendo yenu. Haiwezekani kijana aliyepata div.1 hadi 3 akarudishwa nyumbani eti atatafutiwa chuo kingine cha kwenda kusoma (sio UDOM) wakati kuna wenye div.4 wapo UDOM na wanasoma degree.!

Hawa watoto wa maskini waliokua wakisoma Diploma wameambia wasubiri kwanza maamuzi ya serikali. Lakini watoto wa vigogo wenye di ision four wanaendelea na masomo kama kawaida. Halafu kwa unafiki tunasimama na kuwatetea. Dhambi ni dhambi tu. Ifanywe na mkubwa au mdogo ni dhambi tu. Tujifunze kujadili mambo kwa kuweka utu mbele na si madaraka wa vyeo.

Kama kizazi chetu kitakua cha kuunga mkono yote yanayofanywa na viongozi kwa sababu tunaogopa kuwakosoa hata kama wamekosea, tutakua tumedhulumu pumzi ya mwenyezi Mungu tuliyopewa.

Kwanini hatusimami upande wa hawa vijana 7,802 waliofukuzwa kama mbwa UDOM. Tukavaa viatu vyao, tukashare maumivu yao japo kidogo. Tikawafariji na kuwatia moyo kwamba lipo tumaini?? Tuko busy kuwadhihaki watoto hawa wa maskini, huku tukiwatetea watoto wa vigogo wasio na sifa. Amin amin nawaambia JPM hataondoka madarakani kabla Mungu hajawalipa sawa na matendo yenu.

Namfahamu mtoto mmoja yatima aliyepata div.1 ya point 17 akaenda UDOM kusoma hiyo course maakumu ili amalize haraka apate kazi asaidie wadogo zake. Mpango wake ulikua awe daktari lakini maisha yakamfanya achague kwenda huko kwenye ualimu. Hana baba, hana mama. Aamelelewa na bibi yake ambaye sasa hivi ni kikongwe na anahitaji msaada japo anawalea wadogo zake.

Pesa kidogo za "boom" alizokua anapata alituma kwa bibi ili wadogo zake nao waishi. Juzi kafukuzwa kama mbwa. Kwa kuwa tunafahamiana alinipigia simu nikamtumia fedha kidogo ya kumuwezesha kuishi pamoja na nauli. Kesho yake akaniambia Mchungaji wa kanisa alilokua akisali (TAG) alimtumia fedha nyingine kidogo za kumsaidia.

Hatimaye akafanikiwa kurudi kwa Arusha. Awakuta bibi na wadogo zake hajui hata cha kuwaambia. Maana yeye ndiye aliyekua tegemeo la familia. Yupo tu abasubiri hatma yake. Lakini jana akapata brief kdg kwamba JPM amesema wao ni "vilaza". Inauma,inauma, inauma. Nani asimame kutetea wanyonge hawa?? Nani aseme kwa niaba yao kama wote tupo busy kumtetea Jesca?? Mungu baba simama ukawatetee watu wako maana sisi tumepigwa na upofu wa kutetea wenye mamlaka tu hata wanapokosea.

Japo Rais kasema wenye sifa watatafutiwa vyuo vua kwenda lakini bado inaumiza. Inaumiza jinsi walivyofukuzwa chuoni kama mbwa. Inaumiza walivyotelekezwa mjini Dodoma bila hata nauli za kurudi kwao. Inaumiza kwa sababu hawajui watarudi lini hata kama wanazo sifa. Inaumiza kwa sababu wanazidi kupotezewa muda nyumbani wakati lengo lao lilikua kumaliza mapema wasaidie familia zao.

Lakini Rais pia kasema wenyevsifa HAWATARUDI UDOM badala yake watatafutiwa vyuo vingine vya kwenda ni hoja isiyoeleweka vzr. Kwanini wasirudi UDOM.? Je hoja ni kqa sababu ni form four? Yani hata kama mtu ana division 1 haruhusiwi kurudi UDOM kumalizia diploma yake? Mbona akina Jesca wa a division four na wapo hapohapo UDOM wanasoma degree? Bado suoni logic.!

Nimalizie tu kwa kusema hakuna dhambi mbaya kama unafiki. Kuogopa kukemea dhambi kwa sabanu dhambi hiyo imefanywa na mkubwa ni unafiki.Tujifunze kukemea hata kama aliyekosea ni kigogo. Mimi huwa siogopi kukemea kwa sababu najua Hakuna kigogo zaidi ya Mwenyezi Mungu.

Ikiwa nitakemea maovu na mtu/watu wakaamua kuniua au kunidhuru kwa sababu tu nimesema ukweli siogopi maana thawabu yangu ni kubwa mbinguni. Ili mradi sijamtukana mtu, wala sijatumia lugha ya kuudhi.

Nitaendelea kuhoji na kukemea dhambi wakati wote nitakapoona kuna haja ya kufanya hivyo. Nitahoji bila kuangalia cheo, wadhifa, umri, chama, dini, rangi wala kabila la ninayemhoji.

Albert Einstern aliwahi kusema "duniani pamekua mahali hatari zaidi pa kuishi, si kwa sababu ya kuwepo kwa watu waovu, bali kwa sababu ya kuwepo kwa watu wema lakini hawachukui hatua zozote dhidi ya uovu. Asomaye na afahamu.!

Malisa G.J
 
Kiukweli lile gazeti la Uingereza lilikosea kidogo..for real mkuu wa nchi anaenda siko sasa, maamuzi yake yamekua ya ajabu ajabu kabisa.

Hili la Udom ndio sijamuelewa kabisa, awali nliamini Magufuli will be as smart as he started,kumbe hakuna kabisa. RAis wa nchi anawaambia askari kamateni gari toeni tairi mkauze???

Tunaokoelekea siko!!
 
mkuu hongera hakika unesema kweli tupu mkuki usiwe kwa nguruwe tu ila kwa binaadamu ukawa mchungu inawezekana vipi division 3 akaonekana kilaza lakini division 4 akaonekana amefaulu vyema
 
Pole, ktk maisha usilie lie namna hii, sisi sote wapitaji, huyo usiyemwogopa, mimi na wewe wote tutapita tu, hata uwe mwema kiasi gani au kuwa mdhambi kiasi gani, hakuna wa milele duniani! Jitahidi yako yanyooke huku ukipambana na changamoto za maisha! Punguza kulia!
 
Back
Top Bottom