ZILLAHENDER MPEMA
JF-Expert Member
- Apr 4, 2015
- 2,055
- 4,241
Kauli za namna hii zinaakisi kile alichokisema Sugu kuwa serikali inaongozwa kwa mizuka.Serikali inayosimamia mfumo wa Elimu unaozalisha vilaza haina na haiwezi kuwa na sababu za kuwanyanyapaa vijana wetu waliosoma kupitia mfumo wa serikali unaozalisha vilaza.
Ukilaza ni matokeo ya mfumo wetu wa Elimu ulioshindwa kutoa Elimu bora,badala yake umejikita katika kuongeza maelfu ya vijana wasio na sifa za kielimu.
Angalia matokeo ya kidato cha nne 2015, kisha tumuulize Rais,vilaza hao ni zao la nani kama si serikali yake mwenyewe?
Ikiwa wengi wa wanafunzi wanaomaliza secondary hufeli,nani anayepaswa kulaumiwa kwa matokeo hayo mabovu ya vijana wetu? Ukilaza ni matokeo ya Sera yetu ya Elimu iliyoshindwa kutatua changamoto za utoaji wa Elimu,hivyo anapotokea kiongozi Mwenye mamlaka ya kusimamia Sera,akaanza kutoa dhihaka kwa wananchi wake kwa kuwaita vilaza,kiongozi huyo anakuwa ni kielelezo cha viongozi kushindwa kutumia madaraka yao na dhamana zao kwa ajili ya Taifa letu.