endesha
JF-Expert Member
- Dec 9, 2015
- 1,190
- 1,644
Kwanza nitangulie kwa kusema kwamba Rais ni mtu mkubwa sana na pengine nadiriki hata kusema baada ya Mungu basi Rais ndio mwenye mamlaka ya kutoa maamuzi yoyote ndani ya nchi na hasa tukizungumzia nchi yetu hii pendwa.Kauli yoyote anayotoa Rais huchukuliwa kwa uzito wa hali ya juu.
Lakini nisikitike kwamba kwa siku za karibuni tumeona matamshi mbalimbali kutoka kwake ambayo naona hayaleti afya kwa mustakabali wa Taifa.
Ni mara kadhaa sasa tumesikia kwa kinywa chake mwenyewe akisema yeye ni Rais wa MASIKINI,lakini je hii ni nchi ya maskini peke yao?Je alichaguliwa na masikini peke yao? .pia tumekua tukisikia akisema atawashusha matajiri walio kama malaika waishi kama mashetani.Ni hatua nzuri lakini Bado naona sio lugha nzuri kwa mtu mwenye mamlaka ya juu.
Unaweza kujaza kitabu kauli zilizo na utata lakini huwezi kuziacha mbili za jana kwamba gari litakalokamatwa lingolewe matairi yauzwe.Hivi kwa Polisi wetu hawa waliozoea kutumia mabavu ,kauli hii si kubariki uchukuaji wa sheria mkononi??
Lakini lingine ni hili la kusema watoto wenye Division 4 ni VILAZA.Hivi kweli kama baba,unaweza kumtolea mtoto wako kauli kama hiyo ilihali unajua mazingira aliyopitia mwanao?.Hivi huyu mtoto wako unategemea atakuchukuliaje kama mzazi?Ni ukweli usiopingika kwamba zaidi ya 80 asilimia hupata daraja la 3 hadi 0 kila mwaka.Je wote ni VILAZA?Kama ndiyo ni kauli nzuri kama mzazi?
Mh. Rais ajaribu kuchuja baadhi ya maneno ya kuongea na public ,kwani maneno mengine hugawa watu na pengine kukosa imani naye.Yeye ni Rais wa wote MATAJIRI,MASKINI,,wenye DIV I,II,III,IV na hata 0.

Kuna ukweli ambao baadhi yetu pengine kwa mapenzi yasiyo vipimo huwa tuna kawaida ya kupinga kila jambo. Pamoja na kuwa kila binadamu ana kasoro zake lakini kwa kiasi fulani unatakiwa kuficha sana udhaifu huo hasa unapokuwa kiongozi mkuu.
Rais wetu JPM ni mmoja wao. Mimi nadhani ana tatizo la kuongea hasa hadharani. Tulisema pale mwanzo pengine ni uwana genzi lakini kadiri siku zinavyosogea hali haibadiliki. Masuali yalikuwa mengi kwa nini Rais kila anapotoa hutuba lazima kuwe na manunguniko ? Manunguniko nilidhani pengine ni kwa hutuba zile za kutumbuwa na ufisadi mwanzo niliamini itakuwa wanaolalamika wameguswa tu hapana. Kumbe hata makundi mengine.
Mifano iko mingi. Angalau tutazame hii miwili ya karibuni. Wakati wa ziara yake ya kushukuru kwa kuchaguliwa kule Zanzibar, aliacha sintofahamu na kuwagawa watu. Alitegemewa kama kiongozi mkuu wa nchi kwa yaliyotokea Zanzibar atumie lugha za kupoza watu na kuwafariji lakini haikuwa hivyo maneno haya "fyoko fyoko" " kuuza tungule" na kwa ujumla hutuba ile iliowakera wengi.
Jamii ilitegemea atoe neno la kuwaunganisha watu hakufanya sikwambii kupuuzia mgogoro wenyewe wa Zanzibar.
Wa pili ni huu wa juzi wa Bukoba. Licha ya serikali yake kulaumiwa kwa ilivyolishughulikia tatizo la tetemeko la bukoba na kuchelewa kufika kuwafariji haikutosha. Katumia hutuba yenye ukaklasi na inayokwaza wengi. Hutuba ilikosa matumaini.
Mifano ni mingi mimi nimetoa hiyo miwili. Rais ni kiongozi mkuu wa nchi na ni tumaini popote. Ziara za Rais hasa sehemu zenye matatizo huwa zinavuta hisia za kupata faraja lakini kwa muda huu mfupi wa Rais wetu, hili linaelekea kuwa donda sugu.
Mimi nafikiri Rais JPM ana matatizo binafsi ya kuongea. Na nafikiri ni vyema angesaidiwa kabla madhara zaidi ya kijamii hayajaongezeka.
Unaweza ukajiuliza hivi huwa hajuwi madhara ya kauli zake ? Lakini nini kifanyike ? wasaidizi wake wako wapi na wanafanya nini kumsaidia kuondowa tatizo hili ?
Kuna nini huko kiasi cha kila hutuba yake kulalamikiwa hata ikiwa si hizo za kunyoosha nchi kama anavyosema mwenyewe kwa nini ?
Kwa mtiririko huo, ni maoni yangu kwamba Rais JPM kuna tatizo linamsumbuwa tena inawezekana limeshakuwa sugu.
Kishada