Kauli za Rais Magufuli jinsi zinavokingamana kuhusu suala la Zanzibar

wamisako

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
917
871
November 20,2015 "Kwa kushirikiana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na wadau wa siasa hususan vyama vya CUF na CCM tutahakikisha kua majaribu ya kisiasa yanayoikabili zanzibar yanamalizika kwa salama na amani" Feb 13,2016 "Naheshimu sheria, ZEC ina uhuru wa kuamua mambo yake hiwezi kuingiliwa na yeyote.

Kama kuna mtu anataka tafsiri ya sheria aende MAHAKAMANI, mahakama ipo hutaki kwenda halafu unamwambia MAGUFULI ingilia, siingilii na nitaendelea kukaa kimya"
Chanzo: Tanzania Daima
 
kama anaamini maamuzi ya ZEC yanaweza kuhojiwa mahakamani basi kumbe inawezekana kuhoji ushindi wake mahakamani.Ingawa kisheria sijuwi kama ipo hivyo
 
Haya ukawa mepigwa doro sasa, mlikua mnapiga makelele kila saa magufuli ingilia kati haya mheshimiwa kafunguka
 
ZEC wameshatangaza tarehe ya uchaguzi. CUF wameweka mpira kwapani. Wewe unatakaje sasa?
 
Nyie leteni dhihaka tu lakini linalofinyangwa Zenji litamliza kila mtu tena kwa miaka!
 
Kauli zake zimekingamana kivipi?

Sema tafsiri zetu haziendani na maana ya kauli za Rais Magufuli.

Mlitaka afanye kama mnavyofikiria ninyi?

Majadiliano yalikuwa yanaendelea kati ya serikali ya Mapinduzi na wadau wa siasa lakini Maalim Seif akaamua kwa mbwembwe kujitoa ili atingishe kiberiti.

Baada ya kugundua kiberiti kimejaa njiti, kwa sasa anaomba tena majadiliano yaendelee!
 
Back
Top Bottom