Kauli za kipuuzi za viongozi wa kisiasa dhidi ya vyombo vya dini zinapaswa zipingwe vikali

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
KAULI ZA KIPUUZI ZA VIONGOZI WA KISIASA DHIDI YA VYOMBO ZA DINI ZINAPASWA ZIPINGWE VIKALI

Na: Shujaa Charles Richard Mwaisemba (CRM)

Kwa muda mrefu sasa imeanza kuzoeleka na kuonekana ni desturi kwa viongozi wa kisiasa hasa hawa Ma-DC na RC(Wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa) kutoa kauli za kipuuzi na matamko yenye ukakasi na yasiyofuata misingi ya kisheria kwa kutumia mamlaka zao vibaya kuamrisha matamko yao yafautwe na kutekelezwa kama walivyoyasema

Lakini cha kushangaza kutokana na ujinga wa watanzania walio wengi kwa kutokujua haki za kisheria, bado kumeendelea kuwepo na watu wanatetemeka na kushabikia kauli hizo za kipuuzi za Viongozi hao wa kisiasa.Mfano Majuzi hapa amesimama mkuu wa wilaya ya Ilala,Mhe Sophia Mjema

“Kuna watu wanapiga mapambio Jumatatu mpaka jumatatu, Ukiingia huko ndani watu 5, wewe j3 mpaka j3 unaita watu, huna watu ,funga!” Anaendelea kusema “Tunajua sisi katika kuomba ni mara hizi 3, yaani ijumaa (Waislam), Jumamosi(Wasabato) na Jumapili(Wakristo wengine).HIZI SIKU NYINGINE HAKUNA MARUFUKU, Ninyi kazi mnafanya saa ngapi, Jumatatu hadi Jumatatu, “

DC huyu SOPHIA MJEMA aliendelea kukazia kuwa siku za kusali na kufungulia spika anazozitambua lazima ziwe hizo siku 2 yaani jumamosi na Jumapili kwa wakristo, Hivyo akamalizia kumpatia afisa utamaduni kuyafanyia kazi

Viongozi wa namna hii wasiojua sheria inapaswa wote wafukuzwe mara moja, Ni sheria ipi inayosema siku ya mtu kumuabudu Mungu wake ni ijumaa, jumamosi na Jumapili tu?Wewe mpagani, usiyejua hata sheria za nchi, Utafundisha watu wamuabudu Mungu ni muda gani na siku gani za kusali? Nani kakwambia Mungu anaabududiwa ijumaa, jumamosi au Jumapili? Au ni kwa sheria zako za kipagani?

Unatufundisha wakristo tusali eti jumamosi na jumapili? Kama hujui sheria za katiba yetu inayotupa uhuru wa kuabudu basi usizungumze sheria za ukristo usizozijua.Sheria ya wakristo ya kumwabudu Mungu ni siku zote na hata akichagua siku Fulani ni ya kuadhimisha tu {WARUMI 14:5-6 “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. 14.6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.”}

Kwa mfano Waislam wanaoswali swala tano, Je ni kwamba ni watu ambao hawafanyi kazi? Kila mtu anasisitizwa kufanya kazi kwa wakati wake ili apate kula,Maana kutokufanya kazi hata kwenye maneno ya Mungu ni dhambi.Na kila mtu ana muda wake wa kazi wengine asubuhi wengine usiku, hata hao unaodai wa wachungaji wanaofanya ibada jumatatu hadi jumatatu kazi zao ni hizo hizo za kuwasaidia watu wenye mateso na kuonewa wanaitwa watumishi wa Mungu kama wewe ulivyo mtumishi wa serikali.

Kupiga marufuku watu kusali katikati ya wiki pale wapatapo muda ni kuingilia uhuru wa kuabudu tuliopewa na katiba yetu ya jamuhuri wa muungano “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, KAZI YA KUTANGAZA DINI, KUFANYA IBADA NA KUENEZA DINI ITAKUWA NI HURU NA JAMBO LA HIARI YA MTU BINAFSI; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za Mamlaka ya nchi”. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo: sheria ya 1984 Number 15, ib. 6

Kwahiyo Mtumishi wa serikali unapoanza kuingilia uhuru wa watu kuabudu na kuwapangia muda na siku za kusali unasababisha hatari kubwa na hata unaweza kutowesha amani ya nchi pale kauli za namna hii za kichochezi zinapozungumzwa bila kufuata misingi ya kisheria.

Mpaka hapa ninapozungumza nina ushahidi wa makanisa mengi kupigwa marufuku si tu kuabudu kwenye mikesha, Vyombo kuzuiwa kupigwa na kutumika wakati wa ibada na mbaya zaidi vyombo vya dola yaani polisi wameshaanza kuingilia ibada za watu siku kati kati ya wiki hata jumapili kuzuia wasifanye ibada kwa madai kuwa ni kelele kwa wananchi wanaowazunguka.Jambo hili likinyamaziwa hivi ni hatari kwa nchi na linaweza kuzusha machafuko makubwa kwa kuingilia uhuru wa vyombo vya dini

Ikiwa serikali itaanza kunyamazia kauli za kipuuzi za viongozi kama hawa itafanya watu kuanza kuhoji, Mbona Misikiti kila siku usiku kunakuwepo na azana ambazo zinawatoa watu usingizini hata wasiohusika, Mbona yapo mabaa yanapiga kelele usiku kuchwa na zaidi watu wataanza kuhoji kwanini mnaingilia uhuru wa mtu kuabudu na kuzuia watu kufanya ibada zao isipokuwa siku mnazowapangia wao?Nani kakwambia nchi hii ni ya wakristo na waislam? Wapagani je wasali lini?

Ikiwa Serikali inaona matatizo yanayotokana na hicho kinachoitwa kelele za makanisa, misikiti au mabaa basi serikali itenge maeneo maalum ya majengo hayo ambayo yapo mbali na maeneo ya makazi ya watu, sio kuwapa uhuru kujenga katikati ya makazi ya watu alafu unaanza kuwazuia na kuwapangia siku za kufanya ibada na siku za kukutana na kuwazuia kutumia vyombo vya mziki vinavyoelekezwa Kulingana na imani zao.Serikali inaweza kushauri wapunguze sauti za vyombo vyao ila si kutuma mapolisi kuingilia mikesha na kuzuia watu kufanya ibada.Ikiwa wanataka hizo kauli zao zifanyiwe kazi basi wapeleleke mswada bungeni kupitisha kuondoa sheria ya sasa ya uhuru wa kuabudu kuliko kutumia mamlaka zenu kupiga marufuku kwa mambo yaliyo nje ya katiba za nchi yetu.
 
Mkuu sasa kubali siku za kazi hizo kazi zitafanyikaje? Utaratibu wa kusali hizo siku 3 kwa maana ijumaa kwa waisilamu ,jumamosi na jumapili kwa wakristo ulizingatia na siku za kazi kwa mujibu wa Katiba ya Nchi,tafadhali tiini mamlaka zilizowekwa na Mungu
 
Sasa mkuu nyinyi mashahidi wa Yehova mkubali tu siku ya ibada kwa hizo siku 3. Hata hivyo serikali ilichokataza ni makelele ya spika mitaani. Sidhani kama ukiondoa waislamu na walokole kuna madhehebu mengine yanayoendesha ibada kila siku na kwa sauti kubwa. DC amazungumza mambo ya kisheria kwani walokole wameweka nyumba za ibada hadi kwenye makazi ya watu na makelele usiku mzima. Kwa mujibu wa sheria za mitaa ni kosa. Watu wanalalamika wanakosa utulivu na usingizi. Walokole wasali tu polepole kwani Mungu sikio lake sio zito atawasikia.
 
Kiongozi Ukianza kuingilia mambo ya imani jiandae kupata tabu sana

Huu ni upuuzi, dini zinapumbaza sana watu, watu mmekuwa na imani kwamba suala la dini ni untouchable! Nani kakwambia? yaani watupigie kelele kutwa nzima usiku kucha watoto washindwe kufanya homework kisa wewe unasali? ujinga gani? hatuwezi kukubali, hakuna anayekatazwa kusali hata wakatoliki wana misa ya kila siku asubuhi lakini hawajawahi kuwa kelo, wanapiga kengele kwa dakika moja wanasali kimya na mungu wao. Sasa hawa ambao wana mungu ambaye ili awasikie lazima watuwekee spika huyo mungu wao ni questionable! Let us go back to the drawing board and use our common senses.
 
Hizo speaker zinapiga kelele au wanaweke nyimbo za kumsifu Mungu?
Je, ni Mungu yupi ambaye anakataza kumsifu?
Mungu anasema msifuni Mungu kwa vinada, vunumbi nk, Je, hivyo vinanda vitasikika vipi bila speaker?
Usitake kutumika na shetani kwa kusema wanaomsifu Mungu wanapiga kelele.
Mihemko katika jambo ni baya sana.
Mbona waislamu wanapiga sijui wanaita zana lakini hakuna hata mmoja aliyesema wanapiga kelele. Mana hiyo ndio imani yao.
Yaani ka wewe kusikia nyumbo za kumsifu Mungu unasema ni kelele basi unamatatizo.
 
Sasa mkuu nyinyi mashahidi wa Yehova mkubali tu siku ya ibada kwa hizo siku 3. Hata hivyo serikali ilichokataza ni makelele ya spika mitaani. Sidhani kama ukiondoa waislamu na walokole kuna madhehebu mengine yanayoendesha ibada kila siku na kwa sauti kubwa. DC amazungumza mambo ya kisheria kwani walokole wameweka nyumba za ibada hadi kwenye makazi ya watu na makelele usiku mzima. Kwa mujibu wa sheria za mitaa ni kosa. Watu wanalalamika wanakosa utulivu na usingizi. Walokole wasali tu polepole kwani Mungu sikio lake sio zito atawasikia.
Kwa hiyo unataka kusema hata hao waislamu itafika muda wazuiwe kufanya adhana kwa kuwa kwangu mimi adhana ya saa kumi na moja asubuhi, saa saba mchana, saa tisa, saa kumi na mbili na saa mbili ni kero kwangu! Saa kumi na moja asubuhi nakuwa nimestarehe na mke wangu mara kelele za adhana! Saa saba mchana nakuwa nakula ; mara adhana, saa tisa nakuwa napata siesta; mara adhana; saa kumi na mbili nakuwa mazoezini; mara ashana, saa mbili usiku naongea na wanangu; mara adhana!!!
 
Hizo speaker zinapiga kelele au wanaweke nyimbo za kumsifu Mungu?
Je, ni Mungu yupi ambaye anakataza kumsifu?
Mungu anasema msifuni Mungu kwa vinada, vunumbi nk, Je, hivyo vinanda vitasikika vipi bila speaker?
Usitake kutumika na shetani kwa kusema wanaomsifu Mungu wanapiga kelele.
Mihemko katika jambo ni baya sana.
Mbona waislamu wanapiga sijui wanaita zana lakini hakuna hata mmoja aliyesema wanapiga kelele. Mana hiyo ndio imani yao.
Yaani ka wewe kusikia nyumbo za kumsifu Mungu unasema ni kelele basi unamatatizo.

Tanzania haina dini, ila watu wake wana dini. Just use your common sense, kwa nini usalishe wasiohusika kisa wewe unamuomba mungu wako? Wasio na dini nao je unawasalisha kwa nini? Nchi ni yetu wote wenye dini na wasio na dini muislamu aliyeko pembeni kwa nini umsalishe na mapambio yako?. Na je kila mmoja akiweka speaker kufanya maombi hiyo nchi itakalika? Hoja ya waislamu kwamba wanaweka azana haina mashiko kwa kuwa huwa wanaweka muda mfupi baadae wanaacha wanaendelea na ibada katika tolerable sound, The same applies to Catholics wanapiga kengele muda mfupi wanaendelea na ibada bila kelo na hii ni kila siku asubuhi.
 
Back
Top Bottom