Kauli ya Zitto kuhusu yaliyotokea Arusha

Dear Zitto Kabwe!
I like the way you responded on what happened in Arusha. I real don't understand why Police are using such forces unnecessary. I propose you guys (CHADEMA) especially Zito to take positive action againts the IGP, and other officers.

Lastly, kindly bell out all 41 peoples
Good one Zitto hongera...

... hebu turudi kule PPF tugawane zile pesa ulizofaidi:hat:
 
Kuna mtu kanisms kuwa wabunge waliokuwa Arusha ni watu wa kaskazini tu je, hili linaukweli? Zitto kwa nini mara kadhaa ukosekana kwenye matukio ya Chadema yanayogusa isia za watu wengi?

mmh I cant see how relevant is this? Kwani hujasoma kuwa Zitto alikuwa Mwanza kuhamasisha ushindi wa Chadema katika uchaguzi wa Meya? Je ulitaka viongozi wote wa Chadema wawe Arusha? Vipi shughuli zingine za chama maeneo mengine ya Tanzania ulitaka zisimame?

Mi naamini ni mgawanyo wa majukumu tu!! Labda kama utathibitisha bila shaka yoyote kwamba chama kilitoa mwongozo kuwa viongozi wote kuanzia ngazi fulani wawe Arusha kwa ajiri ya maandamano, hapo tunaweza tukaijadili hii hoja!
 
Ndugu zangu,
Tunalaani matumizi ya ovyo ya nguvu za dola
Kwa mara nyingine tena, jana Jumatatu tarehe 05 Januari 2010, Jeshi la Polisi lilivuruga na kusambaratisha mkutano halali wa hadhara uliondaliwa na chama halali cha siasa jijini Arusha. Katika kuvuruga na kusambaratisha mkutano huu, jeshi la polisi liliua na kuwaumiza vibaya baadhi ya wananchi. Miongoni mwa wananchi walioumizwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe, mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema na mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA mama Josephine Slaa. Wengi wa wananchi walioumizwa ni watoto na akina mama. Kama vile haitoshi, Jeshi la Polisi kwa ubabe na ukatili wa hali ya juu, liliwafuata na kuwakamata Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe Dk Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini Mhe Philemon Ndesamburo wakiwa katika Hoteli ya Mount Meru. Wabunge hawa wamedhalilishwa na jeshi la polisi bila kujali kinga ya bunge walio nayo.

Tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi ya ovyo ya vyombo vya dola. Tunalaani Jeshi la Polisi kuendelea kukubali kutumiwa na wanasiasa katika kuficha udhaifu wao wa kisiasa na kiuongozi. Serikali hii imeshindwa kudhibiti ujambazi nchini kwa kisingizio kuwa haina askari na vifaa vya kutosha, lakini wana askari kedekede na vifaa lukuki vya kudhibiti na kuua wananchi wasio na hatia kwa sababu tu wanaonyesha mapenzi yao kwa vyama vya upinzani badala ya chama tawala. Jeshi la Polisi limeendelea kuvunja sheria kwa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani. Badala ya kutoa ulinzi katika mikutano ya hadhara, jeshi la polisi limegeuka kuwa watoa vibali!

Watawala na jeshi la polisi watambue kuwa hakuna nguvu ya risasi itakayoshinda nguvu ya umma inayotaka mabadiliko, na wala CCM haitaweza kulazimisha kubaki madarakani kwa nguvu ya risasi. CHADEMA tutaendelea na juhudi za kuhamasisha wananchi kudai haki zao za kidemokrasia, ikiwemo kuwajibisha viongozi waliowachagua kuwaletea maendeleo. Matumizi mabovu ya nguvu za dola kunakofanywa na watawala wa CCM ni ushahidi mwingine muhimu wa kwa nini tunahitaji Katiba Mpya kwa haraka iwezekanavyo.

Katika kipindi hiki kigumu, tukiendelea na juhudi za kuwatoa nje viongozi waliowekwa ndani kwa udhalimu, ninawaomba wananchi, wapenzi na wanachama wa CHADEMA wawe wastahimilivu na waendelee na shughuli zao. CHADEMA tutahakikisha haki inatendeka na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya askari waliosababisha maafa yaliyotokea.

Zitto Zuberi Kabwe (Mb)
Naibu Katibu Mkuu (Bara)-CHADEMA
Nimetoa kauli hii Mwanza saa 1300hrs

Hongera Zitto. Mapambano yanaendelea hadi kieleweke
 
Kuna mtu kanisms kuwa wabunge waliokuwa Arusha ni watu wa kaskazini tu je, hili linaukweli? Zitto kwa nini mara kadhaa ukosekana kwenye matukio ya Chadema yanayogusa isia za watu wengi?

Kwani hujui chama chetu kirefu chake ni CHAGGAS DEVELOPMENT MANIFESTO (CHADEMA)
 
oK, KAMA YUKO MWANZA SAWA MAANA LAZIMA ILIBIDI MTU AWEPO PALE KUSIMAMIA UCHAGUZI, NA NASIKIA CDM WAMASHINDA
 
kwa pa1 2tashnda,milele nguvu ya umma haishindwi,mapambano daima mpaka kieleweke,gud boy Zitto,,frm nw police mpaka viongoz wa ccm hatakaa kwa aman,kikwete hi nchi c yako na shemej zako,ckuombei upotee,ili uone tz mpya after 2015,huwez niziba mdomo,ntasema mpaka naingia kaburin,nadhan utakua rais wa kwanza Tz kuleta vita,iliwa hvyo ujue ,hutapotea peke ako na kizaz chako chote
 
atleast Zitto ametoa statement i was worried mbona yupo kimya kiasi hicho?kama yupo kweli yupo mwanza hongera kwa kufanikisha ushindi wa meya
 
But wachangiaji wengine wametutaarif kuwa alikuwa mwanza anaamasisha ushindi wa umeya
 
zitto Mungu akubariki uwe nasi katika majonzi na ukombozi wa taifa letu ambalo linatawaliwa kwa sasa na shetani kama nilivyowahi kuandika. watu wamejibatiza kuwa wao ni Mungu hali wanaishi na kupumua kama sisi. kama vile haitoshi sasa wanachukua madaraka ya kutoa uhai wa watu wengine kwa kuwa wao ni Mungu. tumeshuhudia kikwete akiitwa Mungu Baba huko sumbawanga na sasa mungu baba kikwete amemwaga damu za watu, ulaaniwe wewe na kizazi chako chote.MUNGU wetu aliye mkuu ataunyanyua mkono wake dhidi yako , na kama alivyomangamiza farao na jeshi alko we we na we hauko salama
 
Back
Top Bottom