Kauli ya Zitto kuhusu yaliyotokea Arusha

Kauli ya Zitto kuhusu yaliyotokea Arusha

kiraia

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Posts
1,717
Reaction score
1,012
Ndugu wana JF,

Tangu Raia wema wa Arusha waanze kudai haki yao jana asubuhi na kupelekea viongozi kadhaa wa juu wa chama hicho kuswekwa ndani sijamsikia Zitto Kabwe akiongea chochote, je yuko nchini au bado anasheherekea sikuku za christmass na Mwaka mpya?

==============

UPDATES:

baada ya Kuuliza Zito yu wapi amekuja na tamko hili hapa Chini kama alivyolileta Don Cicci (JF Member)
Ndugu zangu,

Tunalaani matumizi ya ovyo ya nguvu za dola

Kwa mara nyingine tena, jana Jumatatu tarehe 05 Januari 2010, Jeshi la Polisi lilivuruga na kusambaratisha mkutano halali wa hadhara uliondaliwa na chama halali cha siasa jijini Arusha. Katika kuvuruga na kusambaratisha mkutano huu, jeshi la polisi liliua na kuwaumiza vibaya baadhi ya wananchi. Miongoni mwa wananchi walioumizwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe, mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema na mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA mama Josephine Slaa. Wengi wa wananchi walioumizwa ni watoto na akina mama. Kama vile haitoshi, Jeshi la Polisi kwa ubabe na ukatili wa hali ya juu, liliwafuata na kuwakamata Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe Dk Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini Mhe Philemon Ndesamburo wakiwa katika Hoteli ya Mount Meru. Wabunge hawa wamedhalilishwa na jeshi la polisi bila kujali kinga ya bunge walio nayo.

Tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi ya ovyo ya vyombo vya dola. Tunalaani Jeshi la Polisi kuendelea kukubali kutumiwa na wanasiasa katika kuficha udhaifu wao wa kisiasa na kiuongozi. Serikali hii imeshindwa kudhibiti ujambazi nchini kwa kisingizio kuwa haina askari na vifaa vya kutosha, lakini wana askari kedekede na vifaa lukuki vya kudhibiti na kuua wananchi wasio na hatia kwa sababu tu wanaonyesha mapenzi yao kwa vyama vya upinzani badala ya chama tawala. Jeshi la Polisi limeendelea kuvunja sheria kwa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani. Badala ya kutoa ulinzi katika mikutano ya hadhara, jeshi la polisi limegeuka kuwa watoa vibali!

Watawala na jeshi la polisi watambue kuwa hakuna nguvu ya risasi itakayoshinda nguvu ya umma inayotaka mabadiliko, na wala CCM haitaweza kulazimisha kubaki madarakani kwa nguvu ya risasi. CHADEMA tutaendelea na juhudi za kuhamasisha wananchi kudai haki zao za kidemokrasia, ikiwemo kuwajibisha viongozi waliowachagua kuwaletea maendeleo. Matumizi mabovu ya nguvu za dola kunakofanywa na watawala wa CCM ni ushahidi mwingine muhimu wa kwa nini tunahitaji Katiba Mpya kwa haraka iwezekanavyo.

Katika kipindi hiki kigumu, tukiendelea na juhudi za kuwatoa nje viongozi waliowekwa ndani kwa udhalimu, ninawaomba wananchi, wapenzi na wanachama wa CHADEMA wawe wastahimilivu na waendelee na shughuli zao. CHADEMA tutahakikisha haki inatendeka na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya askari waliosababisha maafa yaliyotokea.

Zitto Zuberi Kabwe (Mb)
Naibu Katibu Mkuu (Bara)-CHADEMA
Nimetoa kauli hii Mwanza saa 1300hrs
 
Aliongea na BBC leo asubuhi. Labda ulikuwa bado umelala.
 
Mwacheni huyu ndumila kuwili asitupotezee muda wetu!........nina uhakika atakuwa anatumia kale kahela ka wafisadi na kale anakolipwa kuifanyiua ccm intelijensia...mwacheni ale raha\...tumesema hatuna imani naye na hatumtaki ahamie rasmi ccm kwani yeye ni ccm damu
 
wanajamii mimi nashangaa badala tujadiliane watu kama akina mnyika, Wenje, Halima wako wapi tunaulizana habari za zitto. Zitto is an outdated story. Mnampa umaarufu wa bure kumjadili hapa. Tunapoteza muda. Labda ametumwa na rostam malasia kuchukua mzigo. Nasikia wanafanya biashara pamoja siku hizi.
 
Ameongea nini? hata mimi nilikuwa nimelala

Kuwa wafuasi wa chadema watulie wakati wakifanya mpango wa kuwatoa viongozi kwa dhamana. Pia aligusia suala la haki ya kila mtanzania, chama chochote kuandamana.
 
Zitto Tweeting at 40 minutes ago: "Nipo Mwanza...Tumeshinda Umeya Mwanza kwa kura 17 kwa 15...updates za Arusha nitazirusha hewani"
 
Zitto Tweeting at 10 minutes ago: "Kama kuna vitendo vya uhalifu vishughulikiwe hivyo na si vinginevyo"
 
Ndugu wana JF,

Tangu Raia wema wa Arusha waanze kudai haki yao jana asubuhi na kupelekea viongozi kadhaa wa juu wa chama hicho kuswekwa ndani sijamsikia Zitto Kabwe akiongea chochote, je yuko nchini au bado anasheherekea sikuku za christmass na Mwaka mpya?


Hii ni kutoka kwenye Facebook yake:
Zitto Kabwe
Nipo Mwanza...Tumeshinda Umeya Mwanza kwa kura 17 kwa 15....naendelea kuwasiliana na viongozi wetu Arusha nitawapa updates..naomba subira...It is now official we run 6 cities and municipalities in Tanzania-ukerewe,Karatu, Moshi, Musoma, Mwanza and Kigoma. Bdo Arusha
 
Tatizo zitto kajiongezea sana maadui, viongozi wa cdm si wote walikuwa arusha, kuna akina lwakatale, silinde walikuwa mbeya na shughuli maalum. Asante zitto kwa taarifa ila tunaoomba tu muwahi arusha kuongeza nguvu watoke viongozi wetu mapema. Niko natokea mwanza na pale jioni walianza kuhofu ya arusha kutokea. Hata hii thread aliyeanzisha ni kumsakama zito kuna wana sheria akina tundu lissu wanasughulikia mambo haya
 
Zitto Kabwe tweeting 20 minutes ago "Tunachotaka ni Viongozi wetu wote waachiliwe pasipo masharti;serikali ichukue hatua dhidi ya Polisi waliotumia nguvu kiasi hicho"
 
Tatizo zitto kajiongezea sana maadui, viongozi wa cdm si wote walikuwa arusha, kuna akina lwakatale, silinde walikuwa mbeya na shughuli maalum. Asante zitto kwa taarifa ila tunaoomba tu muwahi arusha kuongeza nguvu watoke viongozi wetu mapema. Niko natokea mwanza na pale jioni walianza kuhofu ya arusha kutokea. Hata hii thread aliyeanzisha ni kumsakama zito kuna wana sheria akina tundu lissu wanasughulikia mambo haya

Inavyoonekana Zitto alikuwa Mwanza kusimamia huo uchaguzi.
 
Ziito zitoooo Zittozitoooo

Acheni kufanya Siasa jukwaaa la taarabu.

Mbona hujauliza viongozi wengine wako wapi ?
Una share na zitto? .......Una Kisas na zitto?......Zitto kateka ubongo wako?............
 
mchekini facebook na twiter huko mitaani kwenye fujo hamtamuona ng'ooooo...........huyo ndo zitto bwaana
 
Back
Top Bottom