Kauli ya Rais imevunja Katiba; kwa kuingilia uhuru wa Mahakama

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,981
45,903
Napenda kusema wazi kabisa kua Rais wetu alishauriwa vibaya, na waliomshauri wamemweka katika kikaango na wadau wa sekta ya sheria.

Hii ni kutokana na kauli aliyoitoa jana katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani au " Law day" pale aliposema kwamba kuna kesi zaidi ya 400 zilizopo mahakamani ambazo kama zikiendeshwa ipasavyo basi serikali inaweza kujipatia kiasi cha shilingi trilioni moja kama fidia toka wa wadaawa, ambazo ameahidi kuwapatia mahakama kiasi cha shilingi bilioni mia mbili.

Kuna mambo machache ya kuangalia hapa ;

1. Ni hakimu gani au jaji atakayekua tayari kutoa hukumu dhidi ya serikali.

2. Ni wakili gani anapoteza muda wake kwenda mahakamani wakati anajua kua mteja wake anakwenda kushindwa.

3. Vipi kuhusiana na uhuru wa mahakama kufanya kazi yake bila kuingiliwa.

4. Vipi kuhusiana na haki ya mtuhumiwa kuwa hana hatia mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani.

5. Ina maana serikali itashinda kesi zote 400??

Napenda nikumbushe kwamba mashauri yakishafikishwa mahakamani mambo hua yanaendeshwa kwa taratibu, kanuni na sheria ambazo tayari zipo, hayaendeshwi kwa kauli za kisiasa, huko ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Kauli ya Rais ukiitazama kwa kina utaona kwamba imevunja ibara ywa 13 (6) (a) na 107B ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977, nanukuu;

Equality before the law 13.-(1) All persons are equal before the law and are entitled, without any discrimination, to protection and equality before the law.

(6) To ensure equality before the law, the state authority shall make procedures which are appropriate or which take into account the following principles, namely: (a) when the rights and duties of any person are being determined by the court or any other agency, that person shall be entitled to a fair hearing and to the right of appeal or other legal remedy against the decision of the court or of the other agency concerned;

Independence of the Judiciary 107B. In exercising the powers of dispensing justice, all courts shall have freedom and shall be required only to observe the provisions of the Constitution and those of the laws of the land.

Ukipitia ibara zote mbili, utaona kwamba kwa kauli ya Rais, majaji na mahakimu hawatakua katika hali ya uhuru wa kufanya kazi zao kwani hawatataka kwenda kinyume na maagizo ya rais ambayo yanaelekeza makusanyo ya trilioni moja.

Vile vile haki ya wadaiwa itakua imevunjwa maana mpaka sasa wanachukuliwa kua tayari ni wakosaji wakati mashauri bado hayajamalizika na mahakama kufikia maamuzi yake.

Jambo la msingi kabisa la kufanyika hapa ni kwa Rais, kuiondoa kauli ile kwani kwa kiasi kikubwa italeta usumbufu mkubwa katika mashauri yanayoendelea mahakamani.

Wanasheria wanaweza kutuhumu majaji kua wamefikia maamuzi yao kutokana kua waliahidiwa bilioni miambili na rais , kwahiyo wanafanya hivyo kutimiza malengo yao.

Kama mwananchi wa kawaida na mdau wa sheria, kwakweli kauli ile haikua sahihi. Na inahitajika uamuzi wa busara kabisa ufanyike ili hili jambo liishe vyema kwani kuna kila dalili ya maombi kupelekwa mahakamani ili mashauri yasimamishwe mpaka kauli hiyo itakapofutwa.

Nawasilisha.
 
Kweli wabongo tuna gubu, katika yote aliyoongea umeona umkosoe tu? msifie basi hata kwa mazuri aliyozungumza. Binafsi sijaona kama amewapangia maamuzi majaji naona kama amewapa mkakati wa kazi tu bado maamuzi yatatolewa na majaji na kwa kufata sheria za nchi.Tatizo wapiga dili wengi walizoea ikulu kama kimbilio lao.
 
Hata hili tukisema watakuja kubisha na kutetea kuwa Rais kasema sawa tuu. Kwa hiyo anasema ni lazima Mahakama iwaone na hatia ili serikali ijipatie hizo Trilioni moja na mahakama iambulie hapo mgawo wake na kupata pesa ili wajilipe posho na mazaga zaga mengine.
Ndio maana tunasema Magu katika hotuba zake anatoa zikiwa hazina viwango. Binafsi ningependa chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kitolee tamko kali la kupinga kauli ile ya Rais. Na sio hao tuu hata Tume ya haki za binadamu nayo isikae kimya kabisa.
 
SIMPLY NOSENSE
Najua utakuja na hoja kwamba urais ni Institution. Lakini Rais pia ni raia wa JMT. Ana haki ya kutoa maoni yake. Hotuba siyo mahakama.
"Independence of the Judiciary 107B. In exercising the powers of dispensing justice, all courts shall have freedom and shall be required only to observe the provisions of the Constitution and those of the laws of the land".
Be fair.
 
Kweli wabongo tuna gubu, katika yote aliyoongea umeona umkosoe tu? msifie basi hata kwa mazuri aliyozungumza. Binafsi sijaona kama amewapangia maamuzi majaji naona kama amewapa mkakati wa kazi tu bado maamuzi yatatolewa na majaji na kwa kufata sheria za nchi.Tatizo wapiga dili wengi walizoea ikulu kama kimbilio lao.
Haupo sahihi kabisa. Hapo tunazungumzia haki za kikatiba za Raia wa nchi hii, sio Rais anaingilia uhuru wa Mahakama kisha mnaona kuwa ni jambo la kawaida tuu.
 
Hata hili tukisema watakuja kubisha na kutetea kuwa Rais kasema sawa tuu. Kwa hiyo anasema ni lazima Mahakama iwaone na hatia ili serikali ijipatie hizo Trilioni moja na mahakama iambulie hapo mgawo wake na kupata pesa ili wajilipe posho na mazaga zaga mengine.
Ndio maana tunasema Magu katika hotuba zake anatoa zikiwa hazina viwango. Binafsi ningependa chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kitolee tamko kali la kupinga kauli ile ya Rais. Na sio hao tuu hata Tume ya haki za binadamu nayo isikae kimya kabisa.

Mkuu kwenye red apo unaweza kutuwekea ka clip ka hayo maneno wakati anayatamka, au wewe kwa akili yako ndo umeelewa ivo.
 
Haupo sahihi kabisa. Hapo tunazungumzia haki za kikatiba za Raia wa nchi hii, sio Rais anaingilia uhuru wa Mahakama kisha mnaona kuwa ni jambo la kawaida tuu.

Ni kweli mkuu lakini mahakama zetu zimegubikwa sana na rushwa, kesi ya wazi kabisa wanaipindisha mtu anashinda. Hela inaweza ikapigwa, walioipiga wakapatikana kwa ushahidi usio na shaka ila ikifika mahakamani wanapeta. Mahakama nazo zimejaa mazingaombwe sana.
 
Kweli wabongo tuna gubu, katika yote aliyoongea umeona umkosoe tu? msifie basi hata kwa mazuri aliyozungumza. Binafsi sijaona kama amewapangia maamuzi majaji naona kama amewapa mkakati wa kazi tu bado maamuzi yatatolewa na majaji na kwa kufata sheria za nchi.Tatizo wapiga dili wengi walizoea ikulu kama kimbilio lao.

Mimi muanzisha mada nimemuelewa sana na kwa kweli kuna mambo hayako sawa. Ile ni kama Decree sasa Majaji na Mahakimu watatoaje hukumu ikiwa mkuu wa Nchi katoa hisia zake tena kwa Public? Nafikiri watu wa Sheria watusaidie kuliweka sawa jambo hili. Mahakamani ni sehemu pekee ambapo hata kama mtu kakosa vipi lazima utetez ufanyike, akithibitika kosa anahukumiwa kwa stahiki ya adhabu imfaayo.

Pamoja na uchungu mkubwa alio nao Mh Rais, lakini ajitahidi mambo mengine awaagize watendaji waandamizi INHOUSE! DPP kwa mfano uliotolewa wa Meno ya Tembo, lakini lazima uchunguz ukamilike, hii inasaidia kuipu
nguzia hasara serikali kama mtuhumiwa akishinda kesi hasa kama mashtaka hayakupangiliwa vema!

Ni ombi letu wanaomshauri Mh. wamsaidie ili kulinda hadhi yake!
 
Tatizo ni uelewa wako mdogo wa maswalal ya sheria, kaa kimya.
 
Mimi kilicho nishitua nimaagizo kwa Dpp yakwamba unamkamata. Mtuu nakizibiti. Etii. Unaperereza. Unaperereza. Nini. Auunatenge za. Rushwa. Tukumbuke. Vyombo. Vyadora. Vimekuwa. Vikituhumiwa. Kuwabambikia. Watuu. Kesii. Jee. Kwakauli. Ya. Raisi. Sasawatu. Siwatabambikiwa madawa. Yakurevya. Naakikatwa. Anafikishwa. Mahakamani Nakesho itabidii. Ahukumiwe Ukweli jambo iloo linabidi liangaliwe. Kwaupana. Kubwa.
 
Hata hili tukisema watakuja kubisha na kutetea kuwa Rais kasema sawa tuu. Kwa hiyo anasema ni lazima Mahakama iwaone na hatia ili serikali ijipatie hizo Trilioni moja na mahakama iambulie hapo mgawo wake na kupata pesa ili wajilipe posho na mazaga zaga mengine.
Ndio maana tunasema Magu katika hotuba zake anatoa zikiwa hazina viwango. Binafsi ningependa chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kitolee tamko kali la kupinga kauli ile ya Rais. Na sio hao tuu hata Tume ya haki za binadamu nayo isikae kimya kabisa.
Mkuu nashukuru kwa kunielewa kwamba, kauli hiyo imeprejudice all the proceedings that are still pending in our courts, chakufanya ni all the proceedings zisimamishwe mpaka maelezo ya kina yatolewe kuhusiana na hii kauli, tunapotoa kauli tuangalie ni kwa namna gani tunapoteza na haki za wengine as well.
 
Mimi muanzisha mada nimemuelewa sana na kwa kweli kuna mambo hayako sawa. Ile ni kama Decree sasa Majaji na Mahakimu watatoaje hukumu ikiwa mkuu wa Nchi katoa hisia zake tena kwa Public? Nafikiri watu wa Sheria watusaidie kuliweka sawa jambo hili. Mahakamani ni sehemu pekee ambapo hata kama mtu kakosa vipi lazima utetez ufanyike, akithibitika kosa anahukumiwa kwa stahiki ya adhabu imfaayo.

Pamoja na uchungu mkubwa alio nao Mh Rais, lakini ajitahidi mambo mengine awaagize watendaji waandamizi INHOUSE! DPP kwa mfano uliotolewa wa Meno ya Tembo, lakini lazima uchunguz ukamilike, hii inasaidia kuipu
nguzia hasara serikali kama mtuhumiwa akishinda kesi hasa kama mashtaka hayakupangiliwa vema!

Ni ombi letu wanaomshauri Mh. wamsaidie ili kulinda hadhi yake!

Mkuu labda mimi uelewa wangu mdogo, ivi inakuwaje umemshika mtu na kidhibiti afu unapeleleza miaka ata mitatu na bado huyo mtu akakutwa hana hatia, mfano sheria inakataza kuua tembo, tembo wanakufa, meno yanakamatwa, wahusika wanakamatwa tena na udhibiti usio na shaka, bado mtu anashinda kesi, Ivi inaingia akilini kweli!!!!!!!!!!!?????????????
 
Kuingilia uhuru wa mahakama nafikiri unavunjwa pale ambapo kuna kesi ipo mahakamani inaendelea na serikali kutoa shinikizo nini kifanyike. Pili, sidhani kama Rais amezungumzia kitu chochote ambacho kipo mahakamani zaidi ya kuwataka Mahakama, Polisi na DPP kumaliza mashauri haraka iwezekanavyo!
 
Mafisadi kiama chenu kimekuja....
AmekuJA KUWASHIKAAAAAAA.

Mtatafuta kila mlango wa kutokea na hamtapata.
Siasa weka pembeni, ile kauli haikutakiwa kutolewa pale, kuna hatari watu kupoteza haki zao, kisa kufikia malengo ya kukusanya trilioni moja,
 
Back
Top Bottom