Kauli ya Nape kuwa hakuna wizi wa vifurushi na mwenye ushahidi apeleke, ni ya hovyo mno

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,562
KAULI YA NAPE KUWA,HAKUNA WIZI WA VIFURUSHI NA MWENYE USHAHIDI APELEKE, NI YA HOVYO MNO.

Na Bashir Yakub, WAKILI
+255 714 047 241.

Wizi upo na ushahidi ni vigumu kuupata. Na hii ni kwasababu ushahidi wa matumizi ya vifurushi wanao wenyewe wanaotuuzia vifurushi. Wao ndo wana Mita za ufuatiaji sisi hatuna.

Mathalan, ni mtumiaji yupi mwenye kifaa cha kufuatilia matumizi ya GB 1 aliyoinunua. Ajue kwamba wakat nikiperuz mita ya matumizi ilikuwa ikitembea kwa spidi fulan hivyo mpaka sasa nimetumia kiasi fulani. Nape mwenyewe hana uwezo huo.

Vifaa hivyo na mita za kufuatilia natumizi wanazo wenyewe wanaotuuzia mabando. Halafu bado Nape anaomba ushahidi wa matumizi kutoka kwa mwananchi wa Manzese, tuachage utani jamani.

Sisi watumiaji ni vipofu. Tunajua tunachonunua lakini hatujui tulichonunua kinatumika vipi na kwa mwendo upi. Kwenye matumizi tumezibwa macho na ni maksudi. Tunasubiri tu kuambiwa BANDO LAKO LIMEKWISHA.

Unawezaje kumtaka kipofu aliyepigwa akupe ushahidi wa kuona aliyempiga. Halafu umlazimishe kuwa kama hakuona basi hujapigwa. Huyu haoni unamtakaje akupe ushahidi wa kuona tukio likitendeka.

Kwanza Nape amejuaje kuwa hakuna wizi. Ni kampuni au taasisi ipi imepata access ya kufanya uchunguzi wa kina kwenye mitambo ya makampuni ya simu na kugundua kuwa hakuna wizi.

Suala la wizi wa vifurushi ni la teknolojia ya hali ya juu mno. Ni suala ambalo kuligundua unahitaji muda na teknolojia iliyo juu ya ile ya makampuni ya simu. Sio suala la kumtaka mwananchi wa Kivule akuletee ushahidi.

Yapo makampuni makubwa ya kimataifa yanafanya kazi hizi. Unahitaji kuyapa kazi na muda ili yakuletee taarifa ya uchunguzi wa kiteknolojia.

Rafiki yangu mmoja kutoka makampuni haya haya ya simu ananiambia hakuna kampuni zinazoogopwa na Makampuni ya simu kama hizi kampuni ambazo kazi yake ni kufuatilia matumizi ya vifurushi na mda wa maongezi.

Ananiambia kuna moja ilitoka ufaransa ikaja kuomba kibali kufanya kazi Tanzania haikuthubutu kupata. Makampuni ya simu kwa kushirikiana na akina fulani yalihakikisha haianzishi operesheni zake nchini na haikuweza.

Suala la wizi wa vifutushi sio dogo. Ni kubwa mno na kilio cha mda mrefu cha Watanzania. Tunahitaji uchunguzi wa kina kutoka makampuni maalum yanayofanya kazi hizi na wadau. Ghana walifanya na wizi uliogindulika ulikuwa wa kutisha.

Sisi sio wajinga tulalamike kila siku tunaibiwa wakati sio kweli, tuheshimiane bana.

Yaani Nape anafanya uchunguzi wa jambo kubwa kama hili kwa kuwauliza makampuni ya simu na Tcra, serious??. Yaani unamuuliza mtuhumiwa halafu unategemea akupe majibu ya kujitia hatiani.

Na wao wanakujibu kwamba hakuna wizi wowote bali ni watu tu wenyewe wanaacha simu zinajiupdate vifurushi vinaliwa halafu wanalalamika wameibiwa. Na wewe unakuja mbio kutwambia hivyo hivyo kama walivyokwambia.

Kwa mfano ulitegemea wakwambie nini labda. Kwamba ni kweli tunawaibia watu vifurushi ama. Tuache mzaha na maisha ya watu.

Ni ahadi yetu ya dhati kwenu kuwa suala la vifurushi katu halitaisha kirahisi bila mwizi kukamatwa, iwe leo ama kesho, liwe jua ama mvua, machweo ama mawio, usiku ama mchana.
 
Mleta mada bila ya wewe pia kuleta ushahidi wa vipi tunaibiwa basi huna tofauti na huyo unayemshutumu.

Muda mrefu uliopita ulijifanya muhanga wa kuwapeleka mahakamani mashirika ya simu kwa suala hili la bando.

Wengi wakakusifia kwamba umekuja wakili wa kututetea dhidi ya haya mashirika.

Mara paap ukapotea na zikatokea fununu hapa JF kwamba umezibwa mdomo kikubwa. Anayeweza kujibu kilichotokea na maendeleo ya kesi kama kweli ilifunguliwa ni wewe.

Isije ikawa umekuja kupima tena upepo.

Prove me wrong please.
 
Waeleze jinsi ya kuzima automatic update. Sio kusema tu kuna automatic updates zinaendelea ndani ya simu kimya kimya
 
Waziri wenye uwezo mdogo wa kuchambua mambo hivi hatujiulizi mbona miaka ya hivi karibuni speed ya mabando imekuwa kubwa sana tofauti na huko nyuma yaani unapewa 1Gb ni kama umepewa mb 300

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo ushahidi hawezi kuulete ila kwanza naungana nae moja kwa moja. Pili wengi wanaompa za uso ni agent wa mitandao hii na hii inajizihirisha pale wasio comment wana koment leo. Hawa agent wanapewa dakika,sms na Gb kwa matumizi yao binafsi na mitandao hii na ndio maana sio wahanga moja kwa moja.

Nije kwenye msingi wake wa hoja, hoja ina mantiki yake hii na mifano ipo mingi japo mifano hiyo haitajenga ushahidi wa moja kwa moja.

Naamza na TIGO tigo hata wao wenyewe wakati wa matumizi ya mwisho ya kifurushi chako cha MB wanajichanganya sana hasa unapokuwa mtandaoni kifurushi hakifanyi kazi like data depleted ila ukicheki salio ni Mb 16 au 5 au 8. Na ukizima data na kufungua tena ndipo zina malizia na itaingia internet.

Huu ni mfano tosha kuonyesha wanawahi kuchukua data au wanakata pakubwa sana kiasi cha mfumo wao kushindwa kuelewa.
Airtel na Halotel hawa ni kama twins kwani mb zao zinaisha hata kama haufanyi kazi kubwa internet. Hapa sina wasiwasi kuwa mb zao sio halisi mfano ukiambiwa GB 1 basi jua hizo ni Mb 550 na hata ukiangalia matumizi ya data kwa airtel na halotel kwenye simu inaonyesha inetumia data kidogo zaidi ukilinganisha na vodacom na Tigo japo mtandao wao upo chini pia.

Vodacom nao pia wanakata Mb mfano nunua kifurushi cha gb au mb 550 zikibaki mb 100 hapo hata nyimbo 10 za audio zenye ukubwa wa mb 4 hautaweza kudownload zote. Huu pia ni wizi mwingine karibia mitandao yote wanafanya na wanajuana kuwa cc tunaiba kwa njia fulani na wanapeana uzoefu.

Juzi nimesajili Tigo na anayesajili amenipiga hela yaani badala ya kuniunganishia cha GB 1 kile cha 1500 yy anenunua cha 500 mb 300. Wizi huu pia umerithishwa hadi kwa mawakala wao na wanachofanya wao ni mwendelezo tu uleule wa kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.

Kwanza tumshukuru kwa kuwatikisa makampuni hadi mda huu airtel na halotel data unaweza kumrushia mwingine, lakini vilevile salio la kawaida halikatwi kama haujajiunga kwani huko nyuma pamoja na kuwa na kifurushi ila walikuwa wanasokonyoa.

Namaliza kukazia hoja yangu kwa kusema mitandao yote inatabia ya kuwaunganisha watu kwenye huduma zao zinazokata salio bila ya ridhaa ya watumiaji wa mtandao huo na huu pia sio wizi? Mnijibu mnaotetea kuwa mitandao haiibi.
 
Mjomba Nape kashiba hawajui wenye njaa... Mitandao inaiba sana , kuna siku niliweka salio likakatwa ukipiga customer care wanasema wanashughulikia mpk sasa hawajarudisha
 
Japo ushahidi hawezi kuulete ila kwanza naungana nae moja kwa moja. Pili wengi wanaompa za uso ni agent wa mitandao hii na hii inajizihirisha pale wasio comment wana koment leo...
Kwenye hii comment naunga mkono hoja ya kuhusu tigo kutokufanya kazi kwa internet ukibakiwa na mb kama 15. Shenzi sana tigo
 
Mbona App za kupima matumizi yako ya data zipo nyingi tu
Hata simu yako unaweza kuset na ukajua jumla ya matumizi yako ya data...... SIMPLE TU
Sijui mleta mada anazungumzia meter gani nyingine, hiyo ndyo kipimo cha kujua unaibiwa ama huibiwi
Screenshot_20220219-081249.jpg
 
Wengi wanaomsapoti Nape ni wale ambao wana vi maslahi na hayo makampuni ya simu.

Nimesema vi-maslahi kwa sababu wanachotuibia hawa Sale's agents ni punje ila tunachopigwa na hizo kampuni ni hell of money!

Nape alipaswa kuwasiliana na TCRA kimya kimya tena ikibidi asiwatumie hao maafisa wa TCRA,Maana nao kwenye hili ni watuhumiwa pia.
Wanakula urefu wa kamba yao.

Uchunguzi unapaswa kufanywa kimya kimya bila matangazo.

Ukitangaza wanarekebisha mitambo kwa muda.
 
Tatizo mnaleta ushoga kwenye hoja za msingi kama hii. Mtoa mada akaeleza vizuri sana. Ni jukumu la serikali kufanya uchunguzi kwa msaada wa vyombo hivyo vya kimataifa. Yeye kamprove wrong waziri. Waziri yeye aliyesema hatuibiwi na tunaibiwa tupeleke ushahidi,yeye alitoa wapi ushahidi uliomsukuma kusema aliyoyasema? Inability to explain the fact is no reason of denying it to be the fact.
 
Back
Top Bottom