Kauli ya Mzee Mwandosya hii hapa

Kauli ya Mzee Mwandosya hii hapa

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Posts
4,582
Reaction score
2,783
Haya ni maneno ya Mzee Mwandosya.

Katika nyakati mbalimbali mataifa, na binadamu pia hupita katika vipindi vya majaribu (testing times). Majaribu hayo ni njia moja ambayo naamini Mwenyezi Mungu, muweza wa yote, humuimarisha mtu na huimarisha Taifa iwapo tunaweza kuyamudu. Hiki ndio kipindi tunachopita sasa kama Taifa. Kwa maneno hayo napenda, kwa unyenyekevu mkubwa, kuwashukuru, na kwa dhati kabisa, wale wote mliotuunga mkono kabla na baada ya kutangaza nia, wakati wa na baada ya kuchukua fomu za kuomba nafasi hiyo, kwa imani kwamba tunakidhi, na pengine tunazidi vigezo vilivyoorodheshwa.

Mliotudhamini kwa matumaini makubwa, mliotusaidia, kwa hali na mali kufanikisha zoezi la kupata wadhamini, na wengi mliotuletea, kwa njia mbalimbali, ujumbe wa kutuunga mkono, tunawashukuru. Haikuwa kama tulivyotarajia, na mlivyotarajia. Kila tukio lina maana yake katika maisha. Hatimaye ukweli unabakia kwamba Taifa ni kubwa kuliko nafsi na utashi wetu kama mtu mmoja mmoja.

Asanteni Kaskazini Pemba, Kusini Pemba, Kaskazini Unguja, Mjini Unguja, Magharibi Unguja, Kusini Unguja, na Tanzania Bara, kutoka Tanga mpaka Katavi, na kutoka Kagera mpaka Mtwara. Mbeya, nawashukuru. Mmenilea na hivyo kunifanya hatimaye nitoe utumishi kwa nchi yetu tunayoipenda. Rungwe,na mahsusi Rungwe Mashariki (Busokelo), mmeniamini na siku zote mmenipa ushirikiano uliotuwezesha kufanya yale mengi tuliyoyaweza.

Ndugu na marafiki zangu na wenzangu katika utumishi wa umma, kwa ujumla wenu, nawashukuru. Asanteni sana. Familia yangu daima imekuwa ngome yangu katika maisha. Nitaendelea kutoa mchango wangu kwa Taifa kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyoniwezesha. Kiswahili hakijasheheni katika istilahi, hasa pale unapotaka kutoa maneno ya shukrani kutoka sakafu ya moyo.

Yatosha kusema ASANTE SANA.
 
Gaza and Israel

kauli inathibitisha Urais sio kufa kupona-lakin tumeona ma opportunist walivyoweza kutos, wapi Nchimbi, Sophia Simba etl?
 
Last edited by a moderator:
Angalau kaonyesha hakukadhamiria kufa na mtu akitoswa, nasubiri kauli kutoka upande mwingine.
 
Busara sana. Nimeipenda hiyo hotuba ya Ku concede defeat. Asiyekubali kushindwa si mshindani. Hongera prof Wang wa ukweli.
 
kauli inathibitisha Urais sio kufa kupona-lakin tumeona ma opportunist walivyoweza kutos, wapi Nchimbi, Sophia Simba etl?

hawa ni vibaka wa kisiasa,huyu sofia kabebwa sana na jk,sasa anataka kunyea kambi.....mda wake umeisha
 
Ur and ll b always the Prof who is truely professor, siasa ni kitu cha ajabu ajabu hasa ktk africa hii ya watu weusi wenye akili nyeusi..najua ulikua kwny mapambano ambayo mara zote kuna option mbili...be blessed Professor wa ukweli
 
Back
Top Bottom