Kauli ya Mufti juu ya katiba mpya

Kauli ya Mufti juu ya katiba mpya

chief72

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
627
Reaction score
309
Amesema...

Nawasihi waislam na wasiokuwa waislam kujiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura, na wala wasipuuze haki hiyo.

Alipoulizwa kama wapige kura ya SIYO au ya NDIO katika katiba pendekezwa alijibu kwa kusema "Siwaambii waislam na wasiokuwa waislam wakapigie Ndio au Hapana ila kila mtu akatumie akili yake mwenyewe kwa kuona inamfaa au hai mfai, hapo ndipo aamue mwenyewe kupiga Ndio au Hapana".

Chanzo: TBC, kipindi cha asubuhi saa tatu
 
Hilo ndio Tamko la Bakwata kwa Waislam, waislam watamfuata maana wengi wanaipenda Bakwata isipokuwa imani kali wachache ndio wanaichukia Bakwata
 
Ni tamko lake binafsi kama lile la Kardinali Pengo kwani wakristo na waislamu wengi wamekwisha kuamua kupiga kura ya HAPANA
 
Mbona huyu nae amechelewa, inakuwa kama ndio anaamka toka usingizini. Mambo ya katiba mpya yameahirishwa ndio anajitokeza leo. Sasa hayo anamwambia nani? _manina!!
 
Mufti na Pengo ndio viongozi wa dini pekee wenye akili na upeo mkubwa wa uelewa wa demokrasia maana yake nini.Tamko la Mufti Liko sawa na Pengo.Watu wasome katiba na waamue wenyewe wapige kura gani.
Asante Mufti mzee wa busara kwa tamko lenye hadhi na linaloachia demokrasia ifanye kazi.Sababu demokrasia huwezi mchagulia mtu appige kura ipi kama walivyofanya wale tamko la maaskofu.

Nyie wazee wawili Mufti na mzee Pengo tunasikia raha kuwa nanyi kama wazee wetu.Asante MUFTI KWA TAMKO HILI.
 
Huyo na Pengo wapo katika payroll ya usalama wa taifa,kamwe hawawezi kuwa wawazi
 
Mufti na Pengo ndio viongozi wa dini pekee wenye akili na upeo mkubwa wa uelewa wa demokrasia maana yake nini.Tamko la Mufti Liko sawa na Pengo.Watu wasome katiba na waamue wenyewe wapige kura gani.
Asante Mufti mzee wa busara kwa tamko lenye hadhi na linaloachia demokrasia ifanye kazi.Sababu demokrasia huwezi mchagulia mtu appige kura ipi kama walivyofanya wale tamko la maaskofu.

Nyie wazee wawili Mufti na mzee Pengo tunasikia raha kuwa nanyi kama wazee wetu.Asante MUFTI KWA TAMKO HILI.
Busara zipi hizo mkuu za Mufti ambaye ameshindwa hata kujenga chuo,hospital,chuo kikuu,hata TV pia imemshinda kuanzisha.Acha kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa manufaa ya watawala
 
  • Thanks
Reactions: BAK
I see, Mawazo ya mufti ni sawa na ya askofu pengo
 
Busara zipi hizo mkuu za Mufti ambaye ameshindwa hata kujenga chuo,hospital,chuo kikuu,hata TV pia imemshinda kuanzisha.Acha kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa manufaa ya watawala

Hizo ni kazi za waumini sio za mufti.
 
Busara zipi hizo mkuu za Mufti ambaye ameshindwa hata kujenga chuo,hospital,chuo kikuu,hata TV pia imemshinda kuanzisha.Acha kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa manufaa ya watawala

Wewe kweli ni kiazi!! Mtoa mada amempongeza mufti kwa tamko lake juu ya kura ya maoni, sasa mambo ya kujenga shule na tv yanahusikaje kwenye mada hii??
 
Mufti na Pengo ndio viongozi wa dini pekee wenye akili na upeo mkubwa wa uelewa wa demokrasia maana yake nini.Tamko la Mufti Liko sawa na Pengo.Watu wasome katiba na waamue wenyewe wapige kura gani.
Asante Mufti mzee wa busara kwa tamko lenye hadhi na linaloachia demokrasia ifanye kazi.Sababu demokrasia huwezi mchagulia mtu appige kura ipi kama walivyofanya wale tamko la maaskofu.

Nyie wazee wawili Mufti na mzee Pengo tunasikia raha kuwa nanyi kama wazee wetu.Asante MUFTI KWA TAMKO HILI.
hapo kwenye red, kabla ya kuahirishwa...watu wangesoma lini hiyo katiba pendekezwa na kufanya maamuzi yao wenyewe? wewe mwenyewe sidhani kama una nakala ya katiba pendekezwa, walioisoma na kufatilia upatikanaji wake wanaona imejaa mizengwe ndo maana wakaja na hayo mapendekezo. pia kumbuka katiba inaandikwa kisheria,....hivo bila kuwa na taaluma ya hiyo fani utaishia kuona tu kwamba 2+3=5 kumbe + mara nyingine ni x
 
Nimejaribu kidownload nakala ya katiba pendekezwa mtandaoni bila mafanikio naomba mwenye link jamani anipe
 
Kwa Tamko Hilo La Mufti Inamaanisha Kuwa Ukipiga Kura Ya HAPANA Sawa Napia Ukipiga Kura Ya NDIO Sawa.Akili Zakuambiwa Changanya Na Zako.
 
Muft katenda haki sio kama wanaomlazimisha mtu apite njia ipi, amri jeshini
 
Mufti na Pengo ndio viongozi wa dini pekee wenye akili na upeo mkubwa wa uelewa wa demokrasia maana yake nini.Tamko la Mufti Liko sawa na Pengo.Watu wasome katiba na waamue wenyewe wapige kura gani.
Asante Mufti mzee wa busara kwa tamko lenye hadhi na linaloachia demokrasia ifanye kazi.Sababu demokrasia huwezi mchagulia mtu appige kura ipi kama walivyofanya wale tamko la maaskofu.

Nyie wazee wawili Mufti na mzee Pengo tunasikia raha kuwa nanyi kama wazee wetu.Asante MUFTI KWA TAMKO HILI.

Hiyo katiba wanayotakiwa kuisoma iko wapi?maana kila kata wanapeleka nakala 3000,sasa je kata moja ina watu 3000 tu?si kila mtu atapata hii katiba pendekezwa
 
Mamluki huyo, huyo ni kiongozi wa waislam feki
 
nasubiri salamu za ngwajima juu ya usemi ulotolewa na mufti
 
Back
Top Bottom