Kauli ya Mkurugenzi LHRC kuhusu Osama ina utata

Mimi nadhani tatizo hapa ni kwamba "ugaidi" -- kwa mtazamo wa nchi za magharibi na wa watu wengine (hata humu JF) ni mauaji yanayofanywa kwa njia za kishenzi na zana za kishenzi. Kwa mfano kujilipua au kwa kutega/kurusha bomu katikati ya watu huuwa watu wasio hatia.

Kwa mtazamo huu vita, kama ile ya Iraq au Afghanistan ambazo pia zinasababisha watu wasio hatia kufa unainishwa kwamba siyo "ugaidi". Wenye mtazamo huu wanaona kwamba njia inayotumika na zana zinazotumika ni za kistaarabu zaidi -- yaani makombora ya Cruise na Tomahawk, vifaru, ndege za kivita nk nk.

Hapa ndipo I see the whole nonsense kwani kufa ni kufa tu -- ukitumia njia zozote -- hata za kistaarabu ni kufa tu! Adui yako usimchagulia silaha -- yaani iwapo mimi nataka kupigana na wewe na sina zana za kisasa, basi niruhusu nitumie njia na zana zangu duni tupigane. Najua sote tutauwa watu wasio hatia lakini usinitangaze eti mie gaidi kwa kuwa nauwa wasio hatia. Na wewe pia gaidi vile vile.

Kwa upande mwingine ndugu zangu -- vita ni ugaidi vile vile ni vigumu kulipinga hili -- kwa sababu watu wasio hatia nao hufa.
 
Nakubaliana na wewe Mkuu...........ndio maana kwenye post yangu nimesema hizi definitions za haki za binadamu pengine tuziangalie upya.........its insane kukaa na kuangalia mtu anaua ua tu huku tukisema eti haki za binadamu.............lets draw a line somewhere.......waliozitunga/ziandika hizo sheria/haki za binadamu ni binadamu kama wewe na mimi.....kitu gani kituzuie tusifikir kwa mapana na kuzirekebisha hizi definitions...............

Sawa Mkuu....ndio maana nikasema hizi haki definitions za binadamu inabidi ziangaliwe upya...............

I personally do not condone neither ugaidi nor to kill someone/anyone or what you guys call haki za binadamu.........ninacho taka kusema hapa watu tumekuwa tunapiga kelele kuhusu haki za binadamu pale tu US anapofanya/pambana na wapinzani wake ambao pia walituathiri na sisi hapa nyumbani (Tanzanians died from OBL actions)............I neither saw my brothers or any body condemning Al Qaida terrorist actions.............sana sana serikali yetu ilipoweka sheria za kupambana na ugaidi..........tukaanza kupiga kelele eti tunakuwa singled out............
 
Inabidi watu waelewe upana wa dhana tunayojadili. Hakuna anayemtetea Osama. Osama alikuwa nembo ya ugaidi duniani kama vile ambavyo America ni nembo ya vita dhidi ya ugaidi. Tunachosema ni kwamba kuuawa kwa Osama ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi maana ni kuua hiyo nembo. Lakini mimi binafsi sikubaliani na Rais Obama anaposema 'Justice has been done'. Haki ingetendeka tu endapo Osama angefikishwa mahakamani ajibu tuhuma zake zote na ahukumiwe kikamilifu kama angepatikana na hatia. Vilevile angekamatwa na kuhukumiwa tungepata fursa ya kujifunza kwa nini alifanya yale aliyoyafanya. Kibaya zaidi ni kwamba hakuna ushahidi kwamba majeshi ya America yalishindwa kumkamata Osama bila kumuua.
 
hawa jamaa haijulikani wanaongozwa na nani na bodi yao iko na akina nani na manejimenti yao ina consist of akina nani
 
Hii inahusiana vipi na alichosema Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu?
 
Hapo kwenye nyekundu pana tatizo ila imekubidi kwa kuwa wanasiasa lazima wakubaliane na wakubwa kwahiyo sitakulaumu sana najua upo kazini na unalinda unga.
 
Mafundisho ya dini zote yanatuasa tusidhulumu nafsi inaonyesha una uchungu na kina OBL kwakuwa waliwaua ndugu zetu I mean hapa nyumbani sisi ni wahanga wa matukio ya ugaidi lakini huoni uchungu kwa wairaki waliouwawa na majeshi ya amerika maelfu kwa mamia kwa kisingizio cha kutafuta silaha za maangamizi nikuulize wewe ndugu yangu hivi zile silaha zilipatikana? jibu unalo na sisi sote tunawajibu wa kukemea kila ovu tunaloliona katika ardhi hii ya Mungu kwani kesho tutakuja kuulizwa kwani
Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Al-Anfaal aya ya 25 amesema:-

"NA IOGOPENI ADHABU YA MWENYEZI MUNGU HAPA DUNIANI AMBAYO HAITAWASIBU PEKE YAO WALE WALIODHULUMU NAFSI ZAO MIONGONI MWENU BALI ITAWASIBU HATA WALIONYAMAZA WASIYAKATAZE MAOVU. NA WENGINEO PIA. NA JUENI YA KWAMBA MWENYEZI MUNGU NI MKALI WA KUADHIBU."
 
Kama umeangalia na kusikiliza vyombo vya habari leo hii wanasema Osama hakuwa na silaha yo yote. Sasa walishindwa nini kumkamata?
Alikataa ku-surrender ! Hiyo ya kujua kuwa hakuwa na silaha yoyote ni baada ya kumuua na kumpekua, lakini kabla ya kumpekua huwezi kujiaminisha kwamba hana silaha, pengine ipo kwenye kanzu/msuli?
 
Mi nami ni shahidi ila Kiwanga pamoja na kubanwa alikuwa na exit door nyingi ambazo kwa level yake hakutakiwa aonyeshe direct msimamo kama wa Marekani.
 
Alikataa ku-surrender ! Hiyo ya kujua kuwa hakuwa na silaha yoyote ni baada ya kumuua na kumpekua, lakini kabla ya kumpekua huwezi kujiaminisha kwamba hana silaha, pengine ipo kwenye kanzu/msuli?
Jamani mbona kila mtu anaongea lake? Tuwekeeni hizo video za Osama anagoma/anakubali kukamatwa na sie tuchague pumba na mchele
 
Unamshangaa Kiwanga. Obama mwenyewe ni mwanasheria lakini pamoja na sheria zake yeye alikubali kuwa Osama auwawe.

Je utamshangaa J . M. Kikwete kushindwa kuwatosaa mafisadi sababu naye anafikiria fikiria kisheria sheria????

Kuna mambo inabidi siasa na porojo ziwekwe pembeni. Ofcurse watu tungependa kusikia maneno tofauti kwa mtu kama kiwanga lakini ukweli na kuweka unafiki pembeni

  • Osama deserved death
  • Osama was in war with USA.
  • kama mwanajeshi kuuwawa na adui ukiwa hata huna silaha ni jambo la kawaida
Hizo ni rules of engangement...........

Sheria ni just one factor kuna mambo mengine mengi to put into consideration. So Kiwanga yuko sawa

Jamani mbona kila mtu anaongea lake? Tuwekeeni hizo video za Osama anagoma/anakubali kukamatwa na sie tuchague pumba na mchele

Hata wasiposema ukweli Mission ilikuwa ni kumuuua tu. na hiyo ndiyo ilikuwa best option sababu kumkamata hai ingekuwa tabu na mamb ya kisheria yangewa cost. Kila mara Osama angesimama kizimbani angezalisha extrimist zaidi ya 100 duniani.
Hayo ndo mambo wameyakwepa kwa kumuondosha.
 
Mkuuu ebu angalia lecture hii ya huyu jamaa wa havard

Moral Side of murder

Last edited by a moderator:
Ukuu wake wa kituo cha haki za Binadamu na uumini wake katika haki za binadamu vinasigana. Hivyo ninachoweza kuona kwa haraka ni kuwa ukuu wake huo ni kwa ajira si uumini wake katikahaki za binadamu bali Huyo anaganga njaa. Msamehe tu
 
Ndugu,
Ninawasilisha ujumbe toka kwa Francis Kiwanga, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kama alivyoniomba kufanya.
Marcossy.

Ndugu zangu JF,
Nimefuatilia mjadala wa Kauli yangu juu ya kifo cha Osama bin Laden katika jukwaa hili na hata nje yake na kugundua mambo kadhaa ambayo nastahili kuyaweka wazi yakaeleweka vema kwenu na wadau wengine. Moja kati ya vilivyojitokeza ni uimara wenu katika kudai, kuhamasisha na kuhimiza haki za binadamu pale mlipo na hata baada ya hapo; jingine ni namna mlivyo na matumaini makubwa juu ya kazi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, LHRC.

Nimejifunza toka mjadala huu kuwa mko makini kujua na kufuatilia HAKI za binadamu bila kujali tofauti eyote miongoni mwa binadamu na namna wengine wanavyoweza kuwahukumu. Naheshimu mawazo yenu kwani mmetimiza wajibu wenu wa Kikatiba. Kwa msingi wa mjadala huu pia nimependelea nitoe ufafanuzi wa maneno niliyonukuliwa na BBC juzi jioni (03 Mei 2011) na kusikika jana (04 Mei 2011) asubuhi ambayo ndiyo yaliyozua mjadala mkali hapa JF. Ukweli ni kuwa maneno yaliyonukuliwa hayakuwa yenye maana ya kujitosheleza:

(…kuuwawa kwa Osama kunaweza kuwa sawa kwa kuzingatia mazingira yake.)

Kichwani mwangu nilikuwa nawaza je, kwa kuzingatia mazingira ya suala hilo kulikuwa na nafasi ya kumkamata Osama/ au yeye mwenyewe kujitokeza katika vyombo vya sheria ili utawala wa sheria uchukue nafasi yake?
Maneno hayo yalitanguliwa na maneno:
"… ni vigumu kushangilia kifo cha mtu yeyote na msimamo wetu kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu … pia ni wajibu wa kila kulinda na kutetea haki za binadamu na kuifanya dunia ni mahali bora pa kuishi"

Katika mahajiano yale, niliweka wazi siungi mkono kwa namna eyote kuuwawa kwa binadamu yeyote, achilia mbali Osama bin Laden. Na labda nirudia kusema pia kuwa hatushangilii kifo cha Osama na pia hatuungi mkono ugaidi na matendo ya kigaidi ambayo lengo lake ni kuleta hofu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani,. Huu ndio uelewa wangu.
Nawasilisha.

Francis Kiwanga

Francis K. Kiwanga
Executive Director
Legal and Human Rights Centre-LHRC
P.O.Box 75254
Dar es salaam
email; fkiwanga@humanrights.or.tz
Phone; +255 22 2773038/48
Mobile;+255 787 229933

"My life is my message" M. Ghandi
 
Ndugu,
Ninawasilisha ujumbe toka kwa Francis Kiwanga, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kama alivyoniomba kufanya.
Marcossy.

Ndugu zangu JF,
Nimefuatilia mjadala wa Kauli yangu juu ya kifo cha Osama bin Laden katika jukwaa hili na hata nje yake na kugundua mambo kadhaa ambayo nastahili kuyaweka wazi yakaeleweka vema kwenu na wadau wengine. Moja kati ya vilivyojitokeza ni uimara wenu katika kudai, kuhamasisha na kuhimiza haki za binadamu pale mlipo na hata baada ya hapo; jingine ni namna mlivyo na matumaini makubwa juu ya kazi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, LHRC.

Nimejifunza toka mjadala huu kuwa mko makini kujua na kufuatilia HAKI za binadamu bila kujali tofauti eyote miongoni mwa binadamu na namna wengine wanavyoweza kuwahukumu. Naheshimu mawazo yenu kwani mmetimiza wajibu wenu wa Kikatiba. Kwa msingi wa mjadala huu pia nimependelea nitoe ufafanuzi wa maneno niliyonukuliwa na BBC juzi jioni (03 Mei 2011) na kusikika jana (04 Mei 2011) asubuhi ambayo ndiyo yaliyozua mjadala mkali hapa JF. Ukweli ni kuwa maneno yaliyonukuliwa hayakuwa yenye maana ya kujitosheleza:

(…kuuwawa kwa Osama kunaweza kuwa sawa kwa kuzingatia mazingira yake.)

Kichwani mwangu nilikuwa nawaza je, kwa kuzingatia mazingira ya suala hilo kulikuwa na nafasi ya kumkamata Osama/ au yeye mwenyewe kujitokeza katika vyombo vya sheria ili utawala wa sheria uchukue nafasi yake?
Maneno hayo yalitanguliwa na maneno:
“… ni vigumu kushangilia kifo cha mtu yeyote na msimamo wetu kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu … pia ni wajibu wa kila kulinda na kutetea haki za binadamu na kuifanya dunia ni mahali bora pa kuishi”

Katika mahajiano yale, niliweka wazi siungi mkono kwa namna eyote kuuwawa kwa binadamu yeyote, achilia mbali Osama bin Laden. Na labda nirudia kusema pia kuwa hatushangilii kifo cha Osama na pia hatuungi mkono ugaidi na matendo ya kigaidi ambayo lengo lake ni kuleta hofu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani,. Huu ndio uelewa wangu.
Nawasilisha.

Francis Kiwanga

Francis K. Kiwanga
Executive Director
Legal and Human Rights Centre-LHRC
P.O.Box 75254
Dar es salaam
email; fkiwanga@humanrights.or.tz
Phone; +255 22 2773038/48
Mobile;+255 787 229933

“My life is my message” M. Ghandi
 
ata mtu awe mbaya vipi, ama amefanya makosa makubwa kiasi gani, katika sheria anahaki zake za msingi ambazo lazima ziheshimiwe, huyo mkurugenzi wa tume ya haki za binadamu kama mwanasheria na vile vile kama mwanaharakati wa haki za binadamu lazima awe analitambua hili,so kwangu mimi maneno aliyoyatoa hayakuwa sahihi.
 
shossi,
Vipi kaka kila nikitupa jicho upo kwenye mada hii? Naona hata xman pia habanduki: salama lakini? Nani amefuatilia picha ninazoambiwa ziko mtandaoni za OBL atujuze hapa?
 
wazungu wanasema he who pays the piper, plays the tune.
"Wazungu wanasema he who pays the piper, plays the tune," sasa kama umeshamlipa piper kwa nini wewe tena ndio u play the tune? Haahahahaaaa...

Tunarudi pale pale, uwezo wetu wa kujieleza Watanzania ni mdogo mno, ndio maana unakuta Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu anasema kumuua suspect ni poa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…