Kauli ya Mkurugenzi LHRC kuhusu Osama ina utata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya Mkurugenzi LHRC kuhusu Osama ina utata

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, May 4, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Jamani wana JF:

  Hii imekaaje? Leo asubuhi katika kipindi cha BBc (swahili) nilimsikia John Selembi akimhoji mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Francis kiwanga kuhusu kifo cha gaidi Osama bin Laden.

  kiwanga alisema kuuwawa kwa Osama ni sawasawa kwani yeye pia aliua watu bila hatia.

  Kwa mtu wa kawaida kauli hiyo ni sawa, lakini kwa yeye akiwa mkuu wa kituo kinachotetea sheria na haki za binadamu siyo sahihi kabisa. Hawezi akasema hivyo wakati taasisi yake inasimamia na inatetea haki ya binadamu pamoja na utaratibu wa mkondo wa sheria kuhusu watuhumiwa -- kwamba wafikishwe mahakamani ili haki itendeke.

  Kauli hiyo ya Kiwanga ina maana kwamba muuwaji akiua naye auwawe bila kufuata mkondo wa sheria, kitu ambacho sicho LHRC inakisimamia.

  Selembi alimbana sana kiwanga kwa kauli hiyo naye akarudia tena majibu hayo hayo.

  Ni bora Kiwanga angeishia tu kwa kusema: "Kuuwawa kwa Osama ni sawa lakini ni bora angekamatwa na kufikishwa mahakamani."

  Hii ingemtakasa Kiwanga na hasa katika kile taasisi yake inachokisimamia -- hata kama suala la kumkamata Osama lilikuwa gumu sana kama inavyoelezwa.

  Nawasilisha mada kwa mjadala.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nami nilimsikia Mkurugenzi huyo wa LHRC akizungumza BBC na nilishangaa kwa kuonekana anabadilisha kile taasisi yake inachokisimamia. Inafaa ajieleze iwapo LHRC sasa inasimamia ukiukwaji wa kanuni za sheria na haki za binadamu, au sivyo ajiuzulu.
   
 3. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  endelea kuota.

  kujiuzulu ni utamaduni. tanzania hatuna huo utamaduni.
   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Kuuwawa kwa Osama ni sahihi, kutokana na mazingira, kumbuka Marekani walikuwa na lengo la kumkamata kwa kujisalimisha, lakini alikataa, na kumbuka yeye alikuwa kiongozi wa taasisi kubwa duniani ya kigaidi.Kuendelea kumbembeleza kungeweza kuleta maafa makubwa zaidi ya yeyey kuuwawa.Hapa ni kuangalia cost benefit analysis, je wafe wengi au afe mmoja na dunia ibaki salama????

  Marekani wangependa zaidi kumkamata akiwa hai kwani ingesaidia kupata taarifa muhimu, lakini haikuwezekana.Mkurugenzi ameongelea kwa kuzingatia cost benefit analysis.
   
 5. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #5
  May 4, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Bahati sijasikiliza hii. Lakini ni kweli, basi hii ni kauli ya kusikitisha sana kwa mtu wa kiwango chake na wa shirika lake. Mambo mawili, ama kutokuelewa upana wa dhana ya haki za binadamu au alilazimika kujiuza kwa wa America kwa sababu ama wanapokea ufadhili kutoka USAID au wanatarajia hivyo huko mbeleni. Bora iwe ya kwanza, kama ni ya pili it is really disappointing for such a huge organisation in our country.
   
 6. v

  valour Senior Member

  #6
  May 4, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nadhani Mkumbo hauko fair ku comment kwasababu hukumsikia Mr. Kiwanga alivyoongea leo asubuhi na BBC. Nadhani alijaribu kuangalia pro and cons na kutoa analysis yake. Hata kama taasisi yake inasimamia haki za binadamu inabidi uangalie case to case. Osama alishakuwa tishio duniani, for him killing was part of his life. Sasa itakuwa ajabu sana kama taasisi itamtetea mtu mmoja wakati huyo mtu anaua massive ya watu. Aliweka wazi kuwa sio kila kitu cha marekani anatetea na kutoa mifano mbalimbali ambayo taasisi yake ilipiinga marekani.

  Mimi nadhani Mr. Kiwanga amekuwa mkweli na kusema kile ambacho anakiamini. Itakuwa sio sahihi kusema kitu usichomaanisha moyoni kama mtoa mada alivyojaribu kumsahihisha "Ni bora Kiwanga angeishia tu kwa kusema: "Kuuwawa kwa Osama ni sawa lakini ni bora angekamatwa na kufikishwa mahakamani."

  Marekani waliweka wazi kuwa nia yao ilikuwa kumshika iliposhindikana hawakuwa na jinsi. Osama ameumiza watu wengi na Tanzania tulikuwa affected. Yaliyofanyika yamefanyika, tugange yajayo.
   
 7. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wengi wanawaogopa wamarekani, ukitetea Osama nawe utaonekana gaidi. Nafikiri amejibu mdomoni lakini akilini na moyoni anajua ofisi yake inachokifanya.
   
 8. T

  Taso JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Kwa nini ni bahati?

  hahahahaaaaa.... Unajua wabongo hatujui kabisa kujieleza, ndo maana watu kama huyo Mkurugenzi wanakuwa wanachemka chemka.

  Kipindi hujakisikia, halafu unaanza na "bahati sijasikiliza," Ph D mzima kweli?

  Kumbe we mwenyewe ungechemka. Unamkosoa kwa ku endorse kifo cha Osama halafu unasema angesema "Kuuwawa kwa Osama ni sawa"! Yani tuna safari ndefu sana mbele yetu.
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  In short LHRC ina support law of the Jungle and it does not believe in rule of law

  Maybe someone should write an e-mail to his management wajieleze

  Ingependeza zaidi JF ikaa waanika hawa jamaa
   
 10. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kama umeangalia na kusikiliza vyombo vya habari leo hii wanasema Osama hakuwa na silaha yo yote. Sasa walishindwa nini kumkamata?

  Kwa hili mimi ni conspiracist, maana kuna kitu wanaficha hawatwambii ukweli. Kuna uwezekano mkubwa aliyeuwawa siye Osama na wamefanya photoshopping au kutuletea picha ya Osama look alike halafu wakasingizia kumuua.

  Huyu jamaa alikuwa kwenye kidney dialysis machine sidhani kama angeweza kusurvive miaka yote hiyo baada ya yale mashambulizi. Na hasa hizo harakati za kusafiri huku na kule katika mazingira ya kutatanisha.

  Wamarekani wanataka kumaliza hii chapter na kujitayarisha na uchaguzi ujao. Subiri baada ya mwaka mmoja utasikia stori nyengine kabisa.
   
 11. m

  macinkus JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  wazungu wanasema he who pays the piper, plays the tune. swali la kujiuliza ni hivi shirika analoliongoza kiwanga ni nani mfadhili wake mkubwa?

  macinkus
   
 12. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Namfahamu huyu jamaa bana, alikuwa bado ana usingizi tu hakuelewa swali vizuri huwa hana majibu ya hivo
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  CHA AJABU HAWAJAWEKA MAJINA YA WHO IS WHO KWENYE HII JUMUIYA

  [​IMG]
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ugaidi/Mauaji yaliyofanywa na OBL na kundi lake....hazikuwepo haki za binadamu eehh............Hivi hizi haki za binadamu ziko kwa OBL tu baada ya kuuawa?..............hivi OBL ndiye alikuwa pekee mwenye damu ya kibinadamu..........hizo definitions za haki za binadamu inabidi tuziangalie upya.................we must draw a line somewhere.............
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa hawaweki majina ya WHO IS WHO kwenye website yao...wanaficha nini?
   
 16. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #16
  May 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye bold watatokea watetezi wa haki za binaadamu watamtetea osama.
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sorry, hujamuelewa mtoa mada wala hujamuelewa alichokisema Mkurugenzi LHRC. Hayo unayosema wewe ni sawa kabisa, wengi wanasema hivyo nami pia. Suala hapa yeye Kiwanga hakupaswa kusema hivyo kwani anawakilisha taasisi inayosimamia misingi ya sheria na haki -- na siyo law of the jungle!

  Ni vyema angemwambia mtangazaji wa BBC kwamba "haya nayosema ni maoni yangu binafsi kama Francis Kiwanga, na siyo ta LHRC." Hapo angeeleweka -- angekuwa namsimamo kama wako, mimi na wengine -- lakini siyo kuihusisha taasisi ya LHRC katika ukiukwaji huo wa sheria na haki.
   
 18. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #18
  May 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Huyo mkurugenzi hajui kwanini Osama na magaidi wengine wanafanya ugaidi? wanyonge wengi huwa wanafanya ugaidi kudai haki zao zinazokandamizwa. Kuna magaidi ndani ya nchi tofauti zinazopinga utawala wa mabavu wa watawala mfano kule Ireland kuna kikundi cha kigaidi kinachopinga wao kutawaliwa na mfalme. Kuna ugaidi unaofanywa na watawala kwa kuwatia hofu wananchi wao!

  Akiwa kama mkurugenzi wa asasi inayosimamia maswala ya haki za kibinaadamu angesema na wale wanaoua wananchi wasio na hatia kwa ajili ya kujibufaisha wao kiuchumi kama kule ivory coast/almasi, Iraq/mafuta, Afghan/mapoda na kote kwenye aina ya utajiri uwe wa halili au haramu basi na wao wauwawe sio kuua kwingine kuwe kuzuri kwingine kuwe kubaya huyo atakuwa si mtetezi wa haki za binaadamu ila ni shetani.
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Umemjibu vizuri huyo kilaza!! Mitanzania bana, akili mgando kama nini! hawaelewi chochote kile wanachokisoma. Mada iko wazi kabisa -- lakini Ogah anakazania tu eti kwani Osama naye alitumia haki na sheria etc etc? Yaani huyu Ogah anataka LHRC nayo isimamie na kuafiki kama yale yafanywayo na magaidi -- kwamba mtu akiuwa naye auwawe bila mkondo wa sheria kufuatwa!

  Basi LHRC watutangazie sasa kuwa msimamo wao sasa hivi ni huo -- yaani ule wa kutokuwa na ulazima ya kuwapa watuhumia haki ya kujitetea nk nk.
   
 20. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #20
  May 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160

  You missing something somewhere my friend, I think you better get the concept first if what you are saying is the case then hata kina Bush na wao wanastahili kifo unajua wamekufa watu wangapi Vietnam, Iraq, Somalia, Afghanstan na kwingeneko? na mauaji hayo yamefanywa na kusimamiwa na Serikali ya Amerika! Ugaidi una maana pana unaweza ukawa Ugaidi wa Taifa moja kulikandamiza taifa jingine au wa kikundi kukandamiza watu fulani fulani. Ugaidi huo huo unaweza ukafanywa na utawala dhidi ya raia zake.

  Ifike sehemu tuone kwa jicho la tatu kuwa OBL kuuliwa sio dawa ila dawa wanyonge wapewe haki zao wenye mafuta waachiwe mafuta yao na wenye almasi waachiwe almasi zao si mnajua ya Savimbi?

  Asanteni sana.
   
Loading...