Wakati mheshimiwa rais anazindua nyumba za NHC Kibada alizungumzia kuhusu riba za mabenki kuwa kubwa hivyo kuyataka mabenki hayo kupunguza riba zinazotozwa kwenye mikopo inayotolewa. Kwa uelewa wangu ni kuwa hapa nchini hakuna sheria kuhusu riba zinazotozwa. Hivyo badala ya kuyataka mabenki ya punguze riba basi kama serikali ina nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi wake basi kupitia BOT ije na sheria ya kudhibiti riba, iwe ndogo itakayowezesha wafanya biashara na watumishi kuweza kupata mikopo yenye riba nafuu. Ni hayo, nawasilisha tafadhali.