Kauli ya mheshimiwa rais kuhusu riba za mabenki

nlambaa

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
361
0
Wakati mheshimiwa rais anazindua nyumba za NHC Kibada alizungumzia kuhusu riba za mabenki kuwa kubwa hivyo kuyataka mabenki hayo kupunguza riba zinazotozwa kwenye mikopo inayotolewa. Kwa uelewa wangu ni kuwa hapa nchini hakuna sheria kuhusu riba zinazotozwa. Hivyo badala ya kuyataka mabenki ya punguze riba basi kama serikali ina nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi wake basi kupitia BOT ije na sheria ya kudhibiti riba, iwe ndogo itakayowezesha wafanya biashara na watumishi kuweza kupata mikopo yenye riba nafuu. Ni hayo, nawasilisha tafadhali.
 

katalina

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
262
0
Wewe huwajui wanasiasa wanapokuwa kwenye majukwaa mbele ya wapiga kura, waweza kutoa kauli kuamrisha mvua kunyesha muda huohuo wakati wakijua hawana uwezo huo! That was a polical statement!
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
2,000
Kiwango cha riba kinaendana na kiasi cha risk inayochukuliwa na bank kutoa mikopo. Nchi kama Tanzania ambayo life expectancy ni ndogo na wakopaji wengi hushindwa kumalizia mikopo yao ndio inalazimu bank kuwa na kiasi kikubwa cha riba. Kimsingi hakuna sheria inayoweza kuset kiasi cha riba kwa sababu principally riba inatakiwa kuwa set na forces of demand and supply na forces of market competition. Kama serikali inaona kutoa riba ndogo inawezekana na faida ikawepo basi kupitia wizara ya fedha wafanye hivyo au waanzishe bank au wakopeshe pesa zao kupitia bank. Biashara na siasa ni vitu viwili tofauti...
 

hekimatele

JF-Expert Member
May 31, 2011
9,898
2,000
Alichosema Baba Mwanaasha ni sawa na kujikosha tu. Wao kwanza si watumiaji wa hiyo mikopo. Kama ni wateja wa benki basi huduma kubwa wanayotumia ni kuweka (saving)
Enewei, tukirudi kwenye mada utakuta BoT hawawezi kuregulate kwa kiasi kikubwa cha kuwafanya commercial banks wapunguze sana riba. It has a ripple effect in their marginal profit.
I don't think they are ready for that.


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom