Kauli ya Mh. Membe mgogoro wa mpaka Malawi

Kauli ya Mh. Membe mgogoro wa mpaka Malawi

omujubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Posts
4,444
Reaction score
2,703
Wakuu hii iko kwenye 'twitter' ya waziri wa mambo ya nje Mh. Benard Membe. Naomba tusaidiane mawazo na michango juu ya kauli hii. Je kunaweza kuwa na madhara yoyote kidiplomasia?

Bernard Membe ‏@BernardMembe 2h Serikali ya Malawi iache kutapatapa. Waheshimu Makubaliano yetu ya kuliachia jopo la usuluhishi la SADC lifanye kazi yake

Retweeted by Jakaya Kikwete
 
Isije ikawa Tanzania inafanya Haya kwa nia ya makusudi ya kuwa provoke watu wa Malawi. Maana Hawa watu wa CCM wanaweza kukushangaza wakati mwingine
 
I am totally lost! Ndilo tamko rasmi la serikali?
 
Isije ikawa Tanzania inafanya Haya kwa nia ya makusudi ya kuwa provoke watu wa Malawi. Maana Hawa watu wa CCM wanaweza kukushangaza wakati mwingine
ndio maana imenishtua kidogo maana Wamalawi wanatushutumu kuwa tumewazunguka wakati suluisho likiendelea.
 
Wakuu hii iko kwenye 'twitter' ya waziri wa mambo ya nje Mh. Benard Membe. Naomba tusaidiane mawazo na michango juu ya kauli hii. Je kunaweza kuwa na madhara yoyote kidiplomasia?

Madame Banda kadeclare wazi hataki usuluhishi wa maraisi wastaafu anaipeleka issue The Hague!
 
Kichwa cha habari hovyo, MGOGOLO ndio kitu gani? Hebu na tuache ujinga, kiingereza broken, na kiswahili nacho tujifanye hatujui.

Mimi sioni kauli tata hapo, kutapatapa sio tusi na Malawi wakiwa na akili zao timamu hawana sababu ya kufanya vita katika hatua hizi za awali.
 
kauli iko sawa. ikiwa mnakubaliana jambo halafu baadae unakataa na kutafuta njia nyingine tena bila kulirudisha kwa wale mliokubaliana ni kutapatapa. Hata mimi naona malawi inatapatapa kwenye hili.
 
I am totally lost! Ndilo tamko rasmi la serikali?

Sio rasmi ila ni tamko la Serikali! Hata hivyo naona halijakaa vizuri, limekaa kimipasho zaidi, busara zaidi inahitajika!
 
Nyerere ametuachia urithi wa majungu tuu na uvamizi wa nchi za watu.
 
Madame Banda kadeclare wazi hataki usuluhishi wa maraisi wastaafu anaipeleka issue The Hague!

The Hague! Anyway, kama UN itaamua kwa kuwapa ziwa lote Malawi kwa kutumia Heligoland - Zanzibar Treaty, tutarejda na kudai kufutwa kwa mataifa ya Rwanda na Burundi kwani mkataba huo unatambua eneo hilo ni sehemu ya Tanganyika. Kagame na Nkurunzinza wanakuwa wakuu wa mikoa ya Rwanda na Burundi mtawalia.
 
Nyerere ametuachia urithi wa majungu tuu na uvamizi wa nchi za watu.

hahaaaa!

jamani bernad na jakaya nao ni watu pia. sio kila kitu wanachokiandika wanakiandika kama waziri au rais. tuwape uhuru kama waTz wengine.
 
Wakuu hii iko kwenye 'twitter' ya waziri wa mambo ya nje Mh. Benard Membe. Naomba tusaidiane mawazo na michango juu ya kauli hii. Je kunaweza kuwa na madhara yoyote kidiplomasia?
tatizo wamalawi wana documents za gavana wa tanganyika kumkabidhi ziwa nyasa gavana wa malawi-nyasaland.sisi tanzania hatuna???utatweet sana bila mafanikio
 
Ili kukaa vizuri kwenye meza ya majadiliano ni vema kukafanyika uhakiki wa uhamiaji kwa kuwa yawezekana hata wale

wanaolizunguka ziwa Nyasa wakawa si watanzania ama wakawa na uraia wa nchi mbili ambao wanaweza kuutumia vibaya

kwa maslai yao binafsi.
 
Thanks mkuu kwa kutukumbusha kuhusu mikoa yetu ya Rwanda na Burundi
The Hague! Anyway, kama UN itaamua kwa kuwapa ziwa lote Malawi kwa kutumia Heligoland - Zanzibar Treaty, tutarejda na kudai kufutwa kwa mataifa ya Rwanda na Burundi kwani mkataba huo unatambua eneo hilo ni sehemu ya Tanganyika. Kagame na Nkurunzinza wanakuwa wakuu wa mikoa ya Rwanda na Burundi mtawalia.
 
Kuna tatizo gani kwenye hiyo tweet? Kusema serikali ya malawi iache kutapatapa, na iheshimu makubaliano ya SADC?
You are too damn sensitive.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
ZIWA NYASA ni letu wote no matter what....lakini usuluhishi kuwa chini ya Msumbiji, Mpwa na binamu wa Tanzania, hakika Malawi hawataweza kutendewa haki!! Nilitarajia Chisano angekataa kuwa Msuluhishi! So, Malawi wameshapoteza haki wanayotaka the time walipokubali Mozambique kuwa Hakimu!
 
Back
Top Bottom