Kauli ya Membe kuhusu NTC ina utata

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
0
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesisitiza msimamo wa Tanzania wa kutotambua Baraza la Mpito la Libya (NTC) na badala yake amelitaka litekeleze mpango wa amani wa Libya uliokubaliwa na Umoja wa Afrika (AU). --HabariLeo.

My take:
Kama Membe halitambui baraza la mpito kwa nini basi analitaka litekeleze mpango wa amani hiyo authority litatoa wapi, kwa kulitaka litekeleze ina maana analitambua kuwa lipo. Kama halitambui ina maana bado anaitambua serikali ya Gaddafi kwa vile nchi haitabaki vacuum bila utawala kwa nini basi asiiambie serikali ya Gaddafi anayoitambua itekeleze huo mpango instead analiambia baraza asilolitambua litekeleze? Haiingii akilini.
 

Prodigal Son

JF-Expert Member
Dec 9, 2009
999
1,000
Subiri SA wakishalitambua na yeye
atawatangazia analitambua, kutambua au kutolitambua hakutaipunguzia wala kuiongezea Tanganyika kitu chochote
as if hatuna kampuni za kwenda kuwaomba NTC kandarasi za kuijenga upya Libya, kama mafuta Total, BP ambao tayari wameshahakikishiwa share watatuchimbia na kutuletea

Tanganyika ni ile ya wakina Nyerere, ndio walikuwa wakisema kitu sio Africa tu dunia nzima ilikuwa inasikiliza, kama wajanja wanaweza mnunulia Baba wa kaya vinguo unategemea nini. kwenye medani ya kimataifa Tanganyika inaishia hapo uwanja wa ndege tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom