Kauli ya Mchungaji kuelekea Uchaguzi 2015

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
4,526
Reaction score
1,552
Uchaguzi 2015

Itikadi kuu ya kitaifa iwe ni kujenga upya Tanzania, kama Taifa huru yenye kuzingatia vipaumbele vifuatavyo: Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uwajibikaji, Uadilifu Uimara na Umoja wa Kitaifa

Wenye Nia Urais, Ubunge, Udiwani wapimwe si kwa kauli zao tuu, bali kwa matendo yao kama wanaweza kujenga: Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uadilifu, Uwajibikaji, Uimara na Umoja

Tusipime wagombea kwa utamu na ntiririko wa ufahamu wa kuongea au maneno tunayotaka kusikia, tusikubali kuwapa dhamana na majukumu makubwa kutonkana na umahiri wa kampeni zao, kujaa kwa umati wa wafuasi au vilio vyao vya kulilia dhamana ya kumkomboa Mtanzania.

Tukague Ufanisi wa utendaji wa wagombea katika miaka yao ya uwakilishi na kulitumikia Taifa na kuzioanisha na kauli walizozitoa miaka hiyo ya nyuma. Je tuwape dhamana na kwaamini wataweza sasa? Kama walishindwa kujenga mfumo fanisi wa maendeleo na uwajibikaji katika ngazi za wilaya, je kwenye duru za Kitaifa watatuaminishaje wana uwezo kufanikiwa?

Tuhoji uimara wao na utendaji wao mpaka sasa katika miaka mitano iliyopita, wamewafanyia nini cha maendeleo wananchi wachache waliowapa dhamana ya uwakilishi na uongozi? Je, kama katika wilaya na majimbo, wamepata matatizo ya ushawishi kustawisha jamii iliyo imara na yenye maendeleo endelevu na si ya maneno,tuaminije wanaweza kuongoza Taifa zima?

Tuhoji umadhubuti na uimara wa wagombea kusimamia haki, kujenga demokrasia ya kweli, kukubali upinzani, kukemea na kuwajibisha uhujumu. Je, matendo yao yameonyesha msimamo unaoeleweka kujenga jamii yenye demokrasia ya kweli yenye ushirikishi?

Tuhoji, je wamekuwa wawazi bila woga kupiga vita uhujumu ambao una sura mbali mbali kama uvivu, uzembe, matumizi mabaya ya dhamana na fedha, uhujumu, rushwa na uonevu?

Uimara wa Tanzania na maendeleo yake ya kijamii, kiuchumi na kisiasa si wingi wa rasilimali na ahadi za kuneemeka bila kuzingatia: Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uadilifu, Uwajibikaji na Umoja katika kujenga Uimara wa Taifa na Utaifa!

Taifa letu, haliwezi kupiga hatua mbele kushinda vita dhidi ya Ujinga, Umasikini, Maradhi na Uhujumu bila kuzingatia malengo haya ya msingi.

Hatutaweza futa ujinga na maradhi tusipothamini Utu, Uzalendo, Uadilifu, Uwajibikaji, Ufanisi na Umoja.

Ni kujidanganya eti utajiri wa rasilimali na mapato ya uzalishaji yatutasaidia kutatua matatizo ya Taifa huku nguzo kuu na tunu za Utaifa wetu zinapuuziwa na kutokupewa kipaumbele kama dira iliyo kuu ya kujenga jamii shirikishi.

Vita kuushinda Uhujumu havina faida kwa Umoja hatuna Uzalendo, Utu, Ufanisi, Uwajibikaji na Uimara kupambana na ufisadi, rushwa, ujangili, utegemezi na utovu wa nidhamu!

Haitawezekana kufuta Umasikini pasipo kuwa na kipumbele cha Uzalendo, Utu, Ufanisi, Uwajibikaji, Uadilifu au Umoja pamoja na rasilimali zote tulizonazo na kujitangaza kwa majisifu.

Tuliposema ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi Siasa Safi na Uongozi Bora, ni wakati huu ambapo tunahitaji kuchagua siasa safi na uongozi bora ulio wazi nawenye dhamira ya kulitumikia Taifa kwa dhati kuzingatia vigezo hivi vya : Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uadilifu, Uimara, Uwajibikaji na Umoja.

Watanzania tuachane na mazoea ya kuamini maneno ya Wanasiasa ambao hawajengi Umoja au Ushirikishi kutokana na Amani tuliyonayo.

Tanzania na Watanzania ni lazima tujisahihishe mwaka huu wa uchaguzi kwa kutoa dhamana kwa watu wenye hekima, busara, ujasiri na uimara wa kutafakari, kufanya kazi na kufanya maamuzi yenye matokeo chanya: bora na endelevu. Tuwape dhamana watu ambao ni wepesi kujisahihisha na kufanyia kazi mapungufu yao.

Watanzania tukatae kupewa viongozi wasiojiheshimu, waongo, wazandiki, wanafiki na wenye tamaa na uchu wa madaraka na mamlaka. Hawatufai Ng'o!

Tanzania itajengwa na kuongozwa na viongozi waadilifu, wasikivu, wavumilivu, wachapa kazi wenye kukubali kukosolewa na kufanyia kazi kwa moyo maoni tofauti na mawazo yao.

Nami natangaza rasmi: Nia yangu ni kuleta na kupata Uongozi utakaoongoza kuzingatia: Uzalendo, Utu, Uadilifu, Ufanisi, Uwajibikaji, UImara na Umoja kwa Taifa letu na Watanzania wote kwa ujumla bila kujali tofauti zozote zile!
 
Karibu sana Rev, baada ya kimya kingi.
 
Uchaguzi 2015
Tanzania itajengwa na kuongozwa na viongozi waadilifu, wasikivu, wavumilivu, wachapa kazi wenye kukubali kukosolewa na kufanyia kazi kwa moyo maoni tofauti na mawazo yao.
Mkuu tumekusikia, na katika sifa hizo zote, kwa bahati nzuri yupo mtangaza nia mmoja tuu aliyezifika na kuzipitiliza, sio tuu kwa kukubali kukosolewa pekee, bali kukubali kuzibeba dhambi za wengine na kukaa nazo pembeni ili kuliepushia taifa na shari, huku ni kujitoa mwenyewe nafsi yako kwa ajili ya taifa lako!.

Kwenye hilo la uadilifu, mtu mwenye karama ya utajiri, anayetoa sehemu za utajiri wake na kuwagawia masikini, kuwagawia wengine, ni mtu mwenye baraka anayestahili kukabidhiwa nchi ili sasa awagawiye wote!.

Mtu wa aina hii ndiye rais wetu October 25!.

Pasco
 
Pasco, kwanini kuzunguka mbuyu? Sema ni Lowassa. Lakini labda niulize swali moja dogo, kwa nini Lowassa anatumia nguvu nyingi sana kutaka kwenda ikulu? Na huo utajiri wake unaosema anawagawia wengine unaweza kutwambia kwa kifupi aliupataje?

Tiba
 
Tiba, ma GT hawataji majina, wao wanadeal na the ideas tuu!. Hatumii hoja za nguvu kuisaka ikulu, bali ni nguvu za hoja ndizo zinazowashawishi Watanzania kuwa ikulu yetu inamuhitaji mtu mwenye sifa hizi!.

Utajiri wake tumesema zaidi ya mara 100 humu, yeye hana utajiri wowote zaidi ya wale ngo'ombe 1000 alioachiwa urithi!. Pesa zote zinazotumika kumpeke ikulu sio fedha zake bali huchangiwa na marafiki zake!.

Naamini sasa Tiba, tutakuwa tumeelewana!.

2015 Tanzania inahitaji mtu anayekerwa kwa dhati na umasikini wa Tanzania na Watanzania!.

Pasco, umesema vizuri kwamba hapa ni sehemu ya GT. Sasa kweli unategemea GT ambaye yupo objective anunue hicho ulichoandika hapa. Kwamba EL hana utajiri wowote mbali ya mifugo 1, 000 ya urithi? Na hao marafiki zake wanamchangia ili aende ikulu halafu? Huyo aliyemchangia ili aende ikulu kesho akifanya ufisadi EL atakuwa na ubavu wa kumkemea huyo? Na huyu EL anachangiwa sana na marafiki zake mpaka walimchangia akanunua nyumba huko London. Aha marafiki zake wanampenda kweli.

The bottom line is EL is not clean and he is not state house/presidential material of our era.

My Sister Tiba,, hapa sasa ndipo lazima uukubali ukweli mchungu, kuwa huyu ndie rais wako ajaye!. Ni kweli hao ngombea ndio utajiri wake pekee alioanza nao maisha ila kwa vile huyu ni mtu wa Mungu, hivyo ana upako fulani kama wa Midas, everything he touches turn to gold!. Alipokuwa mgurugenzi wa AICC neema ikamwangukia, akaanza kumiliki land Arusha, Mungu akamuangazia akapewa wizara ya Ardhi, enzi hizo viwanja vikitolewa bure tena prime areas!, akajenga zile nyumba akakodisha mabalozi faida akaitumia kama mtaji wa Alfa!. Mungu akamuangazia zaidi akapewa wizara ya Mifugo, Ranchi ya zaita zikauzwa kwa bei ya bure na yeye uwezo alikuwa nao hivyo akanunua!. Mungu akambariki zaidi na kumfanya akawa Waziri Mkuu wetu lakini katika maandalizi ya kumfanya awe rais wetu, Mungu akampitisha kwenye majaribu ya Richmond, ili iwe kama kawaida baada ya mateso na kifo, huja ufufuko na uzima wa milele, sasa hii ndio safari ya kukitwaa kile kiti alitayarishiwa na Mungu mwenyewe, au hukumsikia TB Joshua?!.

Kilichoanzisha Alfa ni mtaji kutokana na vitega uchumi vyake, hata hizo Nyumba London ni faida tuu kutoka vitega uchumi vyake!.

Kwa vile ni mtu wa Mungu na mwenye upako wa neema, hao marafiki zake wanaomchangia wamejikuta wanabarikiwa sana hivyo kuchanga zaidi na zaidi kama sadaka tuu makanisani, hawasubiri kuja kulipwa baadae ila kila ukitoa tuu unajikuta unazidishiwa mara sabaini fii sabaa!.

Hiyo the bottom you are very right, EL is not clean!, yae he is not, hata JK was not clean, but he was!, hata CCM is not clean, but it is!, hata YULE aliyekuja kuukomboa ulimwengu huu, aliisha sema hakuja kwa ajili ya wakamilifu!, alikuja kwa ajili ya hao hao ambao sio clean!. Na akasema "Wainuliwe wote wenye mizigo waje kwa YEYE wapumzishwe!", ndio maana hata lile zigo la Richmond, amelibeba tuu sio lake, na sasa anasubiri kuinuliwa ili apumzishwe kule juu!.

Kama JK amweza kuwa presidential material na ametutawala miaka hii kumi, EL ni 100 times better, ataiinua hii nchi kutoka huku kwenye vumbi na majajala na kutupeleka kwenye ile nchi ya ahadi, mabomba mchi nzima yatatoa maziwa na asali!.

Hata alipokuja YEYE, mwanzo alikataliwa hivi hivi mnavyotaka kumkataa huyu mtu!, hivyo sasa YEYE aliyemwandikisha atajidhihirisha utukufu wake kwenu, kwa "lile jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!",

Amesema "Huu ni mwamba na juu ya mwamba huu, nitalifa taifa langu!".

Just wait and see!.

Pasco
 
Mkuu tumekusikia, na katika sifa hizo zote, kwa bahati nzuri yupo mtangaza nia mmoja tuu aliyezifika na kuzipitiliza, sio tuu kwa kukubali kukosolewa pekee, bali kukubali kuzibeba dhambi za wengine na kukaa nazo pembeni ili kuliepushia taifa na shari, huku ni kujitoa mwenyewe nafsi yako kwa ajili ya taifa lako!.

Kwenye hilo la uadilifu, mtu mwenye karama ya utajiri, anayetoa sehemu za utajiri wake na kuwagawia masikini, kuwagawia wengine, ni mtu mwenye baraka anayestahili kukabidhiwa nchi ili sasa awagawiye wote!.

Mtu wa aina hii ndiye rais wetu October 25!.

Pasco

Lakini utajiri wenyewe usiwe wa kutiliwa hata chembe ya shaka.
Asiwe tajiri aliyewaibia hao "anaojifanya " kuwagawia ili apate uongozi na aje aibe zaidi.
Asiwe "tajiri " anaejifanya kapewa hela na "marafiki " wasio na majina wala anuani.
Tanzania ni nchi tajiri. Kinachotakiwa ni kiongozi wa kuusambaza utajiri huo kwa watanzania na sio kujitajirisha yeye!
 
Mkuu Sibo, haya usemayo ni ukweli kabisa!, hili la hela za marafiki ni kama sadaka, au kanisa lako huwa linajua nani katoa sadaka kiasi gani?!, mnapotangaziwa sadaka huwa mnaambiwa na waliotoa?!, bado hao ndio hao marafiki zake, nyie ni kupokea tuu kama sadaka bila kujali zimetoka wapi na zimechangwa na nani!.

Ni kweli Tanzania ni nchi tajiri ndio maana 2015 tunataka rais tajiri aliyeshajitosheleza na utajiri wa ziada kugawa kwa masikini, hatutaki tena rais masikini atakayeanza kwanza kwa kujitajirisha yeye, ndipo aje kuwakumbuka wananchi masikini!.

Huyu 'jamaa yangu' atosha kila idara, ameonyesha kila uwezo na anakidhi kila kigezo!.

We have the one and only!.

Pasco
 
My Sister Tiba,, hapa sasa ndipo lazima uukubali ukweli mchungu, kuwa huyu ndie rais wako ajaye!. Ni kweli hao ngombea ndio utajiri wake pekee alioanza nao maisha ila kwa vile huyu ni mtu wa Mungu, hivyo ana upako fulani kama wa Midas, everything he touches turn to gold!. Alipokuwa mgurugenzi wa AICC neema ikamwangukia, akaanza kumiliki land Arusha, Mungu akamuangazia akapewa wizara ya Ardhi, enzi hizo viwanja vikitolewa bure tena prime areas!, akajenga zile nyumba akakodisha mabalozi faida akaitumia kama mtaji wa Alfa!. Mungu akamuangazia zaidi akapewa wizara ya Mifugo, Ranchi ya zaita zikauzwa kwa bei ya bure na yeye uwezo alikuwa nao hivyo akanunua!. Mungu akambariki zaidi na kumfanya akawa Waziri Mkuu wetu lakini katika maandalizi ya kumfanya awe rais wetu, Mungu akampitisha kwenye majaribu ya Richmond, ili iwe kama kawaida baada ya mateso na kifo, huja ufufuko na uzima wa milele, sasa hii ndio safari ya kukitwaa kile kiti alitayarishiwa na Mungu mwenyewe, au hukumsikia TB Joshua?!.

Kilichoanzisha Alfa ni mtaji kutokana na vitega uchumi vyake, hata hizo Nyumba London ni faida tuu kutoka vitega uchumi vyake!.

Kwa vile ni mtu wa Mungu na mwenye upako wa neema, hao marafiki zake wanaomchangia wamejikuta wanabarikiwa sana hivyo kuchanga zaidi na zaidi kama sadaka tuu makanisani, hawasubiri kuja kulipwa baadae ila kila ukitoa tuu unajikuta unazidishiwa mara sabaini fii sabaa!.

Hiyo the bottom you are very right, EL is not clean!, yae he is not, hata JK was not clean, but he was!, hata CCM is not clean, but it is!, hata YULE aliyekuja kuukomboa ulimwengu huu, aliisha sema hakuja kwa ajili ya wakamilifu!, alikuja kwa ajili ya hao hao ambao sio clean!. Na akasema "Wainuliwe wote wenye mizigo waje kwa YEYE wapumzishwe!", ndio maana hata lile zigo la Richmond, amelibeba tuu sio lake, na sasa anasubiri kuinuliwa ili apumzishwe kule juu!.

Kama JK amweza kuwa presidential material na ametutawala miaka hii kumi, EL ni 100 times better, ataiinua hii nchi kutoka huku kwenye vumbi na majajala na kutupeleka kwenye ile nchi ya ahadi, mabomba mchi nzima yatatoa maziwa na asali!.

Hata alipokuja YEYE, mwanzo alikataliwa hivi hivi mnavyotaka kumkataa huyu mtu!, hivyo sasa YEYE aliyemwandikisha atajidhihirisha utukufu wake kwenu, kwa "lile jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!",

Amesema "Huu ni mwamba na juu ya mwamba huu, nitalifa taifa langu!".

Just wait and see!.

Pasco

Nina ona hapa umezungumzia kitu ambacho hakipo Tb Joshua hakutoa unabii kuwa lowasa atakuwa rais wa taifa hili na Kama unaudhibitisho uweke hapa coz niliangalia that service.
Mungu hakupitishi kwenye jaribu LA uwizi hata siku moja naomba usiyatumie maandiko vibaya mwisho tuonekane wakristo wote hatuna kweli ndani yetu.

Mungu ametupa utashi wa kupambanua mambo hapa nasema kweli maana kweli itawaweka huru watanzania wenzengu wanaolipenda taifa hili kwa dhati....Mungu haungi mkono uovu wowote ule wala hawaungi mkono waovu ...aliyekuja kwa waliopotea ili waache ovu, waache ufisadi, waache rushwa,

Sio kwamba lunch za taifa ziliuzwa kwa bei chee Bali walijiuzia kwa bei raisi kwa sababu ya ubinafsi wao nakumissuse madaraka waliyopewa, Kama waziri unalipenda taifa lako huwezi kukubali Mali ya uma iuzwe pasipo masirahi.

Sio kwamba migodi ya kiwira iliuzwa kwa bei raisi Bali walijiuzia kwa bei raisi kwa kumissuse madaraka waliyopewa na wananchi.

Je Kama lowasa alikuwa waziri wa mifugo aliweza kutothamini utaifa kwanza akaamua kujiuzia lunch kwa bei raisi, je akipewa urais atawezaje kusimamia rasirimali zetu?

Watu wanashadadia tu Mara anamaamuzi magumu mala nini hebu tumpime kwa facts na vidhibitisho wizara zote alizopita amefanya kitu Gan extraordinary mpaka tuseme anaweza? ninaweza kumsifia Kama nitapata uchambuzi wa matatizo sugu ya wananchi kwenye kila wizara aliyopita alivyoyatatua maana mpaka sasa sijaona.

Nyie endeleeni kumpigia debe lakini nataka niwaambie kuwa el hawezi kupambana na changamoto kubwa za ufisadi nk coz angalia marafiki wanaomchangia pesa wote mafisadi na wamekula jasho LA wanyonge wa taifa hili mfn wa marafiki zake change,rostam Aziz, tibaijuka nk
Mungu wangu atawaadhibu watu hawa na kuwakatilia mbali kabisa
 
Nina ona hapa umezungumzia kitu ambacho hakipo Tb Joshua hakutoa unabii kuwa lowasa atakuwa rais wa taifa hili na Kama unaudhibitisho uweke hapa coz niliangalia that service.

Mungu wangu atawaadhibu watu hawa na kuwakatilia mbali kabisa
Alitoa na uthibitisho upo!, ila Mungu huwakatilia mbali na kuwaadhibu wale wote wanaosema mabaya kuhusu watu wake!.

Hala hala angalia usije ukawa wewe!.

Na TB JOSHUA kama mtume aliye tumwa na lucifer na akamtabilia neema ya urais mtu yule.
maana siku hizi za mwisho wamejaa manabii wengi wa uongo ambao dhambi zao ni mfano wa YUDA ESKARIOTI.
Hata miili yao itawaka moto kabla udongo hauja umeza kuwa vumbi!
wao watalaaniwa na hata wawaaminio pia nao wamelaaniwa.
 
Pasco umefafanua vizuri sana:

Alipokuwa mkurugenzi AICC akajimilikisha "Land"

Alipokuwa waziri wa ardhi akajiuzia nyumba na viwanja bei chee maeneo muhimu Dar (anapangisha mabalozi).

Alipokuwa waziri wa mifugo akajiyzia Ranchi za taifa kwa bei poa.

Alipokuwa waziri mkuu apihusishwa na kasha ya Richmond akalazimika kujiuzuru.

Je, akiwa RAIS wa JMT atajiuzia nini? Watch out!!!

TAMAA YA FISI..
 
Pesa zote zinazotumika kumpeke ikulu sio fedha zake bali huchangiwa na marafiki zake!

Hey Pasco,a bad joke eh!
Waroma walisema tangu kale "fear the Greeks and their gifts"
Lowasa kujivunia marafiki wanaofanya kila mbinu kum -instal ikulu ni fedheha kwake na watanzania wote.
 
Uchaguzi 2015

Itikadi kuu ya kitaifa iwe ni kujenga upya Tanzania, kama Taifa huru yenye kuzingatia vipaumbele vifuatavyo: Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uwajibikaji, Uadilifu Uimara na Umoja wa Kitaifa

Wenye Nia Urais, Ubunge, Udiwani wapimwe si kwa kauli zao tuu, bali kwa matendo yao kama wanaweza kujenga: Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uadilifu, Uwajibikaji, Uimara na Umoja

Tusipime wagombea kwa utamu na ntiririko wa ufahamu wa kuongea au maneno tunayotaka kusikia, tusikubali kuwapa dhamana na majukumu makubwa kutonkana na umahiri wa kampeni zao, kujaa kwa umati wa wafuasi au vilio vyao vya kulilia dhamana ya kumkomboa Mtanzania.

Tukague Ufanisi wa utendaji wa wagombea katika miaka yao ya uwakilishi na kulitumikia Taifa na kuzioanisha na kauli walizozitoa miaka hiyo ya nyuma. Je tuwape dhamana na kwaamini wataweza sasa? Kama walishindwa kujenga mfumo fanisi wa maendeleo na uwajibikaji katika ngazi za wilaya, je kwenye duru za Kitaifa watatuaminishaje wana uwezo kufanikiwa?

Tuhoji uimara wao na utendaji wao mpaka sasa katika miaka mitano iliyopita, wamewafanyia nini cha maendeleo wananchi wachache waliowapa dhamana ya uwakilishi na uongozi? Je, kama katika wilaya na majimbo, wamepata matatizo ya ushawishi kustawisha jamii iliyo imara na yenye maendeleo endelevu na si ya maneno,tuaminije wanaweza kuongoza Taifa zima?

Tuhoji umadhubuti na uimara wa wagombea kusimamia haki, kujenga demokrasia ya kweli, kukubali upinzani, kukemea na kuwajibisha uhujumu. Je, matendo yao yameonyesha msimamo unaoeleweka kujenga jamii yenye demokrasia ya kweli yenye ushirikishi?

Tuhoji, je wamekuwa wawazi bila woga kupiga vita uhujumu ambao una sura mbali mbali kama uvivu, uzembe, matumizi mabaya ya dhamana na fedha, uhujumu, rushwa na uonevu?

Uimara wa Tanzania na maendeleo yake ya kijamii, kiuchumi na kisiasa si wingi wa rasilimali na ahadi za kuneemeka bila kuzingatia: Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uadilifu, Uwajibikaji na Umoja katika kujenga Uimara wa Taifa na Utaifa!

Taifa letu, haliwezi kupiga hatua mbele kushinda vita dhidi ya Ujinga, Umasikini, Maradhi na Uhujumu bila kuzingatia malengo haya ya msingi.

Hatutaweza futa ujinga na maradhi tusipothamini Utu, Uzalendo, Uadilifu, Uwajibikaji, Ufanisi na Umoja.

Ni kujidanganya eti utajiri wa rasilimali na mapato ya uzalishaji yatutasaidia kutatua matatizo ya Taifa huku nguzo kuu na tunu za Utaifa wetu zinapuuziwa na kutokupewa kipaumbele kama dira iliyo kuu ya kujenga jamii shirikishi.

Vita kuushinda Uhujumu havina faida kwa Umoja hatuna Uzalendo, Utu, Ufanisi, Uwajibikaji na Uimara kupambana na ufisadi, rushwa, ujangili, utegemezi na utovu wa nidhamu!

Haitawezekana kufuta Umasikini pasipo kuwa na kipumbele cha Uzalendo, Utu, Ufanisi, Uwajibikaji, Uadilifu au Umoja pamoja na rasilimali zote tulizonazo na kujitangaza kwa majisifu.

Tuliposema ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi Siasa Safi na Uongozi Bora, ni wakati huu ambapo tunahitaji kuchagua siasa safi na uongozi bora ulio wazi nawenye dhamira ya kulitumikia Taifa kwa dhati kuzingatia vigezo hivi vya : Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uadilifu, Uimara, Uwajibikaji na Umoja.

Watanzania tuachane na mazoea ya kuamini maneno ya Wanasiasa ambao hawajengi Umoja au Ushirikishi kutokana na Amani tuliyonayo.

Tanzania na Watanzania ni lazima tujisahihishe mwaka huu wa uchaguzi kwa kutoa dhamana kwa watu wenye hekima, busara, ujasiri na uimara wa kutafakari, kufanya kazi na kufanya maamuzi yenye matokeo chanya: bora na endelevu. Tuwape dhamana watu ambao ni wepesi kujisahihisha na kufanyia kazi mapungufu yao.

Watanzania tukatae kupewa viongozi wasiojiheshimu, waongo, wazandiki, wanafiki na wenye tamaa na uchu wa madaraka na mamlaka. Hawatufai Ng'o!

Tanzania itajengwa na kuongozwa na viongozi waadilifu, wasikivu, wavumilivu, wachapa kazi wenye kukubali kukosolewa na kufanyia kazi kwa moyo maoni tofauti na mawazo yao.

Nami natangaza rasmi: Nia yangu ni kuleta na kupata Uongozi utakaoongoza kuzingatia: Uzalendo, Utu, Uadilifu, Ufanisi, Uwajibikaji, UImara na Umoja kwa Taifa letu na Watanzania wote kwa ujumla bila kujali tofauti zozote zile!

baadaya kukupa `like`ninachosema ndani ya ccm hatuwezi kumpata kiongozi wa namna hiyo maana angekuwepo kiongozi wa namna hiyo lazima angewakumbusha wezake. kiongozi wa namna hiyo atapatikana katika chama pinzani maana wao ndio kila siku tunawasikia wanayasema hayo, zote ni mashaidi tunawasikia bungeni lakini ccm wote hawataki kufuata wanaloambiwa, ukitaka mifano ya hayo nitakuambia
 
Alitoa na uthibitisho upo!, ila Mungu huwakatilia mbali na kuwaadhibu wale wote wanaosema mabaya kuhusu watu wake!.

Hala hala angalia usije ukawa wewe!.

Pasco

Yaaa sure endapo unamsema kwa kumsingia mtumishi wa bwana n kweli atakukatilia Bali...lakini Kama unamsema kwa ukweli hawezi

Yohana mbatizaji alimsema mtawala herode alipoa mke wa mdogo wake wala Bwana hakumkatilia mbali

Bwana alimkatilia mbali sauli alipo Fanya uovu

Bwana huwakatilia mbali watenda maovu na watu wote wanaounga uovu wa Kama ufisadi
Ninahakika sitakukuta mbinguni kwa hili unafanya LA kugeuza uongo na kuwa kweli.
 
Back
Top Bottom