Kauli ya Mbunge Lusinde: Wananchi watoana ngeu

Kauli ya Mbunge Lusinde: Wananchi watoana ngeu

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
13,647
Reaction score
21,264
Mbunge wa Mtera, Livingston Lusinde, juzi alisababisha mapigano yaliyojeruhi wapigakura wake kadhaa.

Baadhi ya wapigakura wake kumzomea wakipinga hoja zake alizokuwa akitumia kujinadi katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nkwenda wilayani Chamwino, mkoani Dodoma.

Mkutano uliondaliwa na serikali ya kijiji ili kumpa nafasi mbunge huyo kuzungumza na wananchi wake juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya kwa taktibani miaka minne na nusu.

Alianza kwa kueleza alivyo tumia fedha kutekeleza miradi ya barabara, zahanati, maji pamoja na mambo mengine ambayo yote alisema imegharimu zaidi ya Sh. milioni 400 na vile vile kujinadi kuwa yeye ndiye alileta mradi wa Tasaf na fedha zinazotumika ni za kwake.

Baada ya mbunge kueleza hivyo, kundi la wananchi walianza kuzomea na kupiga kelele kuwa mbunge anadanganya kwa kuwa hakuna miradi ambayo imetekelezwa katika kijiji hicho kwa kiasi cha fedha hizo na za Tasaf ni za serikali sio zake.

“Mbunge huyo ni uongo huwezi kutudunganya hakuna kitu kama hicho baaadhi ya sauti za wananchi zilisikika. Baadhi ya sauti hizo zilisema: ‘

“Mbunge hujafanya kitu, hii miradi sio wewe usindanye wananchi.”

Kutokana kelele hizo zilizodumu kwa zaidi ya dakika kumi na Lusinde kubaini hakuna ayemsikiliza, aliwaeleza wananchi kuwa wakae katika makundi mawili moja wanamuunga mkono na wasio muunga mkono.

“Naomba wale ambao tupo pamoja wakae kulia na wale ambao hatuko pamoja wakae kushoto ili kutambuane kwa vizuri zaidi,” alisema Lusinde.

Baada ya makundi hayo wawili kujitenga huku idadi kubwa ya wanawake ili wale wanaomuunga mkono na wanaume kubaki upande usio muunga mkoano, Lusinde aliwaamuru vijana wapatao 15 kuwashambulia watu wanaopingana naye.

“Sasa nyinyi kama mnajifanya ‘masteling’ basi mimi ni steling zaidi yenu sasa makomando wangu watawashughulikia, sisi tuko tayari hata kufa,” alisema Lusinde.

Baada ya kauli hiyo vijana hao walitoa fimbo na marungu na kuanza kuwashambulia wananchi na kusababisha watu wakaanza kukimbia ovyo na wengine kujificha majumbani kwa kujifungia milango kuhofia kipigo.

Mmoja wa majeruhi hao Yohana Mnyanyi, aliyeshonwa juzi saba, lisema alikuwa akitoka eneo ambalo walikuwa wakichimba kaburi akielekea nyumbani ndipo alipokuna na watu zaidi ya kumi wakiwa wamebeba fimbo na marungu wakikimbiza watu na kuwapiga.

“Mimi wakati nakuja nikakutano na watu wanakimbizana nikauliza kuwa jamii hii ni vita au kitu gani kabla sijamaliza nikapigwa fimbo nikakinga mkononi hapa nilipovimba, lakini pia nikapigwa ya pili kichwani hapa niliposhonwa nyuzi saba na kuaguka chini…lakini mbunge Lusinde naye alikuwepo akisema ngoja leo makomando wangu wafanye kazi yao tuheshimiane,” alisema Mnyanyi.

Saidi Elieza alisema pamoja na watu hao kutumia fimbo lakini pia mmoja wa waopambe wa Mbunge alikuwa ameshikilia panga akisema atayejifanya jeuri atamkata shingo yake.

Alisema kuwa mara baada ya vurugu hizo kuanza walianza kupigwa watu na cha kusikitisha zaidi hadi watu wenye matatizo ya akili walipigwa.

Mganga wa Zahanati ya Kijiji Cha Nkwenda, Elisha Chizuwa, alithibitisha kupokea watu watatu na kuwa wawili kati yao moja alishonwa nyuzi saba, mwingine tano na mwingine alimpatia matibabu ambapo akiwa ameumia ubavuni.
“Nilipatiwa taarifa na ofisa Mtendaji wa Kijiji aliniambia kuwa watu hao wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa mbunge,” alisema.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho Jonas Chitunga, pia alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kuiomba serikali kuongeza ulinzi wakati wa mikutano ya kisiasa.

Lusinde alipoulizwa alidai kuwa kuna watu waliokuwa wamenunuliwa pombe za kienyeji ili waharibu mkutano wake na kuwa waliwaomba watulie, lakini walikataa ndipo na wao wakaanza kuwapiga kwa kujihami.

Chanzo:
Nipashe
 
Siwezi kumlaumu Lusinde hata kidogo hapa ndio mwisho wa akili yake ilipogota.

Niliwashangaa sana wananchi wa Mtera na akili zao wakamchagua mbunge mhuni,asiye na elimu,asiye na maono ya dhamana aliyopewa,asiye akili.Sasa ndio mnavuna mlichopanda na bado ipo siku atawaambia mvue nguo zote....... Ndio mjue yeye ni nani.
 
Kama ushahidi upo kwa nini hakamatwi? Au mpaka yatokee mauaji kama Kiteto ndio mnaanza sijui tume sijui nini. Wakati mwingine kama mtu ana mshale wmtungue huyohuyo mchochezi
 
Siwezi kumlaumu Lusinde hata kidogo hapa ndio mwisho wa akili yake ilipogota.

Niliwashangaa sana wananchi wa Mtera na akili zao wakamchagua mbunge mhuni,asiye na elimu,asiye na maono ya dhamana aliyopewa,asiye akili.Sasa ndio mnavuna mlichopanda na bado ipo siku atawaambia mvue nguo zote....... Ndio mjue yeye ni nani.

“Sasa nyinyi kama mnajifanya ‘masteling’ basi mimi ni steling zaidi yenu sasa makomando wangu watawashughulikia, sisi tuko tayari hata kufa"Kibajaj
 
Hivi hili ni la kweli ama kuchafuana kwa ajili ya uchaguzi? Maana siku hizi kumezuka mambo ya ajabu, unakuta hadithi iko kwenye gazeti lakini ukifuatilia unakuta sio kweli ama imeandikwa kwa kutiwa chumvi sana mpaka ukweli wake unatia shaka. Na kama ni kweli na watu tunajadili kirahisi, hii ni hatari ya dhahiri ambayo haifai kufumbiwa macho kwani iwapo leo huyo Lusinde kafanya hivyo na hakuna hatua stahiki zinachukuliwa, mjue kila mtu ana nyongo na kuna watu wanajua kuiga mambo mabaya tu. Inaweza kutokea watu wa aina hiyo na wakazua balaa kubwa. Mchelea mwana kulia ... Nadhani ni wakati muafaka wa vyombo vya dola kufutatilia hili na kuchukua hatua stahiki bila kujali ni wa chama tawala kwani siku pakiharibika mtangoja wazungu waje wagawe misaada na mpatinishi wao kuja hapa.
 
Lusinde amepoteza mvuto kabisa kwa wananchi wa Mtera!! anachokifanya Lusinde hivi sasa ni kutembea na wapambe wake kusulubu na kuwapiga wote anaowahisi ni wapinzani wake!!!

Viongozi wa ngazi zote wanafahamu hilo na pia polisi wanafahamu lakini wanashindwa kuchukua hatua stahili!!
 
Back
Top Bottom