Kauli ya Mbowe ilaaniwe na wapenda amani

Kauli ya Mbowe ilaaniwe na wapenda amani

makoko jumanne

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2015
Posts
584
Reaction score
164
Kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Mbowe ya kuwataka wapiga kura kupiga kura na kulinda kura zao ni ya uchochezi kwa kuwa serikali imeshatoa maelekezo na sheria ya uchaguzi iko wazi.

Lakini pia sheria nyingine kuhusu ulinzi na usalama zinakataza watu kukusanyika bila kubali kuwa ni kosa la jinai hivyo binafsi simuelewi Mbowe dhamira yake hasa katika hili ni nini.

Kweli huyu ni kiongozi wa kuaminiwa anayetaka kuchochea vurugu kwa kuwa vyama vyenye wagombea ni vingi.Je, iweje kila chama kiwaamuru wafuasi wake kukusanyika mita200 kulinda kura zao.Je, hali itakuwaje?

Busara itumike katika hili tupige kura turudi majumbani tuachane na ushabiki.
 
nani asiyemjua mbowe ni msanii? anataka kuvuruga amani tuliyonayo watanzania ..... Ukawa mshaurini mbowe awe na huruma na wananchi
 
Kubali au kataa lakini unafahamu kuwa Mbowe ni mpigadili na yuko pale kimaslai zaidi..yuko tayari hata kuìingiza nchi vitani
Wapiga dili ni wale waliochota feha za ESCROW kwa magunia wewe...na bado wanataka kuiba kura ili waendelee kupiga dili nyingine...this time mmeshikwa pabaya..povu linawatoka,pumzi kwishney!
 
Hofu ya UKAWA ni kuwa, msije na mabox ya kura zilizopigwa tayari na kuyaacha vituoni halafu mkafanya chenjkota ya kuondoka na yale yaliopigiwa kura kihalali!
 
Elton John alianza na tabia kama hii yako.

Angalia usielekee huko.
 
Kwenye kampeni zenu mnatubeba na malori,fuso na ma-uda, tena mnatupa, elfu 10,tisheti na kofia! Kama haitoshi mnawapandisha akina daimondi na ali kiba jukwani ili watu wajae kwa wingi sana!!! Kiasi mnaita wenyewe mafuriko mara gharika! Yani safi hakuna shida amani haiwezi vunjika hapo!

Ajabu tukisha piga kura hamtutaki tena tukae vituoni tusubiri matokeo ya mlichokuwa mkitupigia kampeni! Eti tutahatarisha amani!

HIVI UNAWEZAJE KUISHI NA MKE ASIYE KUPENDA?? LAZIMISHENI MNAVYOWEZA KUTAWALA NCHI HII LAKINI JUENI WANANCHI WENGI HAWAWAPENDI.
 
Hata kwenye kulinda kura na ccm mtakuwepo kama mbwai ba iwe mbwai. Ntalinda kura yangu kupitia dirishani nyumba yangu ipo ndani ya mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.
 
Ungeeleweka kama ungeandika kwamba KAULI YA MBOWE YALAANIWA NA WEZI WA KURA WOTE!
 
popote pale duniani haijawahi tokea wananchi kuhamia vituo vya kupigia kura eti kwa kigezo cha kulinda kura. Kwani mwenye jukumu la kulinda na kuhakikisha uhesabuji wa kura tayari wanafahamika.
 
Yani wewe ni mmoja wa VILAZA ambao mpo wachache sana hapa duniani? Niambie kama mmefanya mkusanyiko na hamjatenda uhalifu wowote ule,mnakuwa mmetenda jinai gani?

Shauri hili lipo mahakamani subiri ukweli tutaujua ndani ya siku chache kabla ya kupiga kura. Uisfikirie kila kitu kinachosemwa na tume au na JK ndio msahafu..
 
Back
Top Bottom