Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko?

Wanabodi,

Hii ni thread ya swali lililotokana na ile kauli ya Kakobe kumtaka rais "Magufuli Atubu", ambayo sasa imekuwa ni kama jambo limezua jambo kwa kauli hiyo kuwaibua watu wanaohoji asili halisi ya rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, baada ya member fulani humu kuibuka na hoja kuwa rais Magufuli na Askofu Kakobe ni watu wamoja, wanajuana vizuri, wote ni watu wa kutoka kijiji kimoja, ni watu wa kabila moja la Waha wa Kakonko. Jee ukweli ni upi?. Jee rais wetu Magufuli ni Msukuma wa Chato, Mhaya wa Wazilankande au ni Muha wa Kakonko?.

Declaration Kuhusu Ukabila
Japo ni bandiko kuhusu ukweli wa asili ya mtu, kuzungumzia asili ya mtu sio ukabila bali hii inaitwa tracing the originality, uki trace the orgin ya asili za makabila mengi ya Tanzania, utashangaa kukuta kumbe makabila ya asili ya Tanzania ni machache, wakiwemo Wasukuma na Wagogo, na makabila ya mikoa ya kati, lakini mengi ya makabila ya Tanzania ni wahamiaji, hivyo watu wote waliokuwepo kwenye ardhi ya Tanganyika kuanzia ile saa 6:00 wa tarehe 9 Desemba, mwaka 1961, ni Watanzania, regardless walizaliwa wapi na asili zao ni wapi, wote tuu Watanzania na tuu wamoja.

Katika bandiko hili pia tutamuangazia kidogo Askofu Kakobe na hoja yake kumtaka rais Magufuli atubu, kama alichofanya ni kitu sahihi au laa!.

Declaration of Interest of Truthfullness
Naomba kuanza na declaration of interest kuwa mimi Paskali Mayalla ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kuu na ya kwanza ya tasnia yetu ya habari ni "seek the truth, and tell nothing but the truth!" ikimaanisha ukweli ndio nguzo kuu ya tasnia ya habari, kazi ya mwandishi wa habari wa ukweli ni kuutafuta tuu ukweli na kuandika ukweli huo au kuusema ukweli bali katika kuusema ukweli, mwandishi sio anatakiwa kuusema tuu ukweli no matter what, bali kuusema ukweli utakaoisaidia jamii na kuleta manufaa, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Declaration of Interest ya Usukuma
Kwa vile mimi kwa kabila ni Msukuma, na kwa vile tayari kuna hoja za ukabila na Usukumanaization kwenye awamu hii ya Magufuli, naomba kudeclare my interest kuwa, siandiki bandiko hili kwa ajili ya Usukuma wangu, wala bandiko hili sio la ukabila, na Wasukuma sio wakabila, bali ni bandiko la kuhoji ukweli wa kabila halisi la kiongozi wetu, kwa nia njema kabisa ya kuwa na info, to be informed, kwa imani kuwa hakuna ubaya wowote kwa raia wowote wa Tanzania, kufahamu ukweli wa kabila halisi la kweli na asili halisi ya kweli ya kiongozi wetu.

Turudi kwenye mada kuu
Jee Rais Magufuli ni Msukuma, Muhaya au Muha wa Kakonko?.
Siku za nyuma kuna member mwingine humu aliwahi kuibuka na kudai kuwa rais Magufuli sii Msikuma bali ni Muhaya, akaibuka hadi na jina lake halisi la Kihaya kuwa anaitwa Katto, tulipomuomba atufafanulie ukweli huu, aliingia mitini, sasa leo huyu Gungele naye anaibuka na hoja yake kuwa rais Magufuli ni Muha wa Kakonko anakotoka Kakobe!, nimemuomba athibitishe, wakati tukisubiri uthibitisho huu, ndipo ninauliza, kuna ubaya wowote, Watanzania tukafahamishwa kwa ukweli halisi usiotia shaka na kwa uwazi, asili halisi ya rais Magufuli, jee rais wetu Dr. John Pombe Magufuli asili yake kabisa ni Kabila gani?.

NB. Hii tabia ya baadhi ya viongozi kubadili makabila na kutumia makabila mengine, haikuanza leo, ilianza tangu enzi za Baba wa Taifa, watu walisema humu, hata Mkapa naye akasemwa ni wa kule..., Edward Lowassa inafahamika wazi kwa wengi kuwa ni Mmasai wa Monduli, but in reality, Lowassa Mmeru, ila wazazi wake ndio walihamia Monduli, akazaliwa Monduli, akakulia Monduli, akalelewa Kimasai na kukua na morani wa kule, kwa kupitia hatua zote ikiwemo initiations, hivyo sasa yeye kweli ni Mmasai.

Hitimisho.
Rais Magufuli ni rais wetu, tumemchagua kwa kura zetu, yeye sio malaika bali ni binadamu tuu kama sisi, na hivyo kuweza kufanya makosa na hata dhambi, ila hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kumhukumu binadamu mwingiwe kuwa ni mdhambi, na sio kumhukumu kuwa ni mdhambi, na katika kuijua asili yake, kuna baadhi ya mambo ni mambo yake ya binafsi, na hatupaswi kuyaulizia ili tusiingilie uhuru wake binafsi, yaani his right to privacy, lakini kuijua asili yake, dini yake, kabila lake sisi as taxpayers, we have the right to know details, his public as well as his private conduct haswa katika determination ya truthfulness, morality, na integrity ambayo ni ethical issue ni sifa kuu muhimu kabisa kuliko sifa zote za kiongozi wa nchi.
Jumatano Njema ya Kufungia Mwaka.
Paskali.
Rejea
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."
Tuhuma za udini, ukanda na ukabila katika teuzi, kama wote wana sifa, kuna tatizo gani?.
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye Ukabila, Tatizo Ndio Walio Wengi!
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na Zile Boeing ni TT, Then Hatufai!.
https://www.jamiiforums.com/threads...edeye-ni-bomu.570208/page-8n-hatufai.1246099/
Update 1
Haya ni baadhi ya majibu ambayo ambayo ni very objective na yana coherence, na kwakutumia uzoefu wangu wangu wa miaka 27 ya uandishi wa habari, naamini haya yasemwayo ni kweli kwa msingi tuu wa hearsay na third party contributions, confirmation itapatikana kutoka kwa ndugu wa karibu, wana ukoo, next of kin or from the horses mouth.






 
Haaaa sawa vipi lakini ukonpoa leo naona umeamka vibaya hujalipwa japo ya post hata moja
Mkuu!, ipo hivi. Hii mada uliyochangia, sio ya leo au jana. Ipo kitambo kidogo. Kwahiyo jamaa alikuwa anashauri ungeangalia muda wa hii mada iliwekwa lini.
 
Kama kweli paschal ni mwandishi basi kama taifa tutegemee nyuzi kama hizi zisizo na maana. Ukabila wenu pelekeni kenye sio Tanzania
 
Umesh
Mkuu!, ipo hivi. Hii mada uliyochangia, sio ya leo au jana. Ipo kitambo kidogo. Kwahiyo jamaa alikuwa anashauri ungeangalia muda wa hii mada iliwekwa lini.
Umeshwahi kufanya rejea ya vitabu mashuleni wakati wa kijibu au kufanya andiko, vile vitabu ji vupya au
 
Kujua Ni msukuma au muha essence yake Ni nini kwa ustawi wa Taifa Hili. Hatuna haja ya kujua Kiongozi wetu Ni wa kabila gani ili mradi anachapa kaxi kuwatumikia Watanzania

Tuna mambo mengi Sana ya kujadili yenye tija kwa Taifa hili.sio kujuana makabila. Mwalimu alipinga Sana Tabia km hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alionywa Sana na viongozi wa dini asitoke nje ya mstari, ye ndo kwanza akilimpa milioni 60 kila mwezi msiba plus ulinzi juu awatukane viongozi wa dini.
Ukiona imefikia hatua hadi viongozi wa dini wanakuonya na still umeshupaza shingo, your a deadman,na ni lazima Mungu uingilia Kati kukata kiburi chako.
Waganga ni watu wabaya Sana ndio wanawamislead vibaya sana watu kwa kuwaamisha uwongo kwamba wanaweza kwenda against nature. Madikteta wote wamedanganywa na waganga, Hakuna dikteta asiye mshirikina sababu ya kuuza nafsi zao kwa shetani ambae uwatumia kisha uwadump. Human soul, spirit and body.
 
Pascal umepandisha uzi huu kwa lengo gani?

Ama leo unataka baada ya kuchambua andiko lako tuhitimishe kwa kusema kuwa Magufuli hakuwa msukuma ili;

1. Ionekane na kuhalalisha kuwa wasukuma ninyi hamna hulka na silka kama alizokuwa nazo Rais Magufuli na pengine jamii sasa isiwanisibishe naye.

2. Kwamba sasa waliokuwa na dhana ya sukumagang waione kuwa haikuwepo bali ni siasa tu!

Haya ni maoni yangu juu ya uzi huu kwa mkitadha wa kurejeshewa kivingine, tofauti na malengo ya awali.

Pascal nisikusemee embu tuambie nini lengo la uzi huu kupandishwa mara ya pili katika kipindi ambacho tayari Hayati Rais Magufuri hayupo ili tujadili tukiwa na "engo"stahiki.
 
Back
Top Bottom