Kauli ya JJ Mnyika: Kwa nini?

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,429
1,045
Nimefuatilia vyombo vya habari Clouds FM na ITV kusikia tena marudio ya kile alichosema JJ moja kwa moja toka kinywani akiwa Bungeni na kikapelekea yeye kutolewa nje ya Bunge bila mafanikio. Sijajua hii ni mpango wa maksudi au bahati mbaya. Inakuwaje wamenukuu sauti ya Ndugai na wanashindwa kurusha sauti ya mkosaji? Usawa uko wapi na kwa nini wasikilizaji na watazamaji hatupewi fursa ya kusikia na kuhukumu wenyewe? Na kwa nini haki aliyopewa supika kusikika wkt akisoma vifungu vya hukumu hapewi JJ kusikika wakati anatenda kosa?

Nisaidieni majibu na mtazamo wenu.
 
Itakuwa wanaogopa hayo maneno aliyotamka juu ya mkuu wa nchi, yasije geuzwa na kuonekana ni vyombo vyao viliyatamka
 
Hata mimi sikusikiliza bunge na hivo niliweka clauds saa kumi na mbili nikitegemea nitasika live ili niburudike ile wakabana. Wao nao ni waoga, they are not strong.
 
Itakuwa wanaogopa hayo maneno aliyotamka juu ya mkuu wa nchi, yasije geuzwa na kuonekana ni vyombo vyao viliyatamka

Mie maneno ya Kamanda Mnyika kuwa jk ni dhaifu nimeyafanya ringtone kwenye simu zangu liwalo na liwe!
 
Nimefuatilia vyombo vya habari Clouds FM na ITV kusikia tena marudio ya kile alichosema JJ moja kwa moja toka kinywani akiwa Bungeni na kikapelekea yeye kutolewa nje ya Bunge bila mafanikio. Sijajua hii ni mpango wa maksudi au bahati mbaya. Inakuwaje wamenukuu sauti ya Ndugai na wanashindwa kurusha sauti ya mkosaji? Usawa uko wapi na kwa nini wasikilizaji na watazamaji hatupewi fursa ya kusikia na kuhukumu wenyewe? Na kwa nini haki aliyopewa supika kusikika wkt akisoma vifungu vya hukumu hapewi JJ kusikika wakati anatenda kosa?

Nisaidieni majibu na mtazamo wenu.

Nenda kwenye chademablog.blogspot.com utasikiliza yote jinsi ilivyokuwa
 
TBC wamemua kukauka kabisa na kutoongelea suala hilo kwenye news bulletin yao ya saa 2 usiku.
Huwa sielewi vipaumbele vya habari vinachambuliwaje.
 
mimi nausubiri saa sita star tv niicheki na nitairekodi nami pia itakuwa calling tone yangu kwenye simu,jj mnyika kafunguka kisawasa wasa i like the man
 
JJ jimbo la Ubungo limemshinda sasa anatafuta umaarufu tu kwenye vyombo vya habari hasa vile vya makanjanja original.
 
Niwezesheni nami iwe ringtone,wamezoea kurembana hapa kazi2 Mnyika tupo nyuma yako,alutaaaa...
 
pole sana kwa kuikosa ile sauti. Mi ningekuwa najua kuiweka kwenye huu mtandao ningekuwekea maana nilirekodi kwenye Pc yangu kwa kutumia Web camera michango ya wabunge wote makni isipokuwa Lusinde na matusi yake.
 
JJ jimbo la Ubungo limemshinda sasa anatafuta umaarufu tu kwenye vyombo vya habari hasa vile vya makanjanja original.

Loo...yaani hadhi ya JF imeshuka hadi imefikia kiwango hiki...inasikitisha! Bornvilla acha utani, kweli Mhe. Mnyika kuliita koleo kwa jina lake ni kutafuta umaarufu? Mhe. Mnyika hakutolewa bungeni kwa kutukana, ametolewa bungeni kwa kusema ukweli kwa sababu ndani ya CCM, ukweli unaogopwa kama ukoma. Udhaifu wa binadamu utabaki kuwa udhaifu tu hata ukipakwa rangi na manukato na tukiacha unafiki, Mhe. Mnyika ni wa kupongezwa kwa ujasiri wake aliouonesha.
 
Last edited by a moderator:

Sure mkuu badala ya kuogopa kumwambia mfalme yuko uchi ni vizuri akaelezwa ili ajitupie japo msuli!!
 
Back
Top Bottom