Kauli ya Balozi Juma Mwapachu kuhusu Lowassa

Kauli ya Balozi Juma Mwapachu kuhusu Lowassa

Azungumzie pia afya ya lowassa, ya mwili sio shida ila ya akili ndio inagusa maisha yetu. Haiwezekani achaguliwe lakini thinking yote ifanywe na watu wa genge.

Huja soma vizuri na kuelewa hoja yenyewe!
Hayo maneno hapo chini ndiyo content zenyewe sasa na mafuriko unayoyaona ni sehemu ya hayo maneno.
Suala hapa ni mwako na mwelekeo wa Demokrasia.

Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu
 
Sio kwamba wameonyesha misimamo yao hadharani bali wao wameonyesha chuki za wazi wazi kwa lowasa. Wangekuwa wakweli wangewachambua wagombea wote tukaona nani anafaa kuiongoza nchi. Wao wamejikita kwa EL tu wengine hawasemwi. Kuna kashifa nyingi lakini wao ni richmond ndio wanaifahamu. Alishasema rich ni maagizo ya wakubwa. Mwapachu hana chuki na john, ndio maana hajamtaja katika maelezo yake.

Mkuu Tukumbuke Siku Zote Ukweli Lazima Utaubeba Upande Mmoja Tu.Mtu Akizungumza Ukweli Ukaubeba Upande Mwingine Huwezi Ukasema Hizo Ni Chuki Mkuu...
 
Ukweli utadhidi kudhihiri, Lowasa ni tajiri inawezekana, mimi sina uhakika ana kiasi gani cha pesa ila ninachojua alianza utumishi miaka mingi nyuma,na hata biashara naambiwa pia alianza zamani na zingine alirithi, sina uhakika........ila kuna mtoto wa Rais anatuhumiwa pia kuwa na utajiri mkubwa wa ghafla, sina uhakika ila yanasemwa, na hata yule Dr wa Mihogo naye aliwahi kutamka siku moja kuwa dogo ana ukwasi wa ajabu wakati kamaliza chuo juzi juzi tu, kaupata wapi huo utajiri.....hili wanazuoni wetu hawalisemi, wala kina polepole hawasemi......hii Nchi imejaa unafiki na chuki za hatari.
Mwapachu anatufungua macho kuwa huko CCM kuna matajiri wa kufa mtu ila hawasemwi, anayeandamwa ni Lowasa.......wasomi jitokezeni muweke ukweli hadharani, hii Nchi inawahitaji sana wakati huu, tena kupita wakati wowote ule.
Mkuu umenena ukweli... tatizo kubwa la wasomi wetu ni unafiki na kuto kuwa wasafi... walio wengi wakipewa madaraka kuna issues wanafanya hv wanakuwa na makandokando yao na kuogopa kutoka ndani ya mfumo wa ccm na serikali yake hata kama wanaona kabisa wananchi wanaonewa au kilicho mbele yao si maslahi ya taifa.... ndo maana msigwa alisema akisimama prof bungeni, mchango wake ni kama mtu wa darasa la 7... sio kwamba hawajui bali prof anakuwa anatetea jambo ambalo haliamini.....
 
Hivi leo tukichambua nani kati yetu ni tajiri zaidi ya Lowassa tutakuwa na viongozi wanao kidhi mategemeo yetu? Kuhusu hili swala la Richmond: Hivi baada ya taarifa ya Tume ya Bunge ya Dr Mwakyembe, Serikali ilitoa majibu. Mbona kwenye tuhuma za Bunge kuhusu Tegeta Escrow imekuwapo taarifa toka kwa Chief Secretary kuhusu suala hilo?

Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kubwa na muono mpya.
Source: Ibrahim Kibopile

Na hapo ndipo Balozi Mwapachu unapokosea, ama kwa makusudi kabisa una-divert attention kutoka kwenye uovu wa kitendo chenyewe cha ufisadi. Ni ngumu kuamini mtu kama wewe, na uzoefu wako wa uongozi tukiwa tukisikia jina lako tangu tukiwa wadogo, eti hii leo unaweza tena bila aibu yoyote kuongea jambo kama hili la kuhalalisha ufisadi eti kwa vile ni mdogo. Watu kama nyinyi mlitakuwa kuwa mfano wa kuongoza njia kutofautisha lipi jema na lipi zuri. Hivi kweli unapofananisha wizi wa Lowassa na wizi wa wengineo, na uka-conclude kwamba ni ni bora wizi wa Lowassa kwa vile alichoiba si kikubwa.. You are comparing "the worse" with "the worst", instead of comparing "the worse" with "the good or better". Nashangaa basi kwa nini basi hukufanya comparison ya wizi wa Lowassa na mtu ambae sio mwizi, sio fisadi na mwenye rekodi nzuri ya utendaji kazi, hapa nikimzungumzia Magufuli? Mimi nina wasiwasi na watu kama wewe na Kingunge, si bure..watu kama nyie na comments kama hizi mnazozitoa za kutetea ufisadi mnachotaka kufanya ni kulisambaratisha taifa letu. Hamtafanikiwa lakini kwani common sense will prevail. Watanzania sio wajinga hivyo..
 
Mtoto wa rais ni mgombea kwenye uchaguzi huu?
Bandiko lako limejaa "sijui/sina uhakika" kibao.
Unaleta 'speculation' tu jamvini.

RZONe anagombea Chalinze kwenye uchaguzi huu
 
Sifahamu vp Huyu Mwapachu atajiita msomi kwa aliondika hapo juu. Maneno yake hayana substance wala rationale behind them.

Balozi Juma Mwapachu ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM.

Mwapachu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel Tanzania.
​

Mhe.Balozi Juma Mwapachu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi zikiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya AfrikaMashariki.

Aliwahi kuwa Balozi Mwakilishi Ufaransa na UNESCO ikijumuisha nchi za Uhispania, Ureno, Tunisia, Morocco na Algeria.

Aidha Mhe. Balozi Juma Mwapachu amekuwa mjumbe wa Bodi mbalimbali hapa nchini na amewahi kushika nyadhifa za juu katika Taasisi za Umma na binafsi. Kwa muda mrefu alikuwa naibu Mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mhe. Balozi Juma Mwapachu amehitimu shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na alikuwa Mtanzania wa kwanza mwenye shahada ya Chuo Kikuu kujiungana Jeshi la Polisi nchini.

Ni mhitimu wa Diploma ya Juu ya Sheria ya Kimataifa, masuala ya Diplomasia ya Kimataifa kutoka chuo kikuu cha Sheria za Kimatatifa na Diplomasia huko New Dehli India.

Mhe.Balozi Juma Mwapachu aliwahi kutunukiwa shahada mbili za heshima ya udaktari wa falsafa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Rwanda, na amewahi kuhariri na kuchapisha majarida na vitabu mbalimbali.

Ukiw mkweli jamani unachukiwa balaa,ila Sofia ujinga wao uone utakavyopendwa,LOWASA RAIS pasukeni kama mnamaind
 
''Lakini huyo huyo Baba wa Taifa alimpenda sana Edward na kumpa madaraka ndani ya CCM na baraza la mawaziri''
Lowassa aliwahi kuwa Waziri kwenye serikali ya Mwl. Nyerere?

Nisaidieni wanazuoni!

Enzi ya mwalimu nakumbuka Lowassa kutumwa kwenda Rome kupokea TUNZO kwa niaba ya mwalimu!!
 
Edward alivumilia na kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde uteuzi wa mgombea wa CCM hapo 2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995.

Wapo wengi wa Tanzania waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na Edward kumwezesha Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa karibu na Edward katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma. Imani yao ilikuwa kwamba pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995.

Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kubwa na muono mpya.

Juma Volter Mwapachu

Source: Ibrahim Kibopile

Nimeguswa!.

Pasco
 
sifahamu vp huyu mwapachu atajiita msomi kwa aliondika hapo juu. Maneno yake hayana substance wala rationale behind them.

wala hatushangai maana hiyo ndio tabia ya wanaccm mtu yeyote akiongea ukweli anaonekana hafai
hivi mmelogwa na nani?
 
Nimeguswa!.

Pasco

Naamini utakua team lowassa,umeguswa nini? hayo makubaliano ni kwa sababu lowassa mwenyewe anajua hakubaliki, na aliona mbali kwa kujua akimbeba mkwele mambo yatakaa sawa,kwamba ataendelea kubaki kwenye system ,yeye always ni mipango tu ya ufisadi,lowassa anajijua ni fisadi na hakubaliki! anachofanya sasa hivi ni Jeuri na dharau kwa wa tz kwa sababu ya pesa zake za ufisadi, anatafuta nini mtu mgonjwa kabisa,hakubaliki analazimisha,fisadi, halafu wazee walioheshimika miaka yote Leo wanajivua nguo hadhalani,hata sijui wamepewa nini, big up mkapa malofa hao.
 
Watu wa CCM mwaka huu lazima mtage.....Ufisadi wa LOWASA ulianza kuujua lini...unamwambia mgonjwa wewe Afya yako ikoje.....!!! Angekuwa hakubaliki kwanini unamwaga maPOVU humu....Haijalishi jamaa ni Fisadi...au Mgonjwa...Majanga mliyosababishia hii nchi...tunasema imetosha....Kivyovyote.... tumeamua Kimchagua Lowasa ili kuwaadabisha nyie GAMBAZ ili mjue NCHI hii hamna hatimiliki nayo
 
Balozi Juma Mwapachu ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM.

Mwapachu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel Tanzania.
​

Mhe.Balozi Juma Mwapachu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi zikiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya AfrikaMashariki.

Aliwahi kuwa Balozi Mwakilishi Ufaransa na UNESCO ikijumuisha nchi za Uhispania, Ureno, Tunisia, Morocco na Algeria.

Aidha Mhe. Balozi Juma Mwapachu amekuwa mjumbe wa Bodi mbalimbali hapa nchini na amewahi kushika nyadhifa za juu katika Taasisi za Umma na binafsi. Kwa muda mrefu alikuwa naibu Mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mhe. Balozi Juma Mwapachu amehitimu shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na alikuwa Mtanzania wa kwanza mwenye shahada ya Chuo Kikuu kujiungana Jeshi la Polisi nchini.

Ni mhitimu wa Diploma ya Juu ya Sheria ya Kimataifa, masuala ya Diplomasia ya Kimataifa kutoka chuo kikuu cha Sheria za Kimatatifa na Diplomasia huko New Dehli India.

Mhe.Balozi Juma Mwapachu aliwahi kutunukiwa shahada mbili za heshima ya udaktari wa falsafa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Rwanda, na amewahi kuhariri na kuchapisha majarida na vitabu mbalimbali.

Kumbe yoote haya ana kabachelor degree tu ndiyo anajiita Mwanazuoni? Kwa maana mtaani kwetu kuna madogo kibao wana bachelor degrees pia nao niwaite Wanazuoni?
 
Kauli ya Barozi Juma Mwapachu Kuhusu Lowassa nimekuwa kimya kwa muda mrefu katika mabadilishano ya fikra kwenye mtandao huu ambao kwa hakika, kwa maoni yangu, haubidi kuwa ni wa fikra pevu zisizo shawishika na misimamo ya 'kimalaya ya siasa'. Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitisha huu mtandao.

Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususa ni baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimamia wapi katika suala hili. Naomba niseme mwanzoni kabisa kwamba nchi yetu hii leo imefikia mahali ambapo wasomi, wanazuoni kama sisi katika mtandao huu, Hatuna budi kujitokeza na kuhesabika tunamuunga nani mkono katika uchaguzi ujao wa Rais wa Tanzania.

Tuwe wakweli na siyo kuendelea kuegemea katika kificho cha 'uhuru' wa wanazuoni katika kutoa maomi na fikra kama vile sisi si wapiga kura au wananchi wanaothamini umuhimu kuhusu uongozi wa nchi yetu. Wakati huo umepitwa na hali halisi ya itikadi na maana muhimu ya uongozi wa Taifa. Sasa, Mimi binafsi, namuuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa.

Yako mengi ambayo kazuliwa huyu ndugu yetu; tunaambiwa tangu 1995 wakati Mwalimu Julius Nyerere alipotamka kwamba 'huyu kijana ninalo faili lake, ana utajiri usiyoelezeka. Ana nyumba kadhaa.' Lakini huyo huyo Baba wa Taifa alimpenda sana Edward na kumpa madaraka ndani ya CCM na baraza la mawaziri. Kama Edward alikuwa 'corrupt' swali ni kwanini Baba wa Taifa hakumchukulia hatua za kisiasa na kisheria?

Kwanini aseme hayo aliyoyasema mwaka 1995 wakati Edward Lowassa alikuwa akiongoza kupendwa ndani ya CCM, ngazi zote na akitarajiwa ndiye angependekezwa kuwa mgombea wa Urais? Jamani, wanazuoni, lazima mtafakari historia na hali halisi ilivyokuwa. Mhe Jakaya Kikwete hakuwa 'the favourite' candidate in 1995.

Na Mwalimu alimtaka Ben Mkapa wakati ule awe Rais. Ilibidi Lowassa atoswe kinamna! Mimi namfahamu Edward, Ninyi mnaujua huo utajiri wake au basi akitoa michango hapa na pale ni pesa zake? Kati yenu mna utajiri zaidi ya Edward. Edward alivumilia na kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde uteuzi wa mgombea wa CCM hapo 2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995.

Wapo wengi wa Tanzania waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na Edward kumwezesha Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa karibu na Edward katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma. Imani yao ilikuwa kwamba pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995.

Hivi leo tukichambua nani kati yetu ni tajiri zaidi ya Lowassa tutakuwa na viongozi wanao kidhi mategemeo yetu? Kuhusu hili swala la Richmond: Hivi baada ya taarifa ya Tume ya Bunge ya Dr Mwakyembe, Serikali ilitoa majibu. Mbona kwenye tuhuma za Bunge kuhusu Tegeta Escrow imekuwapo taarifa toka kwa Chief Secretary kuhusu suala hilo?

Nani aliyejaribu kutoa maelezo ambayo yangemfungisha Lowassa au kumkomboa kwa kitendo chake cha kujiuzuru kisiasa? Badala yake, wanazuoni wenzangu ambao sidhani kama tunazo facts za kutosha tunaendelea kumshutumu Lowassa na kumwona kama vile ni corrupt na kiongozi asiyefaa. It is not fair. Mimi simlaumu Lowassa kujitoa CCM. Ni haki yake na kajieleza vipasavyo kuhusu maamuzi yake.

Je, ni uamuzi wa uroho kuhusu Urais? Jamani, wanazuoni, hivi kweli tumefikia hatua ya kumwona mtu ana uroho wa Urais? Ili awe au afanye nini ambacho sisi tufunge macho, na siyo tu kutoona, bali pia kuto chukua hatua? Ikifikia hapo, basi hatuna Taifa tena!! Taifa letu limebahatika kufika hapa lilipofika mwaka huu. Wengi hatukutarajia kwamba yale ambayo tumekuwa tukitafakari na hata kusali ghafla yameibuka.

Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kubwa na muono mpya.

Juma Volter Mwapachu

Source: Ibrahim Kibopile

Viva Maguufuli...
 
Kumbe yoote haya ana kabachelor degree tu ndiyo anajiita Mwanazuoni? Kwa maana mtaani kwetu kuna madogo kibao wana bachelor degrees pia nao niwaite Wanazuoni?
Huko kwenu kuitwa mwana zuoni hadi uwe na degree ngapi?
 
Back
Top Bottom