Kauli tata ya Mbowe, Lissu kupoteza ubunge

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha upinzania nchini Tanzania Chadema Freeman Mbowe amesema uamuzi wa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai la kutangaza nafasi kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kilichokuwa kikikaliwa na Tundu Lissu kiko wazi halijawatikisa wala kuwakatisha tamaa bali kuzidi kuimarisha dhamira yao ya kushika dola.

Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Tanzania alitoa msimamo huo wa chama leo jumamosi Juni 29,2019 wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika jana Kanda ya Nyasa

Mbowe alisema chama hicho kipo tayari hata kupoteza viti vyake vyote lakini hakitaacha kufanya kwa ajili ya wananchi hivyo amewataka wanachama wa chama hicho kutokuwa na mioyo ya visasi.

"Yaani Spika leo anamfukuza ubunge Tundu Lissu anafikiria tutalia,tunamwambia mheshimiwa spika wacha Lissu chukueni viti vyote hivi , nani ana shida na ubunge , tuna shida na wananchi " alisema Mbowe

"Wanatupa sababu zaidi za kufanya kazi vitu kama hivi haviwezi kutukatisha tamaa,vinatuimarisha katika dhamira yetu,tunafanyiwa uonevu mwingi ndani ya bunge , tunafanyiwa visa vingi .

Hivi visa havituvunji moyo vinatuimarisha"
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai alisema ,"Hasira ya kufukuza wabunge wetu ,hasira ya kutoheshimu mawazo yetu , tutaimaliza kwa kupeleka wabunge wengi kuondoa wingi wa CCM ndani ya bunge na kuiongoza serikali nchi hii"

Mbowe alilalamikia pia Kamati ya Haki ,Kinga na Maadili ya Bunge kwa kushindwa kuwashughulikia wabunge wa upinzani pekee huku ikionekana kushindwa kuwagusa wabunge wa CCM.

"Uonevu huu wanaotufanyia hatuna sababu ya kuwatukana ,tunacheka lakini dhamira ya mioyo yetu inaimarishwa sana kila mbunge angesimma kueleza anafanyiwa nini sijui ingekuwaje" alisema Mbowe.

 
Mbowe anajua mwenye makosa ni Lissu kwa ukaidi wa kutopeleka official information ofisi ya spika na anaonekana anazulula marekani.
 
Kina Lisu & Co walikuwa wanawahamasisha wana CHADEMA kuandamana, wakiwaminisha wananchi kuwa WAKO TAYARI KUFA, au kukaa jela kama Mandela kwa ajili ya wananchi. Lisu kapigwa tu risasi tuwili kakimbia nchi. Mbowe kakaa ndani miezi mitatu, kaufyata...
Hili ni fundisho kwa wananchi kuwa hawa watu hawana dhamira ya dhati ya kuwatumikia kama ambavyo wamekuwa wakijinasibu kwenye majukwaa ya kisiasa. Wapo kwa ajili ya matumbo yao!
 
Back
Top Bottom